Qurani Kərimin mənaca tərcüməsi - Səvahili dilinə tərcümə - Abdullah Məhəmməd və Nasir Xamis.

Səhifənin rəqəmi:close

external-link copy
7 : 51

وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلۡحُبُكِ

Na Anaapa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kwa mbingu zenye umbo zuri, kwamba nyinyi, enyi wakanushaji, info
التفاسير:

external-link copy
8 : 51

إِنَّكُمۡ لَفِي قَوۡلٖ مُّخۡتَلِفٖ

mko kwenye neno linalogongana kuhusu Qur’ani na kuhusu Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. info
التفاسير:

external-link copy
9 : 51

يُؤۡفَكُ عَنۡهُ مَنۡ أُفِكَ

Anaepushwa na Qur’ani na Mtume yule aliyeepushwa na lile la kuviamini hivyo viwili kwa kuzipa mgongo dalili za Mwenyezi Mungu na hoja Zake za yakini, na kwa hivyo haafikiwi kwenye kheri. info
التفاسير:

external-link copy
10 : 51

قُتِلَ ٱلۡخَرَّٰصُونَ

Wamelaaniwa warongo wenye dhana zisizo za kweli, info
التفاسير:

external-link copy
11 : 51

ٱلَّذِينَ هُمۡ فِي غَمۡرَةٖ سَاهُونَ

waliomo ndani ya dimbwi la ukafiri na upotevu hali ya kuwa wameghafilika na kujikita kwenye ubatilifu wao. info
التفاسير:

external-link copy
12 : 51

يَسۡـَٔلُونَ أَيَّانَ يَوۡمُ ٱلدِّينِ

Wanauliza hawa wenye kukanusha suali la kuonyesha kuwa ni jambo lisilowezekana na la kuonyesha ukanushaji, «Ni lini Siku ya kuhesabiwa na kulipwa?» info
التفاسير:

external-link copy
13 : 51

يَوۡمَ هُمۡ عَلَى ٱلنَّارِ يُفۡتَنُونَ

Siku ya Malipo ni Siku ya wao kuadhibiwa kwa kuchomwa kwa Moto na waambiwe, info
التفاسير:

external-link copy
14 : 51

ذُوقُواْ فِتۡنَتَكُمۡ هَٰذَا ٱلَّذِي كُنتُم بِهِۦ تَسۡتَعۡجِلُونَ

«Onjeni adhabu yenu ambayo mlikuwa mkiifanyia haraka duniani.» info
التفاسير:

external-link copy
15 : 51

إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي جَنَّٰتٖ وَعُيُونٍ

Hakika ya wale wanaomcha Mwenyezi Mungu watakuwa kwenye mabustani ya Pepo makubwa na chemchemi za maji yenye kutembea. Mwenyezi Mungu Atawapa yote wanayoyatamani ya aina mbalimbali za starehe. info
التفاسير:

external-link copy
16 : 51

ءَاخِذِينَ مَآ ءَاتَىٰهُمۡ رَبُّهُمۡۚ إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَبۡلَ ذَٰلِكَ مُحۡسِنِينَ

Watazipokea neema hizo wakiwa wameridhika nazo na nafsi zao zina furaha. Hakika wao, kabla ya kupata sterehe hizo, walikuwa wema duniani kwa matendo yao mema. info
التفاسير:

external-link copy
17 : 51

كَانُواْ قَلِيلٗا مِّنَ ٱلَّيۡلِ مَا يَهۡجَعُونَ

Wema hawa walikuwa wakilala kipindi kichache usiku, wakiswali kwa Mola wao wakimnyenyekea, info
التفاسير:

external-link copy
18 : 51

وَبِٱلۡأَسۡحَارِ هُمۡ يَسۡتَغۡفِرُونَ

na katika nyakati za mwisho wa usiku, kabla ya alfajiri kwa muda mchache, walikuwa wakimuomba Mwenyezi Mungu msamaha wa dhambi zao. info
التفاسير:

external-link copy
19 : 51

وَفِيٓ أَمۡوَٰلِهِمۡ حَقّٞ لِّلسَّآئِلِ وَٱلۡمَحۡرُومِ

Na katika mali yao kulikuwa na haki ya lazima na ya kupendekezwa kupewa wahitaji wanaowaomba watu na wasiowaomba kwa kuona haya. info
التفاسير:

external-link copy
20 : 51

وَفِي ٱلۡأَرۡضِ ءَايَٰتٞ لِّلۡمُوقِنِينَ

Na katika ardhi kuna mazingatio na dalili waziwazi za uweza wa Mwenyezi Mungu kwa watu wenye yakini kuwa Mwenyezi Mungu Ndiye Mola wa haki, Aliye Peke Yake na asiye na mshirika, na wenye kumuamini Mtume Wake. rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. info
التفاسير:

external-link copy
21 : 51

وَفِيٓ أَنفُسِكُمۡۚ أَفَلَا تُبۡصِرُونَ

Na katika kuwaumba nyinyi kuna dalili za uweza wa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na kuna mazingatio ya kuwaonyesha nyinyi upweke wa Muumba wenu na kwamba Yeye hakuna Mola Anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye. Je, mumeghafilika na hilo mkawa hamlioni mkazingatia kwalo? info
التفاسير:

external-link copy
22 : 51

وَفِي ٱلسَّمَآءِ رِزۡقُكُمۡ وَمَا تُوعَدُونَ

Na mbinguni kuna riziki yenu na yale mnayoahidiwa ya kheri na shari, na thawabu na mateso na yasiyokuwa hayo. Yote yameandikwa na kukadiriwa. info
التفاسير:

external-link copy
23 : 51

فَوَرَبِّ ٱلسَّمَآءِ وَٱلۡأَرۡضِ إِنَّهُۥ لَحَقّٞ مِّثۡلَ مَآ أَنَّكُمۡ تَنطِقُونَ

Anaapa Mwenyezi Mungu kwa dhati Yake tukufu kwamba kile Alichowaahidi ni kweli, msikifanyie shaka kama ambavyo hamshuku kuwa nyinyi mnasema. info
التفاسير:

external-link copy
24 : 51

هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ضَيۡفِ إِبۡرَٰهِيمَ ٱلۡمُكۡرَمِينَ

Je imekujia wewe, ewe Mtume, habari ya wageni wa Ibrāhīm aliyewakirimu info
التفاسير:

external-link copy
25 : 51

إِذۡ دَخَلُواْ عَلَيۡهِ فَقَالُواْ سَلَٰمٗاۖ قَالَ سَلَٰمٞ قَوۡمٞ مُّنكَرُونَ

na walikuwa ni miongoni mwa Malaika watukufu- wakati walipomjia nyumbani kwake, wakamwamkia kwa kumwambia, «Salama!»Akawarudishia maamkizi kwa kusema, «Salama ni kwenu! Nyinyi ni watu wageni hatuwajui.» info
التفاسير:

external-link copy
26 : 51

فَرَاغَ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِۦ فَجَآءَ بِعِجۡلٖ سَمِينٖ

Akaondoka kwa siri na akaelekea kwa watu wa nyumbani kwake akamlenga ndama mnono akamchinja, akamchoma info
التفاسير:

external-link copy
27 : 51

فَقَرَّبَهُۥٓ إِلَيۡهِمۡ قَالَ أَلَا تَأۡكُلُونَ

kisha akamuweka mbele yao na akawakaribisha kwa upole kwa kusema, «Si mle». info
التفاسير:

external-link copy
28 : 51

فَأَوۡجَسَ مِنۡهُمۡ خِيفَةٗۖ قَالُواْ لَا تَخَفۡۖ وَبَشَّرُوهُ بِغُلَٰمٍ عَلِيمٖ

Alipowaona hawali aliingiwa na kicho cha kuwaogopa, na hapo wakamwambia, «Usiogope! Sisi ni wajumbe wa Mwenyezi Mungu. Na wakampa bishara kwamba mkewe Sarah atamzalia mtoto atakayekuwa ni miongoni mwa watu wanaomjua Mwenyezi Mungu na kuijua Dini Yake, naye ni Isḥāq, amani imshukie. info
التفاسير:

external-link copy
29 : 51

فَأَقۡبَلَتِ ٱمۡرَأَتُهُۥ فِي صَرَّةٖ فَصَكَّتۡ وَجۡهَهَا وَقَالَتۡ عَجُوزٌ عَقِيمٞ

Aliposikia mke wa Ibrāhīm maneno ya bishara ya hao Malaika, alielekea upande wao na ukelele, akajipiga uso wake kwa kulionea ajabu jambo hili na akasema, «Vipi nitazaa na mimi ni tasa sizai?» info
التفاسير:

external-link copy
30 : 51

قَالُواْ كَذَٰلِكِ قَالَ رَبُّكِۖ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلۡحَكِيمُ ٱلۡعَلِيمُ

Malaika wa Mwenyezi Mungu wakamwambia, «Hivyo ndivyo Alivyosema Mola wako kama tulivyokwambia. Na Yeye Muweza wa hilo, hapana la ajabu kutokana na uweza Wake. Hakika Yeye, Aliyetakasika na kutukuka, Ndiye Mwenyew hekima Anayeviweka vitu mahali pake, Ndiye Mwenye kuyajua maslahi ya waja Wake. info
التفاسير: