Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis

Page Number:close

external-link copy
30 : 47

وَلَوۡ نَشَآءُ لَأَرَيۡنَٰكَهُمۡ فَلَعَرَفۡتَهُم بِسِيمَٰهُمۡۚ وَلَتَعۡرِفَنَّهُمۡ فِي لَحۡنِ ٱلۡقَوۡلِۚ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ أَعۡمَٰلَكُمۡ

Na lau tungalitaka, ewe Nabii, tungalikuonesha hao watu wenyewe, ukawatambua kwa alama zilizo wazi kwao. Na kwa hakika utawajua kutokana na maneno yao yaliyodhihirika yenye kuonyesha malengo yao. Na kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, hakuna chochote kinachofichamana cha matendo ya wanaomtii wala matendo ya wanaomuasi, na Atamlipa kila mmoja kwa anachostahili. info
التفاسير:

external-link copy
31 : 47

وَلَنَبۡلُوَنَّكُمۡ حَتَّىٰ نَعۡلَمَ ٱلۡمُجَٰهِدِينَ مِنكُمۡ وَٱلصَّٰبِرِينَ وَنَبۡلُوَاْ أَخۡبَارَكُمۡ

Na tutawatahini nyinyi, tena tutawatahini, enyi Waumini, kwa kupambana na maadui wa Mwenyezi Mungu na kupigana nao jihadi mpaka yajitokeze yale Aliyoyajua Mwenyezi Mungu tangu kale, ili tuwatenge watu wa jihadi kati yenu na uvumilivu wa kupigana na maadui wa Mwenyezi Mungu na tuyatahini maneno yenu na matendo yenu, na hapo adhihirike mkweli miongoni mwenu kutokana na mrongo. info
التفاسير:

external-link copy
32 : 47

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَصَدُّواْ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ وَشَآقُّواْ ٱلرَّسُولَ مِنۢ بَعۡدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ ٱلۡهُدَىٰ لَن يَضُرُّواْ ٱللَّهَ شَيۡـٔٗا وَسَيُحۡبِطُ أَعۡمَٰلَهُمۡ

Hakika ya wale waliokataa kuwa Menyezi Mungu Ndiye Mola wa haki Peke Yake Asiye na mshirika, wakawazuia watu na Dini Yake, wakaenda kinyume na Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na wakampiga vita baada ya wao kujiwa na hoja na alama za kuwa yeye ni Nabii kutoka kwa Mwenyezi Mungu, hawataidhuru Dini ya Mwenyezi Mungu kitu chochote na Atayatangua malipo ya matendo yao waliyoyafanya duniani, kwa kuwa wao hawakutaka kwa matendo hayo radhi za Mwenyezi Mungu Aliyetukuka. info
التفاسير:

external-link copy
33 : 47

۞ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُواْ ٱلرَّسُولَ وَلَا تُبۡطِلُوٓاْ أَعۡمَٰلَكُمۡ

Enyi wale mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wakafuata Sheria Zake kivitendo! Mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume katika maamrisho yao na makatazo yao, na msiyatangue malipo ya matendo yenu kwa kukanusha na kufanya maasia. info
التفاسير:

external-link copy
34 : 47

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَصَدُّواْ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ ثُمَّ مَاتُواْ وَهُمۡ كُفَّارٞ فَلَن يَغۡفِرَ ٱللَّهُ لَهُمۡ

Hakika ya wale waliokataa kuwa Mwenyezi Mungu Ndiye Mola wa haki Peke Yake Asiye na mshirika na wakawazuia watu na Dini Yake, kisha wakafa wakiwa katika hali hiyo, Mwenyezi Mungu Hatawasamehe, na Atawapa adhabu ikiwa ndio mateso yao kwa ukanushaji wao, na Atawafedhehesha mbele ya halaiki ya watu. info
التفاسير:

external-link copy
35 : 47

فَلَا تَهِنُواْ وَتَدۡعُوٓاْ إِلَى ٱلسَّلۡمِ وَأَنتُمُ ٱلۡأَعۡلَوۡنَ وَٱللَّهُ مَعَكُمۡ وَلَن يَتِرَكُمۡ أَعۡمَٰلَكُمۡ

Basi msiwe wanyonge, enyi wenye kumuamini Mwenyezi Mugu na Mtume Wake, wa kujiepusha na kupambana na washirikina, mkaogopa kupigana nao na mkawaita kwenye suluhu na masikilizano na hali ya kuwa nyinyi ndio wenye ushindi na nguvu juu yao, na Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Yuko pamoja na nyinyi kwa kuwanusuru na kuwapa nguvu. Hapa kuna bishara kubwa ya kupatiwa ushindi na kusaidiwa juu ya maadui. Na Mwenyezi Mungu Hatawapunguzia nyinyi malipo mema ya matendo yenu. info
التفاسير:

external-link copy
36 : 47

إِنَّمَا ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَا لَعِبٞ وَلَهۡوٞۚ وَإِن تُؤۡمِنُواْ وَتَتَّقُواْ يُؤۡتِكُمۡ أُجُورَكُمۡ وَلَا يَسۡـَٔلۡكُمۡ أَمۡوَٰلَكُمۡ

Hakika uhai wa duniani ni mchezo na udanganyifu. Na mtakapomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkamuogopa Mwenyezi Mungu kwa kutekeleza mambo Aliyoyafanya ni ya lazima na kujiepusha na mambo ya kumuasi, Atawapa malipo mema ya matendo yenu, na Hatawataka myatoe mali yenu yote katika Zaka, Anachowataka mfanye ni mtoe sehemo ya hayo mali. info
التفاسير:

external-link copy
37 : 47

إِن يَسۡـَٔلۡكُمُوهَا فَيُحۡفِكُمۡ تَبۡخَلُواْ وَيُخۡرِجۡ أَضۡغَٰنَكُمۡ

Akiwa Atawataka myatoe mali yenu na Akawa Atawakariria na kuwasumbua, mtayafanyia uchoyo na mtakataa kuyatoa, na hapo Atakapowataka myatoe mali yenu Atayatoa nje machukivu yaliyo ndani ya nyoyo zenu. info
التفاسير:

external-link copy
38 : 47

هَٰٓأَنتُمۡ هَٰٓؤُلَآءِ تُدۡعَوۡنَ لِتُنفِقُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ فَمِنكُم مَّن يَبۡخَلُۖ وَمَن يَبۡخَلۡ فَإِنَّمَا يَبۡخَلُ عَن نَّفۡسِهِۦۚ وَٱللَّهُ ٱلۡغَنِيُّ وَأَنتُمُ ٱلۡفُقَرَآءُۚ وَإِن تَتَوَلَّوۡاْ يَسۡتَبۡدِلۡ قَوۡمًا غَيۡرَكُمۡ ثُمَّ لَا يَكُونُوٓاْ أَمۡثَٰلَكُم

Haya nyini, enyi Waumini, mnaitwa kutoa kwenye kupigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu na kuinusuru Dini Yake. Basi miongoni mwenu kuna anayefanya uchoyo kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu. Na mwenye kufanya uchoyo huwa anajifanyia uchoyo nafsi yake. Na Mwenyezi Munmgu, Aliyetukuka, Ndiye Mkwasi wa kutowahitajia nyinyi, na nyinyi ndio mnaomhitajia Yeye. Na mkipa mgongo mkaacha kumuamini Mwenyezi Mungu na kufuata amri Zake, Atawaangamiza na Atawaleta watu wengine, na kisha wasiwe ni kama nyinyi katika kuzipa mgongo amri za Mwenyzi Mungu, bali wao watamtii Yeye na kumtii Mtume Wake na watapigana jihadi katika njia Yake kwa mali yao na nafsi zao. info
التفاسير: