የቅዱስ ቁርዓን ይዘት ትርጉም - የስዋሒሊኛ ትርጉም - በዐሊይ ሙሕሲን አል-በርዋኒይ

Al-Asr

external-link copy
1 : 103

وَٱلۡعَصۡرِ

Naapa kwa Zama! info

Naapa kwa Zama kwa sababu ya maajabu mengi na mazingatio yaliomo ndani yake.

التفاسير:

external-link copy
2 : 103

إِنَّ ٱلۡإِنسَٰنَ لَفِي خُسۡرٍ

Hakika binaadamu bila ya shaka yumo katika khasara, info

Hakika kila binaadamu bila ya shaka yumo katika namna fulani au fulani ya kukhasiri, kwa mujibu wa anavyo ghilibiwa na pumbao na matamanio.

التفاسير:

external-link copy
3 : 103

إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ وَتَوَاصَوۡاْ بِٱلۡحَقِّ وَتَوَاصَوۡاْ بِٱلصَّبۡرِ

Ila wale walio amini, na wakatenda mema, na wakausiana kwa haki, na wakausiana kusubiri. info

Isipo kuwa wale walio muamini Mwenyezi Mungu na wakatenda mema, na wakadumu juu ya ut'iifu, na wakasemezana na kuusiana kwa kushikamana na Haki, kwa itikadi, na maneno, na vitendo. Na wakausiana wasubiri na wavumilie mashaka yanayo wapata wenye kushikamana na Dini. Basi hao ndio wenye kusalimika na hiyo khasara, wenye kufanikiwa duniani na Akhera.

التفاسير: