Qurani Kərimin mənaca tərcüməsi - Səvahili dilinə tərcümə - Əli Muhsin əl-Bərvani.

Abasa

external-link copy
1 : 80

عَبَسَ وَتَوَلَّىٰٓ

Alikunja kipaji na akageuka! info

Uso wake ulitaghayari kwa kuchukia na akageuka,

التفاسير:

external-link copy
2 : 80

أَن جَآءَهُ ٱلۡأَعۡمَىٰ

Kwa sababu alimjia kipofu! info

Kwa sababu kamjia kipofu anamuuliza khabari ya Dini yake.

التفاسير:

external-link copy
3 : 80

وَمَا يُدۡرِيكَ لَعَلَّهُۥ يَزَّكَّىٰٓ

Na nini kitakujuulisha pengine yeye atatakasika? info

Na wewe unajuaje, pengine huyo kipofu atatakasika kwa atayo yapata kwako,

التفاسير:

external-link copy
4 : 80

أَوۡ يَذَّكَّرُ فَتَنفَعَهُ ٱلذِّكۡرَىٰٓ

Au atawaidhika, na mawaidha yamfae? info

Au atawaidhika na mawaidha yamfae.

التفاسير:

external-link copy
5 : 80

أَمَّا مَنِ ٱسۡتَغۡنَىٰ

Ama ajionaye hana haja! info

Ama yule anaye jiona ametosheka kwa mali yake na nguvu zake,

التفاسير:

external-link copy
6 : 80

فَأَنتَ لَهُۥ تَصَدَّىٰ

Wewe ndio unamshughulikia? info

Wewe ndio unamkabili na unamshughulikia kumfikishia wito wako.

التفاسير:

external-link copy
7 : 80

وَمَا عَلَيۡكَ أَلَّا يَزَّكَّىٰ

Na si juu yako kama hakutakasika. info

Na wewe una lawama gani ikiwa yeye hakutakasika kwa Imani?

التفاسير:

external-link copy
8 : 80

وَأَمَّا مَن جَآءَكَ يَسۡعَىٰ

Ama anaye kujia kwa juhudi . info

Ama anaye kukimbilia kutafuta ilimu na uwongofu,

التفاسير:

external-link copy
9 : 80

وَهُوَ يَخۡشَىٰ

Naye anaogopa! info

Naye anamkhofu Mwenyezi Mungu .

التفاسير:

external-link copy
10 : 80

فَأَنتَ عَنۡهُ تَلَهَّىٰ

Ndio wewe unampuuza? info

Wewe unampuuza.

التفاسير:

external-link copy
11 : 80

كَلَّآ إِنَّهَا تَذۡكِرَةٞ

Sivyo hivyo! Huku ni kukumbushana. info

Hakika Aya hizi ni mawaidha.

التفاسير:

external-link copy
12 : 80

فَمَن شَآءَ ذَكَرَهُۥ

Basi anaye penda akumbuke. info

Mwenye kutaka atawaidhika kwa Qur'ani.

التفاسير:

external-link copy
13 : 80

فِي صُحُفٖ مُّكَرَّمَةٖ

Yamo katika kurasa zilizo hishimiwa, info

Nayo Qur'ani imo katika kurasa zilizo tukuzwa kwa Mwenyezi Mungu,

التفاسير:

external-link copy
14 : 80

مَّرۡفُوعَةٖ مُّطَهَّرَةِۭ

Zilizo inuliwa, zilizo takaswa. info

Zina cheo cha juu, na pahala palipo tukuka, zimetakasika na kila upungufu.

التفاسير:

external-link copy
15 : 80

بِأَيۡدِي سَفَرَةٖ

Zimo mikononi mwa Malaika waandishi, info

Katika mikono ya Malaika ambao Mwenyezi Mungu amewafanya ndio mabalozi baina yake na Mitume wake;

التفاسير:

external-link copy
16 : 80

كِرَامِۭ بَرَرَةٖ

Watukufu, wema. info

Walio bora, wema.

التفاسير:

external-link copy
17 : 80

قُتِلَ ٱلۡإِنسَٰنُ مَآ أَكۡفَرَهُۥ

Ameangamia mwanaadamu! Nini kinacho mkufurisha? info

Ameangamia mwanaadamu! Nini kilicho mfanya akufuru na hali Mwenyezi Mungu amemfanyia hisani zote hizi?

التفاسير:

external-link copy
18 : 80

مِنۡ أَيِّ شَيۡءٍ خَلَقَهُۥ

Kwa kitu gani amemuumba? info

Hakumbuki yeye kaumbwa kutokana na nini?

التفاسير:

external-link copy
19 : 80

مِن نُّطۡفَةٍ خَلَقَهُۥ فَقَدَّرَهُۥ

Kwa tone la manii, akamuumba na akamkadiria. info

Kutokana na maji ya kudharauliwa Yeye Mwenyezi Mungu alimwanzisha kumuumba akamjaalia apitie daraja mbali mbali za kukua.

التفاسير:

external-link copy
20 : 80

ثُمَّ ٱلسَّبِيلَ يَسَّرَهُۥ

Kisha akamsahilishia njia. info

Kisha akamfanyia nyepesi njia ya kufikia Imani, na akamfunza njia hiyo.

التفاسير:

external-link copy
21 : 80

ثُمَّ أَمَاتَهُۥ فَأَقۡبَرَهُۥ

Kisha akamfisha, akamtia kaburini. info

Kisha akamfisha na akamtukuza kwa kumtia kaburini.

التفاسير:

external-link copy
22 : 80

ثُمَّ إِذَا شَآءَ أَنشَرَهُۥ

Kisha apendapo atamfufua. info

Na tena akipenda atamhuisha baada ya kufa kwake.

التفاسير:

external-link copy
23 : 80

كَلَّا لَمَّا يَقۡضِ مَآ أَمَرَهُۥ

La! Hajamaliza aliyo muamuru. info

Ni kweli mwanaadamu, juu ya kuwa umri wake mrefu duniani, hakutimiza aliyo amrishwa na Mwenyezi Mungu katika mambo ya Imani na ut'iifu.

التفاسير:

external-link copy
24 : 80

فَلۡيَنظُرِ ٱلۡإِنسَٰنُ إِلَىٰ طَعَامِهِۦٓ

Hebu mtu na atazame chakula chake. info

Hebu mtu na aangalie shani ya chakula chake - vipi tulivyo kipanga na kumsahilishia!

التفاسير:

external-link copy
25 : 80

أَنَّا صَبَبۡنَا ٱلۡمَآءَ صَبّٗا

Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu, info

Ni Sisi tumeiteremsha mvua kutoka mbinguni, ikateremka.

التفاسير:

external-link copy
26 : 80

ثُمَّ شَقَقۡنَا ٱلۡأَرۡضَ شَقّٗا

Tena tukaipasua pasua ardhi kwa nguvu, info

Tena tukaipasua pasua ardhi kwa ajili ya mimea.

التفاسير:

external-link copy
27 : 80

فَأَنۢبَتۡنَا فِيهَا حَبّٗا

Kisha tukaotesha humo nafaka, info

Tukaotesha humo nafaka ambazo watu huzila na huweka akiba.

التفاسير:

external-link copy
28 : 80

وَعِنَبٗا وَقَضۡبٗا

Na zabibu, na mimea ya majani, info

Na mizabibu na mimea ya majani inayo liwa mibichi.

التفاسير:

external-link copy
29 : 80

وَزَيۡتُونٗا وَنَخۡلٗا

Na mizaituni, na mitende, info

Na mizaituni mizuri, na mitende yenye kuzaa,

التفاسير:

external-link copy
30 : 80

وَحَدَآئِقَ غُلۡبٗا

Na bustani zenye miti iliyo songana baraabara, info

Na mabustani yaliyo songamana matawi ya miti yake,

التفاسير:

external-link copy
31 : 80

وَفَٰكِهَةٗ وَأَبّٗا

Na matunda, na malisho ya wanyama; info

Na matunda ya kustaladhi nayo, na malisha ya kula nyama hoa (mifugo).

التفاسير:

external-link copy
32 : 80

مَّتَٰعٗا لَّكُمۡ وَلِأَنۡعَٰمِكُمۡ

Kwa manufaa yenu na mifugo yenu. info

Tumeotesha yote hayo kwa ajili ya faida yenu na wanyama wenu wa kufuga.

التفاسير:

external-link copy
33 : 80

فَإِذَا جَآءَتِ ٱلصَّآخَّةُ

Basi utakapo kuja ukelele, info

Basi utakapo kuja ukelele wa Kiyama utakao tia uziwi masikio,

التفاسير:

external-link copy
34 : 80

يَوۡمَ يَفِرُّ ٱلۡمَرۡءُ مِنۡ أَخِيهِ

Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye, info

Siku mtu atakapo mkimbia ndugu yake,

التفاسير:

external-link copy
35 : 80

وَأُمِّهِۦ وَأَبِيهِ

Na mamaye na babaye, info

Na mama yake, na baba yake,

التفاسير:

external-link copy
36 : 80

وَصَٰحِبَتِهِۦ وَبَنِيهِ

Na mkewe na wanawe. info

Na mkewe, na wanawe!

التفاسير:

external-link copy
37 : 80

لِكُلِّ ٱمۡرِيٕٖ مِّنۡهُمۡ يَوۡمَئِذٖ شَأۡنٞ يُغۡنِيهِ

Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha info

Kila mmojapo katika hawa atakuwa na jambo lake la kumshughulisha!

التفاسير:

external-link copy
38 : 80

وُجُوهٞ يَوۡمَئِذٖ مُّسۡفِرَةٞ

Siku hiyo ziko nyuso zitazo nawiri, info

Zipo nyuso siku hii zenye mwangaza,

التفاسير:

external-link copy
39 : 80

ضَاحِكَةٞ مُّسۡتَبۡشِرَةٞ

Zitacheka, zitachangamka; info

Zenye kung'ara na kufurahi kwa neema za Mwenyezi Mungu.

التفاسير:

external-link copy
40 : 80

وَوُجُوهٞ يَوۡمَئِذٍ عَلَيۡهَا غَبَرَةٞ

Na nyuso siku hiyo zitakuwa na mavumbi, info

Na nyuso nyengine siku hii zina vumbi zimesawijika.

التفاسير:

external-link copy
41 : 80

تَرۡهَقُهَا قَتَرَةٌ

Giza totoro litazifunika, info

Zimegubikwa na kiza na weusi.

التفاسير:

external-link copy
42 : 80

أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡكَفَرَةُ ٱلۡفَجَرَةُ

Hao ndio makafiri watenda maovu info

Wenye nyuso hizi ni makafiri wapotovu, ambao walio kuwa hawabali maasi waliyo kuwa wakiyatenda.

التفاسير: