ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس

رقم الصفحة:close

external-link copy
238 : 2

حَٰفِظُواْ عَلَى ٱلصَّلَوَٰتِ وَٱلصَّلَوٰةِ ٱلۡوُسۡطَىٰ وَقُومُواْ لِلَّهِ قَٰنِتِينَ

Zihifadhini, enyi Waislamu, Swala tano zilizofaradhiwa kwa kudumu nazo katika kuzitekeleza kwa nyakati zake, masharuti yake, nguzo zake yanayopasa yake. Na muhufadhi swala iliyo katikati ya swala hizo, nayo ni Swala ya Alasir Na simameni katika Swala zenu hali ya kumtii Mwenyezi Mungu, kumnyenyekea na kumdhalilikia. info
التفاسير:

external-link copy
239 : 2

فَإِنۡ خِفۡتُمۡ فَرِجَالًا أَوۡ رُكۡبَانٗاۖ فَإِذَآ أَمِنتُمۡ فَٱذۡكُرُواْ ٱللَّهَ كَمَا عَلَّمَكُم مَّا لَمۡ تَكُونُواْ تَعۡلَمُونَ

Na iwapo mtawaogopa maadui maadui wenu, swalini swala ya khofu, mkiwa mwatembea au mumepanda, kwa namna yoyote ile mnayoiweza, hata kama ishara, au hata kama hamkulekea kibla. Na pindi khofu yenu itakapokwisha, swalini swala ya amani na mumtaje Mwenyezi Mungu humo. Wala msiipunguze kwakuitoa kwenye namna yake ya asili. Na mshukuruni Mwenyezi Mungu kwa kuwafundisha mambo ya ibada na hukumu ambayo hamkuwa na ujuzi nayo. info
التفاسير:

external-link copy
240 : 2

وَٱلَّذِينَ يُتَوَفَّوۡنَ مِنكُمۡ وَيَذَرُونَ أَزۡوَٰجٗا وَصِيَّةٗ لِّأَزۡوَٰجِهِم مَّتَٰعًا إِلَى ٱلۡحَوۡلِ غَيۡرَ إِخۡرَاجٖۚ فَإِنۡ خَرَجۡنَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡكُمۡ فِي مَا فَعَلۡنَ فِيٓ أَنفُسِهِنَّ مِن مَّعۡرُوفٖۗ وَٱللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٞ

Na waume wanaofariki na wakaacha wake baada yao, inawalazimu waume hao wawekee wasia hao wake zao kwamba waliwazwe mwaka mzima kuanzia siku ya kufariki, kwa kupewa Makao katika nyumba ya mume, bila ya kutolewa na mawarithi kwa muda wa mwaka. Hilo likiwa ni maliwazo kwa yule mke na ni wema kwa aliyefariki. Na iwapo wanawake hao waliofiliwa watatoka, kwa hiyari yao kabla mwaka kumalizika, basi hamna makosa, nyinyi warithi, katika hilo. Pia, hakuna makosa kwa hao wanawake kwa kitendo chao cha halali walichojifanyia nafsi zao. Mwenyezi Mungu ni Mshindi katika ufalme Wake, ni Mwingi wa hekima katika amri Zake na Makatazo Yake. Aya hii, hukumu zake zimeondolewa kwa neno Lake Mwenyezi Mungu Aliyetukaka, «Na wale wanaofariki kati yenu na wakaacha wake zao, (Basi wake hao) wajizuie nafsi zao miezi mine na siku kumi»(2:234). info
التفاسير:

external-link copy
241 : 2

وَلِلۡمُطَلَّقَٰتِ مَتَٰعُۢ بِٱلۡمَعۡرُوفِۖ حَقًّا عَلَى ٱلۡمُتَّقِينَ

Na wanawake waliotalikiwa wanastahiki wapewe kiliwazo cha mavazi na matumizi kwa mujibu wa mpango unaojulikana na kupendekezwa na kisheria. Hiyo ikiwa ni haki juu ya wale wanaomuogopa Mwenyezi Mungu katika amri Zake na Makatazo Yake. info
التفاسير:

external-link copy
242 : 2

كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمۡ ءَايَٰتِهِۦ لَعَلَّكُمۡ تَعۡقِلُونَ

Mfano wa maelezo hayo yaliyo wazi, katika hukumu za watoto na wanawake, Anawabainishia Mwenyezi Mungu mafunzo aya Zake na hukumu Zake kuhusu kila mnachokihitajia katika maisha yenu ya ulimwengu na marejeo yenu ya Akhera, ili mzitie akilini nz mzitumie. info
التفاسير:

external-link copy
243 : 2

۞ أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ خَرَجُواْ مِن دِيَٰرِهِمۡ وَهُمۡ أُلُوفٌ حَذَرَ ٱلۡمَوۡتِ فَقَالَ لَهُمُ ٱللَّهُ مُوتُواْ ثُمَّ أَحۡيَٰهُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَذُو فَضۡلٍ عَلَى ٱلنَّاسِ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَشۡكُرُونَ

Kwani hujui, ewe Mtume, kisa cha waliokimbia kutoka ardhi yao na nyumba zao, wakiwa ni maelfu mengi, wakiogopa kufa kwa sabababu ya janga la ugonjwa hatari au vita, Mwenyezi Mungu Akawaambia, «Kufeni», wakafa, papo hapo, kwa mara moja, ikiwa ni adhabu kwao kwa kukimbia kadara ya Mwenyezi Mungu, kisha Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Akawahuisha baada ya muda kupita, ili waukamilishe muda wa uhai wao, na ili wapate kuwaidhika na kutubia? Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kubwa kwa watu, kwa neema zake nyingi, lakini watu wengi hawazishukuru fadhila za Mwenyezi Mungu zilio kwao. info
التفاسير:

external-link copy
244 : 2

وَقَٰتِلُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٞ

Na piganeni nao, enyi Waislamu, hao makafiri ili kuinusuru Dini ya Mwenyezi Mungu, na mjue kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyasikia maneno yenu na ni Mwenye kuzijua nia zenu na vitendo vyenu. info
التفاسير:

external-link copy
245 : 2

مَّن ذَا ٱلَّذِي يُقۡرِضُ ٱللَّهَ قَرۡضًا حَسَنٗا فَيُضَٰعِفَهُۥ لَهُۥٓ أَضۡعَافٗا كَثِيرَةٗۚ وَٱللَّهُ يَقۡبِضُ وَيَبۡصُۜطُ وَإِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ

Ni yupi ambaye atatoa katika njia ya Mwenyezi Mungu, kutoa kuliko kuzuri kwa kutarajia malipo, Mwenyezi Mungu Apate kumuongezea nyongeza nyingi zisizohesabika za thawabu na malipo mema? Hakika Mwenyezi Mungu Anazuia na Anatoa. Kwa hivyo, toeni wala msijali, kwani Yeye Ndiye Mruzuku, Anambana Anayemtaka, miongoni mwa waja Wake, katika riziki na Anaikunjua, hiyo riziki, kwa wengine. Ana hekima kubwa katika hayo. Na Kwake Yeye Peke Yake mtarudi baada ya kufa, na hapo Atawalipa kwa vitendo vyenu. info
التفاسير: