የቅዱስ ቁርዓን ይዘት ትርጉም - የስዋሒሊኛ ትርጉም - በዐሊይ ሙሕሲን አል-በርዋኒይ

Quraish

external-link copy
1 : 106

لِإِيلَٰفِ قُرَيۡشٍ

Kwa walivyo zoea Maqureshi, info

Hebu staajabuni kwa yanayo walazimu Makureshi! Kuwalazimu safari za musimu wa baridi kwenda Yaman,

التفاسير:

external-link copy
2 : 106

إِۦلَٰفِهِمۡ رِحۡلَةَ ٱلشِّتَآءِ وَٱلصَّيۡفِ

Kuzoea kwao safari za siku za baridi na siku za joto. info

Na safari za musimu wa joto kwenda Shamu, kufanya biashara na kutafuta riziki kwa utulivu na amani. (Hizo safari za biashara za Yaman ndizo zilizo waleta Waarabu Afrika Mashariki kwa maelfu ya miaka, na zikauleta Uislamu pande za Afrika kabla ya kuenea Arabuni. Kwani nchi za Afrika Mashariki zilikaliwa na Waarabu kwa maelfu ya miaka. Soma Periplus of the Erythrean Sea, na East Africa and Its Invaders ya Prof. Coupland, na vitabu vya Sir John Gray na Dr. L.W. Hollingsworth.)

التفاسير:

external-link copy
3 : 106

فَلۡيَعۡبُدُواْ رَبَّ هَٰذَا ٱلۡبَيۡتِ

Basi nawamuabudu Mola Mlezi wa Nyumba hii, info

Basi wamtakasie ibada Mola Mlezi wa Nyumba hii aliye wawezesha kuzifanya hizi safari mbili.

التفاسير:

external-link copy
4 : 106

ٱلَّذِيٓ أَطۡعَمَهُم مِّن جُوعٖ وَءَامَنَهُم مِّنۡ خَوۡفِۭ

Ambaye anawalisha wasipate njaa, na anawalinda na khofu. info

Ambaye anawalisha wasione njaa, na hali wao wamo katika bonde lisio na makulima, na akawalinda na khofu na watu wengine pembezoni mwao wananyakuliwa.

التفاسير: