[40] Mwenyezi Mungu Subhaanu Alietakasaika, ndie aliekuumbeni, kisha kakupeni cha kukupeeni maisha, kisha ndie anaekufesheni, na kisha atakufufueni kutoka makaburini mwenu. Je? Yupo yoyote katika hao miungu ya kishirikina mnao dai na mukaawabudu badala ya Mwenyezi Mungu mwenye kutenda hayo ya kuumba na kukuruzuku, na kufisha na kukufua, au kitendo chochote, Mwenyezi Mungu ametakasika na hayo wanao mshirikisha naye.