Übersetzung der Bedeutungen von dem heiligen Quran - Die Übersetzung in Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani.

Nummer der Seite:close

external-link copy
60 : 23

وَٱلَّذِينَ يُؤۡتُونَ مَآ ءَاتَواْ وَّقُلُوبُهُمۡ وَجِلَةٌ أَنَّهُمۡ إِلَىٰ رَبِّهِمۡ رَٰجِعُونَ

Na wale ambao wanatoa walicho pewa, na hali nyoyo zao zinagopa kwa kuwa watarejea kwa Mola wao Mlezi, info

Na wale ambao wanatoa katika vile anavyo waruzuku Mwenyezi Mungu, na wanafanya a'mali yao na hali wao wana khofu wasifanye taksiri, kwa sababu bila ya shaka wao ni wenye kurejea kwa Mwenyezi Mungu kwa kufufuliwa na watahisabiwa,

التفاسير:

external-link copy
61 : 23

أُوْلَٰٓئِكَ يُسَٰرِعُونَ فِي ٱلۡخَيۡرَٰتِ وَهُمۡ لَهَا سَٰبِقُونَ

Basi wote hao ndio wanao kimbilia katika mambo ya kheri, na ndio watakao tangulia kuyafikia. info

Hao wote hukimbilia na a'mali zao kuendea kupata kheri, na wao ni wenye kuwatangulia wengineo katika kupata huko.

التفاسير:

external-link copy
62 : 23

وَلَا نُكَلِّفُ نَفۡسًا إِلَّا وُسۡعَهَاۚ وَلَدَيۡنَا كِتَٰبٞ يَنطِقُ بِٱلۡحَقِّ وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ

Na hatuilazimishi nafsi ila kwa kadri ya uwezo wake. Na tunacho kitabu kisemacho kweli. Nao hawatadhulumiwa. info

Na Sisi hatumlazimishi mtu yeyote ila kwa analo liweza kulifanya, kwa sababu limo ndani ya makdara yake. Na kila a'mali katika a'mali za waja zimesajiliwa kwetu katika kitabu, na tutawapa khabari zake kama zilivyo. Na wao hawatadhulumiwa kwa kuongezewa adhabu wala kupunguziwa thawabu.

التفاسير:

external-link copy
63 : 23

بَلۡ قُلُوبُهُمۡ فِي غَمۡرَةٖ مِّنۡ هَٰذَا وَلَهُمۡ أَعۡمَٰلٞ مِّن دُونِ ذَٰلِكَ هُمۡ لَهَا عَٰمِلُونَ

Lakini nyoyo zao zimeghafilika na hayo, na wanavyo vitendo vinginevyo wanavyo vifanya. info

Lakini makafiri kwa sababu ya inadi yao na chuki zao ni wenye kughafilika na kufanya kheri, na kujikalifu kufanya liwezekanalo, na kwamba kuna hisabu ya kuchungua kila kitu. Na mbali na hayo bado wanavyo vitendo vingine viovu wanavyo dumu navyo.

التفاسير:

external-link copy
64 : 23

حَتَّىٰٓ إِذَآ أَخَذۡنَا مُتۡرَفِيهِم بِٱلۡعَذَابِ إِذَا هُمۡ يَجۡـَٔرُونَ

Hata tutakapo watia katika adhabu wale walio dekezwa kwa starehe kati yao, hapo ndipo watapo yayatika. info

Na Sisi tunapo wapatiliza adhabu matajiri wenye kudeka katika starehe zao hupiga makelele na wakayayatika kuomba msaada.

التفاسير:

external-link copy
65 : 23

لَا تَجۡـَٔرُواْ ٱلۡيَوۡمَۖ إِنَّكُم مِّنَّا لَا تُنصَرُونَ

Msiyayatike leo! Hakika nyinyi hamtanusurika nasi. info

Basi tunawaambia: Msiyayatike, wala msiombe msaada hivi sasa. Hamtatoka ndani ya adhabu yangu, wala kuyayatika kwenu hakufai kitu.

التفاسير:

external-link copy
66 : 23

قَدۡ كَانَتۡ ءَايَٰتِي تُتۡلَىٰ عَلَيۡكُمۡ فَكُنتُمۡ عَلَىٰٓ أَعۡقَٰبِكُمۡ تَنكِصُونَ

Hakika zilikuwa Aya zangu mkisomewa, nanyi mkirudi nyuma juu ya visigino vyenu, info

Hamna udhuru. Kwani Aya zangu zenye kuteremshwa kwa wahyi zilikuwa mkisomewa, nanyi mkizipuuza kwa mapuuza yenye kugeuza hali zenu, na wala hamkuzisadiki, wala hamkuzifuata kwa vitendo.

التفاسير:

external-link copy
67 : 23

مُسۡتَكۡبِرِينَ بِهِۦ سَٰمِرٗا تَهۡجُرُونَ

Na huku mkitakabari na usiku mkiizungumza (Qur'ani) kwa dharau. info

Na nyinyi katika mapuuza yenu mlikuwa mnatakabari na mnafanyia maskhara, mkiutaja huu Wahyi kwa sifa mbaya mnapo kutana katika taanusi zenu za usiku.

التفاسير:

external-link copy
68 : 23

أَفَلَمۡ يَدَّبَّرُواْ ٱلۡقَوۡلَ أَمۡ جَآءَهُم مَّا لَمۡ يَأۡتِ ءَابَآءَهُمُ ٱلۡأَوَّلِينَ

Je, hawakuifikiri kauli, au yamewajia yasiyo wafikia baba zao wa zamani? info

Je! Hawa wenye kupuuza wamekuwa wajinga hata hawakuizingatia Qur'ani wakaijua kwamba hii hakika ni Haki? Au huu wito wa Muhammad kwao umekuwa ni namna mbali kuliko walio kuja nayo Mitume wengine kwa kaumu zilizo kwisha tangulia walio ambao baba zao waliwawahi?

التفاسير:

external-link copy
69 : 23

أَمۡ لَمۡ يَعۡرِفُواْ رَسُولَهُمۡ فَهُمۡ لَهُۥ مُنكِرُونَ

Au hawakumjua Mtume wao, ndio maana wanamkataa? info

Au hawamjui Mtume wao Muhammad aliye kulia kati yao katika tabia zake tukufu ambazo hazijapata kuwa na uwongo, na wao hivi sasa wanaukataa wito wake kwa dhulma na husda.

التفاسير:

external-link copy
70 : 23

أَمۡ يَقُولُونَ بِهِۦ جِنَّةُۢۚ بَلۡ جَآءَهُم بِٱلۡحَقِّ وَأَكۡثَرُهُمۡ لِلۡحَقِّ كَٰرِهُونَ

Au wanasema: Ana wazimu? Bali amewajia kwa Haki, na wengi wao wanaichukia Haki. info

Au wanasema kuwa huyu ni mwendawazimu? Hasha! Huyu hakika kawaletea Dini ya Haki, na wengi wao wanaichukia haki, kwani hiyo ni kinyume na matamanio yao na mapenzi yao, basi kwa hivyo hawamuamini.

التفاسير:

external-link copy
71 : 23

وَلَوِ ٱتَّبَعَ ٱلۡحَقُّ أَهۡوَآءَهُمۡ لَفَسَدَتِ ٱلسَّمَٰوَٰتُ وَٱلۡأَرۡضُ وَمَن فِيهِنَّۚ بَلۡ أَتَيۡنَٰهُم بِذِكۡرِهِمۡ فَهُمۡ عَن ذِكۡرِهِم مُّعۡرِضُونَ

Na lau kuwa Haki ingeli fuata matamanio yao, basi zingeli haribika mbingu na ardhi na waliomo ndani. Bali tumewaletea ukumbusho wao, nao wanajitenga mbali na ukumbusho wao. info

Ingeli kuwa Haki inafuata matamanio yao ufisadi ungeli enea ulimwenguni, na hawa za nafsi zingeli pambana wenyewe kwa wenyewe. Lakini Sisi tumewapelekea Qur'ani ambayo inawakumbusha haki ambayo inapasa wote wajumuike juu yake. Na juu ya hivyo wao wanayapuuza hayo. "Na lau kuwa Haki ingeli fuata matamanio yao, basi zingeli haribika mbingu na ardhi na waliomo ndani. Bali tumewaletea ukumbusho wao, nao wanajitenga mbali na ukumbusho wao." Hilo neno "Haki" ni tamko lenye maana kadhaa. Huweza kuwa maana yake ni "Mwenyezi Mungu" Subhanahu wa Taa'la , mfano wa kauli yake Mtukufu: "Ametukuka Mwenyezi Mungu wa Haki". Pengine huwa maana yake ni "Qur'ani" , kwa mfano :"Hakika Sisi tumekutuma kwa Haki". Na huenda kukusudiwa "Dini yote", yaani miongoni mwake ni Qur'ani na Sunna (Hadithi) Sahihi, mfano wa kauli yake: "Na sema: Imekuja Haki na uwongo umetoweka". Na iliyo dhaahiri katika tamko la Haki hapa ni kuwa makusudio yake ni ile maana ya kwanza, yaani "Mwenyezi Mungu" Aliye takasika na kutukuka. Na kwa hivyo maana iliyo kusudiwa na Aya ni: Lau kuwa mwenendo wa Mwenyezi Mungu unafuatana na watakayo na wanayo yapendekeza makafiri mpango usingeli bakia katika hali iliyo simamia shani ya mpango wa mbingu na ardhi na wa viumbe viliomo ndani yake. Lakini Mwenyezi Mungu Mwenye hikima kuu na uwezo wa kutenda na ujuzi wake ulio enea kwa viumbe vyake na hikima yake ikadhamini kwa mpango madhubuti, na Qur'ani kusema kwa uwazi ya kwamba mbingu zina viumbe, anatuelekeza tufahamu: Kwanza kuwa Kuamini hayo kwa jumla ni yakini, tuache tafsili yake mpaka apendavyo Mwenyezi Mungu Subhanahu kuidhihirisha kwa kuambatana na kauli yake: "Tutawaonyesha Ishara zetu angani na katika nafsi zao." Pili: Anatuelekeza kwenye utafiti wa kisayansi kama tunaweza "kwani kufikilia hakika hii inatutilia nguvu Imani yetu. Na Imani ndiyo lengo muhimu katika kuelekea kwetu kwenye Ishara hizo."

التفاسير:

external-link copy
72 : 23

أَمۡ تَسۡـَٔلُهُمۡ خَرۡجٗا فَخَرَاجُ رَبِّكَ خَيۡرٞۖ وَهُوَ خَيۡرُ ٱلرَّٰزِقِينَ

Au unawaomba ujira? Lakini ujira wa Mola wako Mlezi ni bora, na Yeye ndiye Mbora wa wanao ruzuku. info

Kwani, ewe Nabii! Unawataka ujira kwa huku kufikisha kwako ujumbe? Hayakuwa hayo! Kwa kuwa ujira hakika ujira wa Mola wako Mlezi ni bora zaidi kuliko walio nao wao; na Yeye ndiye Mbora wa kutoa.

التفاسير:

external-link copy
73 : 23

وَإِنَّكَ لَتَدۡعُوهُمۡ إِلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ

Na kwa yakini wewe unawaita kwenye Njia Iliyo Nyooka. info

Na hakika wewe, ewe Muhammad, hapana shaka yoyote unawaitia Dini ambayo ndiyo Njia Iliyo Nyooka yenye kupelekea Uwokovu.

التفاسير:

external-link copy
74 : 23

وَإِنَّ ٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ عَنِ ٱلصِّرَٰطِ لَنَٰكِبُونَ

Na hakika wale wasio iamini Akhera wanajitenga na Njia hiyo. info

Na hakika hao wasio iamini Akhera na yalioko huko ya Pepo au Moto wanaiacha Njia Iliyo Nyooka inayo mhifadhi mpitaji wakaishika njia ya ubabaishi na misukosuko na ufisadi.

التفاسير: