Qurani Kərimin mənaca tərcüməsi - Səvahili dilinə tərcümə - Abdullah Məhəmməd və Nasir Xamis.

Səhifənin rəqəmi:close

external-link copy
51 : 28

۞ وَلَقَدۡ وَصَّلۡنَا لَهُمُ ٱلۡقَوۡلَ لَعَلَّهُمۡ يَتَذَكَّرُونَ

Na kwa hakika, tuliifafanua na kuieleza Qur’ani kwa kuwaonea huruma watu wako, ewe Mtume, huenda wao wakakumbuka na wakawaidhika nayo. info
التفاسير:

external-link copy
52 : 28

ٱلَّذِينَ ءَاتَيۡنَٰهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ مِن قَبۡلِهِۦ هُم بِهِۦ يُؤۡمِنُونَ

Wale ambao tuliwapa Kitabu kabla ya Qur’ani, nao ni Mayahudi na Wanaswara ambao hawakugeuza, wanaiamini Qur’ani na wanamuamini Muhammad, rehema na amani zimshukiye. info
التفاسير:

external-link copy
53 : 28

وَإِذَا يُتۡلَىٰ عَلَيۡهِمۡ قَالُوٓاْ ءَامَنَّا بِهِۦٓ إِنَّهُ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّنَآ إِنَّا كُنَّا مِن قَبۡلِهِۦ مُسۡلِمِينَ

Na pindi isomwapo hii Qur’ani kwa wale tuliowapa Kitabu wanasema, «Tumeiamini na tumeifuata kivitendo, hiyo ni haki itokayo kwa Mola wetu, hakika sisi tulikuwa, kabla haijateremka, ni Waislamu wenye kumpwekesha, kwani Dini ya Mwenyezi Mungu ni moja, nayo ni Uislamu.» info
التفاسير:

external-link copy
54 : 28

أُوْلَٰٓئِكَ يُؤۡتَوۡنَ أَجۡرَهُم مَّرَّتَيۡنِ بِمَا صَبَرُواْ وَيَدۡرَءُونَ بِٱلۡحَسَنَةِ ٱلسَّيِّئَةَ وَمِمَّا رَزَقۡنَٰهُمۡ يُنفِقُونَ

Hawa ambao sifa zao zimetangulia, watapewa malipo ya matendo yao mema mara mbili: ya kukiamini Kitabu chao na kuiamini kwao Qur’ani kwa vile walivyosubiri. Na miongoni mwa sifa zao ni kwamba wao wanalikinga baya kwa zuri, na katika kile tunachowaruzuku wanatumia katika njia ya uzuri na wema. info
التفاسير:

external-link copy
55 : 28

وَإِذَا سَمِعُواْ ٱللَّغۡوَ أَعۡرَضُواْ عَنۡهُ وَقَالُواْ لَنَآ أَعۡمَٰلُنَا وَلَكُمۡ أَعۡمَٰلُكُمۡ سَلَٰمٌ عَلَيۡكُمۡ لَا نَبۡتَغِي ٱلۡجَٰهِلِينَ

Na wanaposikia, watu hawa, maneno ya ubatilifu, hawayapulikizi, na wanasema, «Sisi tuna matendo yetu tusiyoyaepuka, na nyinyi muna matendo yenu msiyoyaepuka. Sisi hatujishughulishi kuwarudi nyinyi, na hamtasikia kutoka kwetu isipokuwa mema, na hatutasema na nyinyi kulingana na ujinga wenu, kwa kuwa sisi hatutaki njia ya wajinga na hatuipendi.» Na haya ni miongoni mwa maneno mazuri zaidi ambayo walinganizi kwa Mwenyezi Mungu wanayasema. info
التفاسير:

external-link copy
56 : 28

إِنَّكَ لَا تَهۡدِي مَنۡ أَحۡبَبۡتَ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ يَهۡدِي مَن يَشَآءُۚ وَهُوَ أَعۡلَمُ بِٱلۡمُهۡتَدِينَ

Wewe, ewe Mtume, humuongoi, uongofu wa kumuafikia, unayependa aongoke. Lakini hilo liko kwenye mkono wa Mwenyezi Mungu, Anamuongoa Anayemtaka kumuongoa kwenye Imani na kumuafikia aifuate. Na Yeye Ndiye Anayemjua zaidi anayefaa kuongoka, hivyo basi Anamuongoa. info
التفاسير:

external-link copy
57 : 28

وَقَالُوٓاْ إِن نَّتَّبِعِ ٱلۡهُدَىٰ مَعَكَ نُتَخَطَّفۡ مِنۡ أَرۡضِنَآۚ أَوَلَمۡ نُمَكِّن لَّهُمۡ حَرَمًا ءَامِنٗا يُجۡبَىٰٓ إِلَيۡهِ ثَمَرَٰتُ كُلِّ شَيۡءٖ رِّزۡقٗا مِّن لَّدُنَّا وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ

Na makafiri wa Makkah wanasema, «Tukiifuata haki uliyotuletea na tukajiepusha na wategemewa na waungu, tutanyakuliwa kutoka kwenye ardhi yetu kwa kuuawa na kutekwa na kuporwa mali.» Kwani hatukuwafanya wao wamakinifu ndani ya mji wa amani, ambao ndani yake tumeharamisha umwagaji damu na ambao yanaletwa huko matunda ya kila aina yakiwa ni riziki kutoka kwetu? Lakini wengi wa hawa washirikina hawajui kadiri ya neema hizi kwao, wakapata kumshukuru Aliyewaneemesha wao kwazo na wakamtii. info
التفاسير:

external-link copy
58 : 28

وَكَمۡ أَهۡلَكۡنَا مِن قَرۡيَةِۭ بَطِرَتۡ مَعِيشَتَهَاۖ فَتِلۡكَ مَسَٰكِنُهُمۡ لَمۡ تُسۡكَن مِّنۢ بَعۡدِهِمۡ إِلَّا قَلِيلٗاۖ وَكُنَّا نَحۡنُ ٱلۡوَٰرِثِينَ

Na wengi miongoni mwa watu wa miji tuliwaangamiza yalipowapumbaza wao maisha yao yakawashughulisha wasiwaamini Mitume, kwa hivyo wakakufuru na wakapita kiasi. Basi hayo ndio majumba yao, hayakukaliwa baada yao isipokuwa machache katika hayo. Na sisi daima ndio wenye kuwarithi waja: tunawafisha, kisha wanarejea kwetu tukawalipa kwa matendo yao. info
التفاسير:

external-link copy
59 : 28

وَمَا كَانَ رَبُّكَ مُهۡلِكَ ٱلۡقُرَىٰ حَتَّىٰ يَبۡعَثَ فِيٓ أُمِّهَا رَسُولٗا يَتۡلُواْ عَلَيۡهِمۡ ءَايَٰتِنَاۚ وَمَا كُنَّا مُهۡلِكِي ٱلۡقُرَىٰٓ إِلَّا وَأَهۡلُهَا ظَٰلِمُونَ

Na hakuwa Mola wako, ewe Mtume, ni mwenye kuiangamiza miji iliyo pambizoni mwa Makkah katika zama zako mpaka Atumilize kwenye kilele cha miji hiyo, nacho ni Makkah, Mtume atakayewasomea wao aya zetu. Na hatukuwa ni wenye kuiangamiza miji isipokuwa na watu wake wanajidhulumu wenyewe kwa kumkanusha Mwenyezi Mungu na kumuasi, basi wao kwa hivyo wanastahili mateso na adhabu. info
التفاسير: