Übersetzung der Bedeutungen von dem heiligen Quran - Die Übersetzung in Swahili

Nummer der Seite:close

external-link copy
51 : 5

۞ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَتَّخِذُواْ ٱلۡيَهُودَ وَٱلنَّصَٰرَىٰٓ أَوۡلِيَآءَۘ بَعۡضُهُمۡ أَوۡلِيَآءُ بَعۡضٖۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمۡ فَإِنَّهُۥ مِنۡهُمۡۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلظَّٰلِمِينَ

Enyi mlioamini, msiwafanye Mayahudi na Wanaswara ni washirika na wasaidizi wenu juu ya watu wa Imani. Hii ni kwa kuwa wao hawawapendi Waumini. Mayahudi wanasaidiana wao kwa wao, na hivyo hivyo ndivyo walivyo Wanaswara. Na makundi yote mawili yanakutana kwenye kuwafanyia nyinyi uadui. Na nyinyi, enyi Waumini, mnafaa zaidi kusaidiana nyinyi kwa nyinyi. Na yoyote mwenye kuwategemea wao katika nyinyi, basi yeye atakuwa ni miongoni mwao, na hukumu yake ni yao. Mwenyezi Mungu Hatawaafikia madhalimu wanaowategemea makafiri. info
التفاسير:

external-link copy
52 : 5

فَتَرَى ٱلَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٞ يُسَٰرِعُونَ فِيهِمۡ يَقُولُونَ نَخۡشَىٰٓ أَن تُصِيبَنَا دَآئِرَةٞۚ فَعَسَى ٱللَّهُ أَن يَأۡتِيَ بِٱلۡفَتۡحِ أَوۡ أَمۡرٖ مِّنۡ عِندِهِۦ فَيُصۡبِحُواْ عَلَىٰ مَآ أَسَرُّواْ فِيٓ أَنفُسِهِمۡ نَٰدِمِينَ

Mwenyezi Mungu Anasimulia habari ya kikundi cha wanafiki kwamba wao walikuwa wakikimbilia kupendana na Mayahudi kwa kuwa ndani ya nyoyo zao mulikuwa na shaka na unafiki, na walikuwa wakisema, «Sisi tunapendana nao kwa kuogopa wasije wakawashinda Waislamu wakatudhuru sisi pamoja na wao.» Mwenyezi Mungu, uliotukuka utajo Wake, Anasema: Huenda Mwenyezi Mungu Akauleta ushindi- yaani ushindi wa kuukomboa mji wa Makkah-, Akamnusuru Nabii Wake na Akaupa nguvu Uislamu na Waislamu juu ya makafiri au Akatayarisha mambo ambayo yataifanya iyondoke nguvu ya Mayahudi na Wanaswara, na hapo waje wawanyenyekee Waislamu. Wakati huo watajuta wanafiki kwa yale waliyoyaficha kwenye nafsi zao ya kuwategemea Mayahudi na Wanaswara. info
التفاسير:

external-link copy
53 : 5

وَيَقُولُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَهَٰٓؤُلَآءِ ٱلَّذِينَ أَقۡسَمُواْ بِٱللَّهِ جَهۡدَ أَيۡمَٰنِهِمۡ إِنَّهُمۡ لَمَعَكُمۡۚ حَبِطَتۡ أَعۡمَٰلُهُمۡ فَأَصۡبَحُواْ خَٰسِرِينَ

Wakati huo watasema baadhi ya Waumini kuwaambia wengine, wakionea ajabu hali ya wanafiki, pindi mambo yao yatakapofichuka, «Je, hawa ndio wale ambao waliapa viapo vizito kwamba wao wako nasi?» Zimebatilika amali za wanafiki walizozifanya ulimwenguni, hawana malipo mema ya amali hizo, kwa kuwa wao walizifanya bila ya Imani. Hapo basi, wamepata hasara ya ulimwenguni na Akhera. info
التفاسير:

external-link copy
54 : 5

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَن يَرۡتَدَّ مِنكُمۡ عَن دِينِهِۦ فَسَوۡفَ يَأۡتِي ٱللَّهُ بِقَوۡمٖ يُحِبُّهُمۡ وَيُحِبُّونَهُۥٓ أَذِلَّةٍ عَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ أَعِزَّةٍ عَلَى ٱلۡكَٰفِرِينَ يُجَٰهِدُونَ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَلَا يَخَافُونَ لَوۡمَةَ لَآئِمٖۚ ذَٰلِكَ فَضۡلُ ٱللَّهِ يُؤۡتِيهِ مَن يَشَآءُۚ وَٱللَّهُ وَٰسِعٌ عَلِيمٌ

Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkazifuata sheria zake kivitendo, Yoyote kati yenu atakayerudi nyuma akaiacha Dini yake, na akachukua badala yake dini ya Kiyahudi au ya Kinaswara au dini nyengineyo, basi hao hawatamdhuru Mwenyezi Mungu chochote; na Atawaleta watu bora kuliko wao: Anaowapenda na wanaompenda, wenye huruma kwa Waumini, wakali kwa makafiri, wanapigana jihadi na maadui wa Mwenyezi Mungu na hawamuogopi, kwa kumridhisha Mwenyezi Mungu, yoyote. Kuneemeshwa huko ni miongoni mwa nyongeza za Mwenyezi Mungu anazompa Amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mkunjufu wa fadhila, ni Mjuzi wa anayestahiki fadhila Zake katika waja Wake. info
التفاسير:

external-link copy
55 : 5

إِنَّمَا وَلِيُّكُمُ ٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱلَّذِينَ يُقِيمُونَ ٱلصَّلَوٰةَ وَيُؤۡتُونَ ٱلزَّكَوٰةَ وَهُمۡ رَٰكِعُونَ

Hakika msaidizi wenu , enyi Waumini, ni Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na Waumini wanaojilazimisha na Swala za faradhi na wanatekeleza Zaka kwa hiari yao na hali wao ni wanyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
56 : 5

وَمَن يَتَوَلَّ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ فَإِنَّ حِزۡبَ ٱللَّهِ هُمُ ٱلۡغَٰلِبُونَ

Na mwenye kushikamana na Mwenyezi Mungu na akafuata muongozo wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na akawa na muelekeo wa Waumini, basi yeye ni katika kundi la Mwenyezi Mungu, na kundi la Mwenyezi Mungu ndilo la washindi wenye kunusurika. info
التفاسير:

external-link copy
57 : 5

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَتَّخِذُواْ ٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُواْ دِينَكُمۡ هُزُوٗا وَلَعِبٗا مِّنَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ مِن قَبۡلِكُمۡ وَٱلۡكُفَّارَ أَوۡلِيَآءَۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ

Enyi ambao mlimuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkafuata sheria Yake kivitendo, msiwafanye wale wanaoifanyia shere na kuichezea Dini yenu, miongoni mwa waliopewa Vitabu na makafiri, kuwa ni wasimamizi wa mambo yenu. Na muogopeni Mwenyezi Mungu mkiwa nyinyi mnamuamini Yeye na mnaziamini sheria Zake. info
التفاسير: