Prijevod značenja časnog Kur'ana - Prijevod na svahili jezik - Abdullah Muhammed i Nasir Hamis

An-Nur

external-link copy
1 : 24

سُورَةٌ أَنزَلۡنَٰهَا وَفَرَضۡنَٰهَا وَأَنزَلۡنَا فِيهَآ ءَايَٰتِۭ بَيِّنَٰتٖ لَّعَلَّكُمۡ تَذَكَّرُونَ

Hii ni sura kubwa miongoni mwa sura za Qur’ani, tumeiteremsha na tumelazimisha kuzifanyia kazi hukumu zake, na tumeteremsha ndani yake hoja nyingi zilizo waziwazi ili mupate kujikumbusha, enyi Waumini, kwa aya hizi zilizo waziwazi na muzitumie. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 24

ٱلزَّانِيَةُ وَٱلزَّانِي فَٱجۡلِدُواْ كُلَّ وَٰحِدٖ مِّنۡهُمَا مِاْئَةَ جَلۡدَةٖۖ وَلَا تَأۡخُذۡكُم بِهِمَا رَأۡفَةٞ فِي دِينِ ٱللَّهِ إِن كُنتُمۡ تُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِۖ وَلۡيَشۡهَدۡ عَذَابَهُمَا طَآئِفَةٞ مِّنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Mzinifu mwanamume na mzinifu mwanamke ambao hawajawahi kuoa au kuolewa, adabu ya kila mmoja kati yao ni kupigwa mboko mia moja. Na imethibiti katika Sunnah (mapokezi kutoka kwa Mtume) kwamba pamoja na mboko hizi, ahamishwe kwa kipindi cha mwaka mmoja. Wala kusiwafanye nyinyi kule kuwahurumia kuacha kuwatia adabu hiyo au kuipunguza, iwapo munamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na munazifuata kivitendo hukumu za Kiislamu. Na waihudhurie adabu hiyo kikundi cha Waumini kwa kuwaumbua na iwe ni kitisho, mawaidha na mazingatio. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 24

ٱلزَّانِي لَا يَنكِحُ إِلَّا زَانِيَةً أَوۡ مُشۡرِكَةٗ وَٱلزَّانِيَةُ لَا يَنكِحُهَآ إِلَّا زَانٍ أَوۡ مُشۡرِكٞۚ وَحُرِّمَ ذَٰلِكَ عَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Mwanamume mzinifu haridhiki isipokuwa kumuoa mwanamke mzinifu au mwanamke mshirikina asiyekubali uharamu wa uhalifu wa uzinifu, na mwanamke mzinifu haridhiki isipokuwa kuolewa na mwanamume mzinifu mwanamume mshirikina asiyekubali uharamu wa uzinifu. Ama wanaume na wanawake wanaojizuia na uzinifu, wao hawaridhiki na hilo, na ndoa hiyo imeharamishwa kwa Waumini. Na huu ni ushahidi wazi wa uharamu wa kumuoa mwanamke mzinifu mpaka atubie, vilevile uharamu wa kumuoza mwanamume mzinifu mpaka atubie. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 24

وَٱلَّذِينَ يَرۡمُونَ ٱلۡمُحۡصَنَٰتِ ثُمَّ لَمۡ يَأۡتُواْ بِأَرۡبَعَةِ شُهَدَآءَ فَٱجۡلِدُوهُمۡ ثَمَٰنِينَ جَلۡدَةٗ وَلَا تَقۡبَلُواْ لَهُمۡ شَهَٰدَةً أَبَدٗاۚ وَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡفَٰسِقُونَ

Na wale wanaowatuhumu watu waliojihifidhi, miongoni mwa wanaume na wanawake, kwa uchafu wa uzinifu pasi na kushuhudia pamoja na wao mashahidi wanne waadilifu, basi wapigeni mboko themanini na msiwakubalie ushahidi mwingine wowote kabisa, na hao ndio waliotoka nje ya utiifu wa Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 24

إِلَّا ٱلَّذِينَ تَابُواْ مِنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَ وَأَصۡلَحُواْ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Lakini mwenye kutubia, akajuta, akarudi nyuma katika tuhuma yake na akatengeneza matendo yake, kwa kweli Mwenyezi Mungu Atamsamehe dhambi zake, Atamuonea huruma na Ataikubali toba yake. info
التفاسير:

external-link copy
6 : 24

وَٱلَّذِينَ يَرۡمُونَ أَزۡوَٰجَهُمۡ وَلَمۡ يَكُن لَّهُمۡ شُهَدَآءُ إِلَّآ أَنفُسُهُمۡ فَشَهَٰدَةُ أَحَدِهِمۡ أَرۡبَعُ شَهَٰدَٰتِۭ بِٱللَّهِ إِنَّهُۥ لَمِنَ ٱلصَّٰدِقِينَ

Na wale wanaowatuhumu wake zao kwa uzinifu, na wakawa hawana mashahidi wa kutilia nguvu tuhuma yao isipokuwa wao wenyewe, basi ni juu ya mmoja wao hao wenye kutuhumu, atoe ushahidi mbele ya kadhi mara nne kwa kusema, «Ninashuhudia kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba mimi ni mkweli katika lile la uzinifu ambalo nimemtuhumu mke wangu kwalo.» info
التفاسير:

external-link copy
7 : 24

وَٱلۡخَٰمِسَةُ أَنَّ لَعۡنَتَ ٱللَّهِ عَلَيۡهِ إِن كَانَ مِنَ ٱلۡكَٰذِبِينَ

Na aongeze kwenye ushahidi wa tano kujiapiza nafsi yake kuwa inastahili kupata laana ya Mwenyezi Mungu iwapo yeye ni mrongo katika maneno yake hayo. info
التفاسير:

external-link copy
8 : 24

وَيَدۡرَؤُاْ عَنۡهَا ٱلۡعَذَابَ أَن تَشۡهَدَ أَرۡبَعَ شَهَٰدَٰتِۭ بِٱللَّهِ إِنَّهُۥ لَمِنَ ٱلۡكَٰذِبِينَ

Na kwa ushahidi wake huu, itapasa kwa yule mke aliyetuhumiwa kutiwa adabu ya uzinifu, nayo ni kupigwa mawe mpaka kufa. Na haitamuepukia adabu hii mpaka atoe ushahidi wa kupinga ule ushahidi wa mumewe, mara nne kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba mumewe ni mrongo katika madai yake kuwa yeye amezini. info
التفاسير:

external-link copy
9 : 24

وَٱلۡخَٰمِسَةَ أَنَّ غَضَبَ ٱللَّهِ عَلَيۡهَآ إِن كَانَ مِنَ ٱلصَّٰدِقِينَ

Na aongeze katika ushahidi wake wa mara ya tano kwa kujiapiza kuwa anapaswa kushukiwa na hasira za Mwenyezimngu iwapo mumewe ni mkweli katika madai yake kuwa yeye amezini. Na katika hali hii watatenganishwa baina ya wao wawili. info
التفاسير:

external-link copy
10 : 24

وَلَوۡلَا فَضۡلُ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ وَرَحۡمَتُهُۥ وَأَنَّ ٱللَّهَ تَوَّابٌ حَكِيمٌ

Na lau kama si wema wa Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema Zake kwenu, enyi Waumini, kwa mapitisho haya ya kisheria kwa waume na wake, na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuitikia toba kwa aliyetubia miongoni mwa waja wake ni Mwingi wa hekima katika sheria Zake na maongozi Yake, basi yangalimpata mmoja wa wale wawili wanaolaaniana yale aliyojiapiza. info
التفاسير: