আল-কোৰআনুল কাৰীমৰ অৰ্থানুবাদ - শ্বাহিলি অনুবাদ- আলী মুহছিন আল-বাৰওৱানী

পৃষ্ঠা নং:close

external-link copy
46 : 11

قَالَ يَٰنُوحُ إِنَّهُۥ لَيۡسَ مِنۡ أَهۡلِكَۖ إِنَّهُۥ عَمَلٌ غَيۡرُ صَٰلِحٖۖ فَلَا تَسۡـَٔلۡنِ مَا لَيۡسَ لَكَ بِهِۦ عِلۡمٌۖ إِنِّيٓ أَعِظُكَ أَن تَكُونَ مِنَ ٱلۡجَٰهِلِينَ

Akasema: Ewe Nuhu! Huyu si katika ahali zako. Mwendo wake si mwema. Basi usiniombe jambo usio na ujuzi nalo. Mimi nakuwaidhi usije ukawa miongoni mwa wajinga. info

Allah Subhanahu akasema: Hakika huyo mwanao si katika ahali zako. Kwani yeye kwa ukafiri wake na mwendo wake pamoja na makafiri amekata makhusiano baina yako na yeye. Naye ametenda vitendo visio vyema. Kwa hivyo amekuwa si katika wewe. Nawe usitake jambo usilo lijua, kuwa ndilo au silo. Wala usende kufuata huruma zako. Na mimi nakuongoza njia ya Haki ili usiwe katika wajinga ukasahau kwa huruma zako Hakika iliyo thibiti!

التفاسير:

external-link copy
47 : 11

قَالَ رَبِّ إِنِّيٓ أَعُوذُ بِكَ أَنۡ أَسۡـَٔلَكَ مَا لَيۡسَ لِي بِهِۦ عِلۡمٞۖ وَإِلَّا تَغۡفِرۡ لِي وَتَرۡحَمۡنِيٓ أَكُن مِّنَ ٱلۡخَٰسِرِينَ

Nuhu akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Mimi najikinga kwako nisikuombe nisio na ujuzi nalo. Na kama hunisamehe na ukanirehemu, nitakuwa katika walio khasiri. info

Nuhu akasema: Ewe Muumba wangu, uliye tawala mambo yangu yote! Mimi nakuangukia Wewe. Sitakuomba nisicho kijua hakika yake. Nawe nisamehe kwa niliyo yasema kutokana na huruma zangu. Kama hukunipa fadhila ya msamaha wako, na ukanirehemu kwa rehema yako, nitakuwa katika makundi ya walio khasiri.

التفاسير:

external-link copy
48 : 11

قِيلَ يَٰنُوحُ ٱهۡبِطۡ بِسَلَٰمٖ مِّنَّا وَبَرَكَٰتٍ عَلَيۡكَ وَعَلَىٰٓ أُمَمٖ مِّمَّن مَّعَكَۚ وَأُمَمٞ سَنُمَتِّعُهُمۡ ثُمَّ يَمَسُّهُم مِّنَّا عَذَابٌ أَلِيمٞ

Ikasemwa: Ewe Nuhu! Shuka kwa salama itokayo kwetu, na baraka nyingi juu yako na juu ya watu walio pamoja nawe. Na zitakuwapo kaumu tutakazo zistarehesha, na kisha zitashikwa na adhabu chungu itokayo kwetu. info

Akaambiwa kwa wahyi: Ewe Nuhu! Teremka nchi kavu kutokana na hiyo Safina ya uwokovu, salama usalimina, kwa amani itokanayo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na baraka nyingi zitokazo kwa Mwenyezi Mungu juu yako na juu ya hao walio pamoja nawe, ambao watakuja kuwa mataifa mbali mbali baada yako. Na baadhi yao watapata baraka ya Imani na ut'iifu, na baadhi yao watakuwa watu wanao itaka starehe ya dunia, na watapata starehe yake bila ya kuit'ii Haki. Kisha Siku ya Kiyama itawapata adhabu chungu na kali.

التفاسير:

external-link copy
49 : 11

تِلۡكَ مِنۡ أَنۢبَآءِ ٱلۡغَيۡبِ نُوحِيهَآ إِلَيۡكَۖ مَا كُنتَ تَعۡلَمُهَآ أَنتَ وَلَا قَوۡمُكَ مِن قَبۡلِ هَٰذَاۖ فَٱصۡبِرۡۖ إِنَّ ٱلۡعَٰقِبَةَ لِلۡمُتَّقِينَ

 Hizi ni katika khabari za ghaibu tunazo kufunulia. Hukuwa ukizijua wewe, wala watu wako, kabla ya hii. Basi subiri! Hakika Mwisho ni wa wachamngu. info

Hizo ni simulizi tulizo kusimulia wewe, ewe Nabii, juu ya Nuhu na kaumu yake. Hizo ni khabari za ghaibu ambazo hazijui ila Mwenyezi Mungu. Wewe wala watu wako hamkuwa mkizijua kwa namna hii, na kwa tafsili hii, kabla ya wahyi huu. Basi wewe vumilia maudhi ya watu wako, kama walivyo subiri Manabii wa kabla yako. Kwani mwisho wako ni kufuzu kama ulivyo kuwa mwisho wao hao. Na Mwisho mwema daima ni wa wale wanao iogopa adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa kuamini na kutenda vitendo vyema.

التفاسير:

external-link copy
50 : 11

وَإِلَىٰ عَادٍ أَخَاهُمۡ هُودٗاۚ قَالَ يَٰقَوۡمِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنۡ إِلَٰهٍ غَيۡرُهُۥٓۖ إِنۡ أَنتُمۡ إِلَّا مُفۡتَرُونَ

Na kwa kina A'adi tulimtuma ndugu yao Hud. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu! Nyinyi hamna mungu isipo kuwa Yeye. Nyinyi si chochote ila ni wazushi tu. info

Na Sisi tuliwapelekea Kaumu ya A'adi wa mwanzo ndugu yao katika kabila yao, naye ni huyo Huud. Akawaambia: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu pekee. Kwani hamna anaye stahiki kuabudiwa isipo kuwa Yeye. Na nyinyi si cho chote ila mnazua uwongo tu kudai kuwa Mwenyezi Mungu ana washirika wanao stahiki nao kuabudiwa ili wawe waombezi wenu kwa Mwenyezi Mungu! Tazama maelezo ya ki-ilimu juu ya Aya 65 katika Sura Al-Aa'raaf. (7).

التفاسير:

external-link copy
51 : 11

يَٰقَوۡمِ لَآ أَسۡـَٔلُكُمۡ عَلَيۡهِ أَجۡرًاۖ إِنۡ أَجۡرِيَ إِلَّا عَلَى ٱلَّذِي فَطَرَنِيٓۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ

Enyi watu wangu! Sikuombeni ujira kwa ajili ya haya. Haukuwa ujira wangu ila kwa Yule aliye niumba. Basi hamtumii akili? info

Enyi watu! Kwa nasaha hii sitaki kwenu kulipwa kwa cheo, au utawala, au mali. Kwani ujira wangu uko kwa Mwenyezi Mungu aliye niumba. Wala haikufaliini nyinyi mkawa mmechotwa akili zenu kwa kughafilika msitambue linalo kufaeni na linalo kudhuruni!

التفاسير:

external-link copy
52 : 11

وَيَٰقَوۡمِ ٱسۡتَغۡفِرُواْ رَبَّكُمۡ ثُمَّ تُوبُوٓاْ إِلَيۡهِ يُرۡسِلِ ٱلسَّمَآءَ عَلَيۡكُم مِّدۡرَارٗا وَيَزِدۡكُمۡ قُوَّةً إِلَىٰ قُوَّتِكُمۡ وَلَا تَتَوَلَّوۡاْ مُجۡرِمِينَ

Na enyi watu wangu! Muombeni msamaha Mola wenu Mlezi, kisha mtubie kwake. Atakuleteeni mbingu zenye kunyesha mvua ya kumiminika, na atakuzidishieni nguvu juu ya nguvu zenu. Wala msigeuke mkawa wakosefu. info

Enyi watu! Mtakeni aliye kuumbeni akusameheni madhambi yaliyo kwisha tangulia. Kisha rejeeni kwake. Hapana shaka mkifanya hayo atakuleteeni mvua nyingi mfululizo, basi zitaongezeka kheri zenu, na zitazidi nguvu zenu juu ya nguvu mnazo jivunia sasa! Wala msiyawache haya ninayo kuiteni muyafwate, mkashikilia maasi ambayo yatakuangamizeni kwenye hilaki.

التفاسير:

external-link copy
53 : 11

قَالُواْ يَٰهُودُ مَا جِئۡتَنَا بِبَيِّنَةٖ وَمَا نَحۡنُ بِتَارِكِيٓ ءَالِهَتِنَا عَن قَوۡلِكَ وَمَا نَحۡنُ لَكَ بِمُؤۡمِنِينَ

Wakasema: Ewe Huud! Hujatuletea dalili wazi. Wala sisi hatuiachi miungu yetu kwa kufuata kauli yako. Na wala sisi hatukuamini wewe. info

Wakasema: Ewe Huud! Hukutuletea hoja yoyote iliyo wazi ya kuonyesha ukweli wa hayo unayo tuitia. Wala sisi hatutoacha kuabudu miungu yetu kwa kufuata kauli yako tu! Je, tuwawache hao, na hali sisi hatukusadiki wewe?

التفاسير: