Qurani Kərimin mənaca tərcüməsi - Səvahili dilinə tərcümə - Əli Muhsin əl-Bərvani.

external-link copy
27 : 8

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَخُونُواْ ٱللَّهَ وَٱلرَّسُولَ وَتَخُونُوٓاْ أَمَٰنَٰتِكُمۡ وَأَنتُمۡ تَعۡلَمُونَ

Enyi mlio amini! Msimfanyie khiana Mwenyezi Mungu na Mtume, wala msikhini amana zenu, nanyi mnajua. info

Enyi mlio isadiki Haki mkaifuata! Haikufaliini kumkhini Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa kufanya urafiki na maadui wa Haki, na kukhuni katika ngawira, au kwa kuacha kwenda kwenye Jihadi. Wala msikhuni amana mnazo pewa nanyi mnajua amri na makatazo yake.

التفاسير: