Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Ali Muhsen Al-Berwani

Page Number:close

external-link copy
17 : 56

يَطُوفُ عَلَيۡهِمۡ وِلۡدَٰنٞ مُّخَلَّدُونَ

Wakitumikiwa na wavulana wa ujana wa milele, info

Wakiwazungukia kwa kuwakhudumia vijana watakao baki milele hivyo hivyo,

التفاسير:

external-link copy
18 : 56

بِأَكۡوَابٖ وَأَبَارِيقَ وَكَأۡسٖ مِّن مَّعِينٖ

Kwa vikombe na mabirika na bilauri za vinywaji kutoka chemchem safi. info

Nao wamechukua vikombe na mabirika yaliyo jaa vinywaji vya Peponi, na bilauri zenye mvinyo kutoka chemchem zinazo miminika,

التفاسير:

external-link copy
19 : 56

لَّا يُصَدَّعُونَ عَنۡهَا وَلَا يُنزِفُونَ

Hawataumwa kichwa kwa vinywaji hivyo wala hawatoleweshwa. info

Vinywaji hivyo haviwaletei kuumwa kichwa wala kutokwa akili kwa ulevi.

التفاسير:

external-link copy
20 : 56

وَفَٰكِهَةٖ مِّمَّا يَتَخَيَّرُونَ

Na matunda wayapendayo, info

Na matunda ya kila namna wanayo yapenda na wanayo yaona;

التفاسير:

external-link copy
21 : 56

وَلَحۡمِ طَيۡرٖ مِّمَّا يَشۡتَهُونَ

Na nyama za ndege kama wanavyo tamani. info

Na nyama za ndege kama zinavyo tamani nafsi zao.

التفاسير:

external-link copy
22 : 56

وَحُورٌ عِينٞ

Na Mahurulaini, info

Na wanawake wenye macho ya vikombe,

التفاسير:

external-link copy
23 : 56

كَأَمۡثَٰلِ ٱللُّؤۡلُوِٕ ٱلۡمَكۡنُونِ

Walio kama mfano wa lulu zilio hifadhiwa. info

Kama mfano wa lulu zilio hifadhiwa katika chaza, kwa usafi wao na urembo wao.

التفاسير:

external-link copy
24 : 56

جَزَآءَۢ بِمَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Ni malipo kwa waliyo kuwa wakiyatenda. info

Watapewa haya kuwa ni malipo kwa mambo mema waliyo kuwa wakiyatenda duniani.

التفاسير:

external-link copy
25 : 56

لَا يَسۡمَعُونَ فِيهَا لَغۡوٗا وَلَا تَأۡثِيمًا

Humo hawatasikia porojo wala maneno ya dhambi, info

Huko Peponi hawatasikia maneno yasiyo kuwa na maana, wala masimulizi ya kumtia dhambini mwenye kuyasikia.

التفاسير:

external-link copy
26 : 56

إِلَّا قِيلٗا سَلَٰمٗا سَلَٰمٗا

Isipo kuwa maneno ya Salama, Salama. info

Ila watalo sikia ni kauli ya wao kwa wao: Tunakusalimuni kwa Salama.

التفاسير:

external-link copy
27 : 56

وَأَصۡحَٰبُ ٱلۡيَمِينِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلۡيَمِينِ

Na wale wa mkono wa kulia, ni yepi yatakuwa ya wa kuliani? info

Na watu wa mkono wa kulia, hapana ajuaye nini malipo ya watu wa kuliani.

التفاسير:

external-link copy
28 : 56

فِي سِدۡرٖ مَّخۡضُودٖ

Katika mikunazi isiyo na miba, info

Katika miti ya mikunazi iliyo katwa miba yake,

التفاسير:

external-link copy
29 : 56

وَطَلۡحٖ مَّنضُودٖ

Na migomba iliyo pangiliwa, info

Na migomba iliyo pangika na ndizi zake zimepandana juu ya mikungu,

التفاسير:

external-link copy
30 : 56

وَظِلّٖ مَّمۡدُودٖ

Na kivuli kilicho tanda, info

Na kivuli kilicho enea wala hakiondoki,

التفاسير:

external-link copy
31 : 56

وَمَآءٖ مَّسۡكُوبٖ

Na maji yanayo miminika, info

Na maji yanayo miminika karibu yao popote wayatakapo,

التفاسير:

external-link copy
32 : 56

وَفَٰكِهَةٖ كَثِيرَةٖ

Na matunda mengi, info

Na matunda ya namna nyingi na kabila nyingi yasiyo tindikia wakati wowote,

التفاسير:

external-link copy
33 : 56

لَّا مَقۡطُوعَةٖ وَلَا مَمۡنُوعَةٖ

Hayatindikii wala hayakatazwi, info

Wala hazuiwiliwi ayatakayo,

التفاسير:

external-link copy
34 : 56

وَفُرُشٖ مَّرۡفُوعَةٍ

Na matandiko yaliyo nyanyuliwa. info

Na matandiko yaliyo nyanyuliwa ya starehe.

التفاسير:

external-link copy
35 : 56

إِنَّآ أَنشَأۡنَٰهُنَّ إِنشَآءٗ

Hakika Sisi tutawaumba (Mahurulaini) upya, info

Hakika Sisi tulianza kuwaumba Mahurulaini mwanzo,

التفاسير:

external-link copy
36 : 56

فَجَعَلۡنَٰهُنَّ أَبۡكَارًا

Na tutawafanya vijana, info

Na tukawafanya kuwa ni vijana,

التفاسير:

external-link copy
37 : 56

عُرُبًا أَتۡرَابٗا

Wanapendana na waume zao, hirimu moja. info

Wenye kupendwa na waume zao, wenye umri ulio karibiana,

التفاسير:

external-link copy
38 : 56

لِّأَصۡحَٰبِ ٱلۡيَمِينِ

Kwa ajili ya watu wa kuliani. info

Wa tayari kwa neema ya watu wa kuliani.

التفاسير:

external-link copy
39 : 56

ثُلَّةٞ مِّنَ ٱلۡأَوَّلِينَ

Fungu kubwa katika wa mwanzo, info

Watu wa kulia ni wengi katika mataifu yaliyo kwisha tangulia,

التفاسير:

external-link copy
40 : 56

وَثُلَّةٞ مِّنَ ٱلۡأٓخِرِينَ

Na fungu kubwa katika wa mwisho. info

Na kikundi kikubwa katika umma wa Muhammad.

التفاسير:

external-link copy
41 : 56

وَأَصۡحَٰبُ ٱلشِّمَالِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلشِّمَالِ

Na watu wa kushotoni; je ni yepi ya wa kushotoni? info

Na watu wa kushoto, hapana anaye jua nini adhabu ya watu wa kushoto.

التفاسير:

external-link copy
42 : 56

فِي سَمُومٖ وَحَمِيمٖ

Katika upepo wa moto, na maji yanayo chemka, info

Watakuwa kwenye upepo umoto utakao wazunguka, unao penya katika tundu za mwili, na maji yaliyo chemshwa motoni wayanywe na wamiminiwe vichwani,

التفاسير:

external-link copy
43 : 56

وَظِلّٖ مِّن يَحۡمُومٖ

Na kivuli cha moshi mweusi, info

Na katika kivuli cha kiza cheusi cha moshi umoto,

التفاسير:

external-link copy
44 : 56

لَّا بَارِدٖ وَلَا كَرِيمٍ

Si cha kuburudisha wala kustarehesha. info

Hapana ubaridi wa kupunguza joto la hewa, wala huruma ya kuwaletea nafuu wanapo vuta pumzi.

التفاسير:

external-link copy
45 : 56

إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَبۡلَ ذَٰلِكَ مُتۡرَفِينَ

Hakika hao walikuwa kabla ya haya wakiishi maisha ya anasa. info

Hakika hao kabla ya haya walikuwa wamepita kiasi katika kustarehea neema za duniani, wamepumbaa hawataki kumt'ii Mwenyezi Mungu Mtukufu.

التفاسير:

external-link copy
46 : 56

وَكَانُواْ يُصِرُّونَ عَلَى ٱلۡحِنثِ ٱلۡعَظِيمِ

Na walikuwa wakishikilia kufanya madhambi makubwa, info

Na walikuwa wameshikilia daima kufanya dhambi kubwa kabisa, kwani waliapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba kabisa Mwenyezi Mungu hatamfufua aliye kufa.

التفاسير:

external-link copy
47 : 56

وَكَانُواْ يَقُولُونَ أَئِذَا مِتۡنَا وَكُنَّا تُرَابٗا وَعِظَٰمًا أَءِنَّا لَمَبۡعُوثُونَ

Na walikuwa wakisema: Tutakapo kufa na tukawa udongo na mafupa, ati ndio tutafufuliwa? info

Na walikuwa wakisema kwa kukanusha kurejea tena: Ati tutafufuliwa baada ya kwisha kufa, na baadhi ya miili yetu ikisha kuwa udongo na mengine mifupa iliyo chakaa? Ati sisi tutarudishwa tuwe hai mara ya pili?

التفاسير:

external-link copy
48 : 56

أَوَءَابَآؤُنَا ٱلۡأَوَّلُونَ

Au baba zetu wa zamani? info

Ati tutafufuliwa sisi na baba zetu wa zamani walio kwisha kuwa udongo ulio tapanyika na umepotea katika ardhi?

التفاسير:

external-link copy
49 : 56

قُلۡ إِنَّ ٱلۡأَوَّلِينَ وَٱلۡأٓخِرِينَ

Sema: Hakika wa zamani na wa mwisho info

Waambie kwa kuwajibu kukanusha kwao: Hakika wa zamani na wa mwisho, ambao nyinyi ni katika jumla ya hao,

التفاسير:

external-link copy
50 : 56

لَمَجۡمُوعُونَ إِلَىٰ مِيقَٰتِ يَوۡمٖ مَّعۡلُومٖ

Bila ya shaka watakusanywa kwa wakati wa siku maalumu. info

Nyote mtakusanywa katika wakati wa siku malumu, na wala hamtoipita.

التفاسير: