Prijevod značenja časnog Kur'ana - Prijevod na svahili jezik: Alija Muhsin el-Bervani.

Broj stranice:close

external-link copy
9 : 69

وَجَآءَ فِرۡعَوۡنُ وَمَن قَبۡلَهُۥ وَٱلۡمُؤۡتَفِكَٰتُ بِٱلۡخَاطِئَةِ

Na Firauni na walio mtangulia, na miji iliyo pinduliwa chini juu, walileta khatia. [9] info

[9] Akaja Firauni, na mataifa mengine yaliyo kufuru kabla yake, na wale jamaa walio acha mwendo wa haki na vitendo vya maumbile wakafanya vitendo vichafu kabisa hata miji yao ikapinduliwa juu chini.

التفاسير:

external-link copy
10 : 69

فَعَصَوۡاْ رَسُولَ رَبِّهِمۡ فَأَخَذَهُمۡ أَخۡذَةٗ رَّابِيَةً

Wakamuasi Mtume wa Mola wao Mlezi, ndipo Yeye Mola akawakamata kwa mkamato ulio zidi nguvu. [10] info

[10] Kila umma katika hawa walimuasi Mtume wa Mola wao Mlezi. Naye Mwenyezi Mungu akawashika kwa kuwaadhibu kwa mshiko ulio zidi ukali.

التفاسير:

external-link copy
11 : 69

إِنَّا لَمَّا طَغَا ٱلۡمَآءُ حَمَلۡنَٰكُمۡ فِي ٱلۡجَارِيَةِ

Maji yalipo furika Sisi tulikupandisheni katika safina, [11] info

[11] Maji yalipo zidi ukomo wake, na yakapanda juu ya milima katika tukio la tofani ya Nuhu, Sisi tulikupandisheni, yaani kwa kuwapandisha wazee wenu wa asli, katika safina inayo kwenda baharini.

التفاسير:

external-link copy
12 : 69

لِنَجۡعَلَهَا لَكُمۡ تَذۡكِرَةٗ وَتَعِيَهَآ أُذُنٞ وَٰعِيَةٞ

Ili tuyafanye hayo kuwa ni waadhi kwenu na kila sikio linalo sikia liyahifadhi. [12] info

[12] Ili kulifanya tukio hilo la kuwaokoa Waumini na kuwazamisha makafiri liwe zingatio na mawaidha kwenu, na lihifadhiwe na kila sikio lenye kuhifadhi linalo sikia.

التفاسير:

external-link copy
13 : 69

فَإِذَا نُفِخَ فِي ٱلصُّورِ نَفۡخَةٞ وَٰحِدَةٞ

. Na litapo pulizwa barugumu mpulizo mmoja tu, [13] info

[13] Litakapo pulizwa barugumu kwa mpulizo mmoja,

التفاسير:

external-link copy
14 : 69

وَحُمِلَتِ ٱلۡأَرۡضُ وَٱلۡجِبَالُ فَدُكَّتَا دَكَّةٗ وَٰحِدَةٗ

Na ardhi na milima ikaondolewa, na ikavunjwa kwa mvunjo mmoja, [14] info

[14] Na ardhi na milima ikaondolewa pahala ilipo, na ikavunjwa mara moja,

التفاسير:

external-link copy
15 : 69

فَيَوۡمَئِذٖ وَقَعَتِ ٱلۡوَاقِعَةُ

Siku hiyo ndio Tukio litatukia. [15] info

[15] Siku hiyo ndiyo kitashuka cha kushuka,

التفاسير:

external-link copy
16 : 69

وَٱنشَقَّتِ ٱلسَّمَآءُ فَهِيَ يَوۡمَئِذٖ وَاهِيَةٞ

Na mbingu zitapasuka, kwani siku hiyo zitakuwa dhaifu kabisa. [16] info

[16] Na mbingu zitapasuka kwa kuondoka hukumu zake na sharia zake, kwani siku hiyo zitakuwa dhaifu baada ya kuwa madhubuti zenye nguvu.

التفاسير:

external-link copy
17 : 69

وَٱلۡمَلَكُ عَلَىٰٓ أَرۡجَآئِهَاۚ وَيَحۡمِلُ عَرۡشَ رَبِّكَ فَوۡقَهُمۡ يَوۡمَئِذٖ ثَمَٰنِيَةٞ

Na Malaika watakuwa pembezoni mwa mbingu; na wanane juu ya hawa watakuwa wamebeba Kiti cha Enzi cha Mola wako Mlezi. [17] info

[17] Na Malaika pembezoni mwake, na wapo Malaika wanane siku hiyo watakao beba Kiti cha Enzi cha Mola wako Mlezi, juu ya Malaika hawa wengine.

التفاسير:

external-link copy
18 : 69

يَوۡمَئِذٖ تُعۡرَضُونَ لَا تَخۡفَىٰ مِنكُمۡ خَافِيَةٞ

Siku hiyo mtahudhurishwa - haitafichika siri yoyote yenu. [18] info

[18] Siku hiyo ndio mtaletwa kwa ajili ya kuhisabiwa. Wala haifichikani siri yenu yoyote mliyo kuwa mkiificha.

التفاسير:

external-link copy
19 : 69

فَأَمَّا مَنۡ أُوتِيَ كِتَٰبَهُۥ بِيَمِينِهِۦ فَيَقُولُ هَآؤُمُ ٱقۡرَءُواْ كِتَٰبِيَهۡ

Basi ama atakaye pewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, atasema: Haya someni kitabu changu! [19] info

[19] Ama mwenye kupewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, atasema akiwatangazia furaha yake walio karibu naye: Chukueni msome kitabu changu!

التفاسير:

external-link copy
20 : 69

إِنِّي ظَنَنتُ أَنِّي مُلَٰقٍ حِسَابِيَهۡ

Hakika nalijua ya kuwa nitapokea hisabu yangu. [20] info

[20] Mimi nilikuwa na yakini tangu duniani kuwa nitapata hisabu yangu, basi nikajitayarisha nafsi yangu kwa mkutano huu.

التفاسير:

external-link copy
21 : 69

فَهُوَ فِي عِيشَةٖ رَّاضِيَةٖ

Basi yeye atakuwa katika maisha ya kupendeza, [21] info

[21] Basi huyo atakuwa katika maisha yaliyo enea kupendeza.

التفاسير:

external-link copy
22 : 69

فِي جَنَّةٍ عَالِيَةٖ

Katika Bustani ya juu, [22] info

[22] Katika Bustani ya pahali na daraja ya juu.

التفاسير:

external-link copy
23 : 69

قُطُوفُهَا دَانِيَةٞ

Matunda yake yakaribu. [23] info

[23] Matunda yake yakaribu kwa kuyachuma. (kuyatunda).

التفاسير:

external-link copy
24 : 69

كُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ هَنِيٓـَٔۢا بِمَآ أَسۡلَفۡتُمۡ فِي ٱلۡأَيَّامِ ٱلۡخَالِيَةِ

Waambiwe: Kuleni na mnywe kwa furaha kwa sababu ya mlivyo tanguliza katika siku zilizo pita. [24] info

[24] Kuleni na mnywe kwa kula na kunywa kusio na karaha, wala maudhi, kwa sababu ya vitendo vyema mlivyo kwisha vitanguliza katika siku za duniani zilizo pita.

التفاسير:

external-link copy
25 : 69

وَأَمَّا مَنۡ أُوتِيَ كِتَٰبَهُۥ بِشِمَالِهِۦ فَيَقُولُ يَٰلَيۡتَنِي لَمۡ أُوتَ كِتَٰبِيَهۡ

Na ama atakaye pewa kitabu chake katika mkono wake wa kushoto, basi yeye atasema: Laiti nisingeli pewa kitabu changu! [25] info

[25] Ama mwenye kupewa kitabu chake kwa mkono wake wa kushoto atasema kwa majuto na huzuni: Laiti kuwa sikupewa kitabu changu,

التفاسير:

external-link copy
26 : 69

وَلَمۡ أَدۡرِ مَا حِسَابِيَهۡ

Wala nisingeli jua nini hisabu yangu. [26] info

[26] Wala sikuijua hisabu yangu!

التفاسير:

external-link copy
27 : 69

يَٰلَيۡتَهَا كَانَتِ ٱلۡقَاضِيَةَ

Laiti mauti ndiyo yangeli kuwa ya kunimaliza kabisa. [27] info

[27] Laiti kuwa kule kufa niliko kwisha kufa kungeli kuwa ndio kumalizika kwangu kwa mwisho, wala nisingeli fufuliwa tena!

التفاسير:

external-link copy
28 : 69

مَآ أَغۡنَىٰ عَنِّي مَالِيَهۡۜ

Mali yangu hayakunifaa kitu. [28] info

[28] Hapana chochote nilicho kimiliki duniani kilicho nifaa.

التفاسير:

external-link copy
29 : 69

هَلَكَ عَنِّي سُلۡطَٰنِيَهۡ

Madaraka yangu yamenipotea. [29] info

[29] Uzima wangu umenipotea, na nguvu zangu zimenitoka.

التفاسير:

external-link copy
30 : 69

خُذُوهُ فَغُلُّوهُ

(Pasemwe): Mshikeni! Mtieni pingu! [30] info

[30] Wataambiwa walinzi wa Jahannamu: Mshikeni, na mfungeni mikono yake kwenye shingo yake.

التفاسير:

external-link copy
31 : 69

ثُمَّ ٱلۡجَحِيمَ صَلُّوهُ

Kisha mtupeni Motoni! [31] info

[31] Kisha msimtie popote ila ndani ya Moto wa Jahannamu,

التفاسير:

external-link copy
32 : 69

ثُمَّ فِي سِلۡسِلَةٖ ذَرۡعُهَا سَبۡعُونَ ذِرَاعٗا فَٱسۡلُكُوهُ

Tena mtatizeni katika mnyororo wenye urefu wa dhiraa sabiini! [32] info

[32] Kisha mfungeni kwenye mnyororo mrefu kabisa.

التفاسير:

external-link copy
33 : 69

إِنَّهُۥ كَانَ لَا يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ ٱلۡعَظِيمِ

Kwani huyo hakika alikuwa hamuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu, [33] info

[33] Hakika huyo alikuwa hamsadiki Mwenyezi Mungu Mtukufu,

التفاسير:

external-link copy
34 : 69

وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلۡمِسۡكِينِ

Wala hahimizi kulisha masikini. [34] info

[34] Wala hamhimizi yoyote kuwalisha masikini.

التفاسير:

external-link copy
35 : 69

فَلَيۡسَ لَهُ ٱلۡيَوۡمَ هَٰهُنَا حَمِيمٞ

Basi leo hapa hana jamaa wa kumwonea uchungu, [35] info

[35] Basi hii leo huyu kafiri hana jamaa wa kumtetea,

التفاسير: