Übersetzung der Bedeutungen von dem heiligen Quran - Die Übersetzung in Swahili

external-link copy
53 : 5

وَيَقُولُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَهَٰٓؤُلَآءِ ٱلَّذِينَ أَقۡسَمُواْ بِٱللَّهِ جَهۡدَ أَيۡمَٰنِهِمۡ إِنَّهُمۡ لَمَعَكُمۡۚ حَبِطَتۡ أَعۡمَٰلُهُمۡ فَأَصۡبَحُواْ خَٰسِرِينَ

Wakati huo watasema baadhi ya Waumini kuwaambia wengine, wakionea ajabu hali ya wanafiki, pindi mambo yao yatakapofichuka, «Je, hawa ndio wale ambao waliapa viapo vizito kwamba wao wako nasi?» Zimebatilika amali za wanafiki walizozifanya ulimwenguni, hawana malipo mema ya amali hizo, kwa kuwa wao walizifanya bila ya Imani. Hapo basi, wamepata hasara ya ulimwenguni na Akhera. info
التفاسير: