Prijevod značenja časnog Kur'ana - Prijevod na svahili jezik - Abdullah Muhammed i Nasir Hamis

Broj stranice:close

external-link copy
11 : 24

إِنَّ ٱلَّذِينَ جَآءُو بِٱلۡإِفۡكِ عُصۡبَةٞ مِّنكُمۡۚ لَا تَحۡسَبُوهُ شَرّٗا لَّكُمۖ بَلۡ هُوَ خَيۡرٞ لَّكُمۡۚ لِكُلِّ ٱمۡرِيٕٖ مِّنۡهُم مَّا ٱكۡتَسَبَ مِنَ ٱلۡإِثۡمِۚ وَٱلَّذِي تَوَلَّىٰ كِبۡرَهُۥ مِنۡهُمۡ لَهُۥ عَذَابٌ عَظِيمٞ

Kwa hakika, wale waliokuja na urongo mbaya kabisa, nao ni kumsingizia Mama wa Waumini 'Aishah, radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie, kuwa amefanya kitendo kichafu, ni kikundi cha watu wanaohusiana na nyinyi, enyi kongamano la Waislamu. Msidhanie maneno yao ni shari kwenu, ilivyo ni kuwa maneno yao ni kheri kwenu, kwa kuwa yalitokamana na maneno hayo kutakaswa Mama wa Waumini na uchafu, kusafika kwake na kuukuza utajo wake, kuzipandisha daraja, kuyafuta maovu na kuwasafisha Waumini. Kila mmoja aliyouzungumza urongo huo atapata malipo ya kitendo chake cha dhambi. Na yule aliyebeba jukumu kubwa zaidi katika uzushi huo, naye ni 'Abdullāh bin Ubayy bin Salūl, kiongozi wa wanafiki, Mwenyezi Mungu Amlaani, atakuwa na adhabu kubwa huko Akhera, nayo ni kukaa milele wakati waliposikia uzushi huo, nayo nikumuepushia kile ambacho hao (wazushi) walimsngizia nacho na kusema, «Huu ni urongo waziwazi juu ya 'Aishah, radhi za Mwenyezi Mungu zimshukuie. info
التفاسير:

external-link copy
12 : 24

لَّوۡلَآ إِذۡ سَمِعۡتُمُوهُ ظَنَّ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتُ بِأَنفُسِهِمۡ خَيۡرٗا وَقَالُواْ هَٰذَآ إِفۡكٞ مُّبِينٞ

Si ingalikuwa bora kwa Waumini wanaume na wanawake wadhaniane kheri wao kwa wao pindi walikposikia uzushi huo, kuwa yale waliyosingiziwa hawanayo, na waseme, «Huu ni urongo ulio wazi» juu ya ‘Aishah, radhi za Mwenyezi Mungu zimfikie. info
التفاسير:

external-link copy
13 : 24

لَّوۡلَا جَآءُو عَلَيۡهِ بِأَرۡبَعَةِ شُهَدَآءَۚ فَإِذۡ لَمۡ يَأۡتُواْ بِٱلشُّهَدَآءِ فَأُوْلَٰٓئِكَ عِندَ ٱللَّهِ هُمُ ٱلۡكَٰذِبُونَ

Si ingalikuwa walete mashahidi waadilifu wanne kuthibitisha maneno yao waliyoyasema. Na kwa kuwa hawakulifanya hilo, basi wao ni warongo mbele ya Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
14 : 24

وَلَوۡلَا فَضۡلُ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ وَرَحۡمَتُهُۥ فِي ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِ لَمَسَّكُمۡ فِي مَآ أَفَضۡتُمۡ فِيهِ عَذَابٌ عَظِيمٌ

Na lau kama si wema wa Mwenyezi Mungu kwenu na rehema Zake, kwa kuwa wema Wake umewakusanya nyinyi katika Dini yenu na Akhera yenu, Asifanye haraka kuwaadhibu na aikubali toba ya mwenye kutubia miongoni mwenu, basi inagaliwapata adhabu kali kwa sababu ya maneno ya uvumi mliyojihusisha nayo. info
التفاسير:

external-link copy
15 : 24

إِذۡ تَلَقَّوۡنَهُۥ بِأَلۡسِنَتِكُمۡ وَتَقُولُونَ بِأَفۡوَاهِكُم مَّا لَيۡسَ لَكُم بِهِۦ عِلۡمٞ وَتَحۡسَبُونَهُۥ هَيِّنٗا وَهُوَ عِندَ ٱللَّهِ عَظِيمٞ

Kipindi mlichokuwa mnaupokea uzushi na mnaueneza kwa midomo yenu, nao ni yale maneno ya urongo na ambayo hamuna ujuzi nao. Na mambo mawili haya yameharamishwa: kusema maneno ya urongo na kusema bila ya ujuzi. Na mnadhani kuwa hilo ni jambo dogo, nalo ni kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu. Katika haya pana makemeo bayana juu ya kupuuza makatazo ya uenezaji ubatilifu. info
التفاسير:

external-link copy
16 : 24

وَلَوۡلَآ إِذۡ سَمِعۡتُمُوهُ قُلۡتُم مَّا يَكُونُ لَنَآ أَن نَّتَكَلَّمَ بِهَٰذَا سُبۡحَٰنَكَ هَٰذَا بُهۡتَٰنٌ عَظِيمٞ

Mbona hamukusema mlipousikia uzushi huo, «Haifai kwetu kuusema urongo huu. Kutakasika ni kwako, ewe Mola, kuyasema hayo juu ya mke wa Mtume wako Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. Huu ni urongo uliobeba mzigo mkubwa wa madhambi.» info
التفاسير:

external-link copy
17 : 24

يَعِظُكُمُ ٱللَّهُ أَن تَعُودُواْ لِمِثۡلِهِۦٓ أَبَدًا إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ

Mwenyezi Mungu Anawakumbusha na Anawakataza msirudie kitendo hiki cha kusingizia urongo, iwapo nyinyi ni wenye kumuamini Yeye. info
التفاسير:

external-link copy
18 : 24

وَيُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمُ ٱلۡأٓيَٰتِۚ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ

Na Anawafafanulia nyinyi aya zinazokusanya hukumu za kisheria na mawaidha. Na Mwenyezi Mungu Anayajua sana matendo yenu, ni Mwenye hekima katika sheria Zake na uendeshaji Wake. info
التفاسير:

external-link copy
19 : 24

إِنَّ ٱلَّذِينَ يُحِبُّونَ أَن تَشِيعَ ٱلۡفَٰحِشَةُ فِي ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ فِي ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِۚ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ وَأَنتُمۡ لَا تَعۡلَمُونَ

Kwa hakika,wale wanaopenda kuenea machafu kwa Waislamu, ya tuhuma za uzinifu au jambo lolote baya, watapata adhabu kali ulimwenguni, kwa kupigwa mboko, na mengineyo miongoni mwa mitihani ya kilimwengu, na watapata adhabu ya Motoni huko Akhera wakiwa hawakutubia. Na Mwenyezi Mungu, peke Yake, Ndiye Anayejua urongo wao na Ndiye Anayeyajua maslahi ya waja wake na mwisho wa mambo , na nyinyi hamyajui hayo. info
التفاسير:

external-link copy
20 : 24

وَلَوۡلَا فَضۡلُ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ وَرَحۡمَتُهُۥ وَأَنَّ ٱللَّهَ رَءُوفٞ رَّحِيمٞ

Na lau kama si wema wa Mwenyezi Mungu juu ya wale waliohusika kwenye tukio la uzushi na rehema zake kwao na kwamba Mwenyezi Mungu Anawahurumia waja Wake Waumini huruma kunjufu katika yale wanaokuwa na pupu nayo (ya ulimwengu) na yale wanayoyasubiri (ya Akhera), hangalizifunua wazi hukumu hizi na mawaidha na Angalifanya haraka kumuadhibu yule aendaye kinyume na amri Yake. info
التفاسير: