ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس

رقم الصفحة:close

external-link copy
163 : 4

۞ إِنَّآ أَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡكَ كَمَآ أَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰ نُوحٖ وَٱلنَّبِيِّـۧنَ مِنۢ بَعۡدِهِۦۚ وَأَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰٓ إِبۡرَٰهِيمَ وَإِسۡمَٰعِيلَ وَإِسۡحَٰقَ وَيَعۡقُوبَ وَٱلۡأَسۡبَاطِ وَعِيسَىٰ وَأَيُّوبَ وَيُونُسَ وَهَٰرُونَ وَسُلَيۡمَٰنَۚ وَءَاتَيۡنَا دَاوُۥدَ زَبُورٗا

Hakika sisi tumekuletea wahyi, ewe Mtume, ili ufikishe ujumbe kama tulivyomletea wahyi Nūḥ na Manabii wengine baada yake. Na tumewapelekea wahyi Ibrāhīm, Ismā’īl, Isḥāq, Ya‘qūb na Asbāṭ, nao ni Manabii waliokuwa katika makabila kumi na mbili ya wana wa Isrāīl wanaotokana na kizazi cha Ya’qūb, na pia ‘Īsā, Ayyūb, Yūnus, Hārūn na Sulaimān na tukampa Dāwūd Zaburi, nacho ni kitabu na kurasa zilizoandikwa. info
التفاسير:

external-link copy
164 : 4

وَرُسُلٗا قَدۡ قَصَصۡنَٰهُمۡ عَلَيۡكَ مِن قَبۡلُ وَرُسُلٗا لَّمۡ نَقۡصُصۡهُمۡ عَلَيۡكَۚ وَكَلَّمَ ٱللَّهُ مُوسَىٰ تَكۡلِيمٗا

Na tumewatumiliza Mitume ambao tumekuelezea habari zao katika Qur’ani, kabla ya aya hii, na Mitume wengine ambao hatukukuelezea hahabari zao kwa hekima tuliyoikusudia.Na Mwenyezi Mungu Alisema na Mūsā waziwazi ili kumtukuza kwa sifa hii. Katika aya hii tukufu kuna uthibitisho wa sifa ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, ya kusema kama inavyolingana na utukufu Wake, na kwamba Yeye Mwenyezi Mungu Alisema na Nabii Wake Mūsā, amani imshukie, kikweli bila ya mtu wa kati (baina yao). info
التفاسير:

external-link copy
165 : 4

رُّسُلٗا مُّبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ لِئَلَّا يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلَى ٱللَّهِ حُجَّةُۢ بَعۡدَ ٱلرُّسُلِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَزِيزًا حَكِيمٗا

Nimweatuma wajumbe kwa viumbe wangu wakatoe habari njema ya malipo yangu mema na waonye juu ya adhabu yangu, ili wanadamu wasiwe na hoja watakayoifanya ni kisingizio cha udhuru baada ya kutumiliza Mitume. Na daima Mwenyezi Mungu ni Mshindi katika mamlaka Yake, ni Mwingi wa hekima katika uendeshaji mambo Wake. info
التفاسير:

external-link copy
166 : 4

لَّٰكِنِ ٱللَّهُ يَشۡهَدُ بِمَآ أَنزَلَ إِلَيۡكَۖ أَنزَلَهُۥ بِعِلۡمِهِۦۖ وَٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ يَشۡهَدُونَۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ شَهِيدًا

Iwapo Mayahudi na wengineo watakukanusha, ewe Mtume, hakika Mwenyezi Mungu Anashuhudia kuwa wewe ni Mtume Wake Aliyemteremshia Qur’ani tukufu; Ameiteremsha kwa ujuzi Wake. Na vilevile Malaika wanashuhudia ukweli wa wahyi uliyoletewa. Na ushahidi wa Mwenyezi Mungu Peke Yake unatosha. info
التفاسير:

external-link copy
167 : 4

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَصَدُّواْ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ قَدۡ ضَلُّواْ ضَلَٰلَۢا بَعِيدًا

Hakika wale walioupinga unabii wako na wakawazuia watu kuufuata Uislamu, wamekuwa mbali kabisa na njia ya haki. info
التفاسير:

external-link copy
168 : 4

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَظَلَمُواْ لَمۡ يَكُنِ ٱللَّهُ لِيَغۡفِرَ لَهُمۡ وَلَا لِيَهۡدِيَهُمۡ طَرِيقًا

Hakika wale waliomkanusha Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wakadhulumu kwa kuendelea kwao na ukafiri, Mwenyezi Mungu Hatakuwa ni Mwenye kuwasamehe madhambi yao wala kuwaongoza njia ya kuwaokoa. info
التفاسير:

external-link copy
169 : 4

إِلَّا طَرِيقَ جَهَنَّمَ خَٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدٗاۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى ٱللَّهِ يَسِيرٗا

Isipokuwa njia ya moto wa Jahanamu, hali ya kuwa wao ni wenye kukaa humo milele. Na hilo kwa Mwenyezi Mungu ni jepesi; hivyo basi, hakuna chenye kumshinda. info
التفاسير:

external-link copy
170 : 4

يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ قَدۡ جَآءَكُمُ ٱلرَّسُولُ بِٱلۡحَقِّ مِن رَّبِّكُمۡ فَـَٔامِنُواْ خَيۡرٗا لَّكُمۡۚ وَإِن تَكۡفُرُواْ فَإِنَّ لِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمٗا

Enyi watu, amewajia nyinyi Mjumbe wetu,Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na Uislamu, Dini ya haki, kutoka kwa Mola wenu, basi ikubalini na muifuate, kwani kuiyamini ni bora kwenu. Na iwapo mtaendelea na ukafiri wenu, basi Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, Hana haja nanyi, na pia Hana haja ya kuamini kwenu, kwa kuwa Yeye ni Mmiliki wa vilivyo mbinguni na ardhini. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi mno wa maneno yenu na vitendo vyenu, ni Mwingi wa hekima katika uwekaji Sheria Wake na amri Zake. Na iwapo mbingu na ardhi zimemnenyekea Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, katika kuwa na kukadiriwa, kama viumbe vyingine vyote vilivyomnyenyekea, basi ni bora kwenu mumwamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, muiamini Qur’ani Aliyomteramshia na muifuate Dini hiyo kisheria hadi ulimwengu wote uwe ni wenye kumnyenyekea Mwenyezi Mungu kimpango uliokadiriwa na kisheria. Katika aya hii kuna dalili ya kuwa ujumbe wa Nabii wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, unakusanya ulimwengu wote. info
التفاسير: