የቅዱስ ቁርዓን ይዘት ትርጉም - የስዋሂሊ ትርጉም - በዐብደላህ ሙሐመድ ናስር ኸሚስ

Al-Mursalat

external-link copy
1 : 77

وَٱلۡمُرۡسَلَٰتِ عُرۡفٗا

Anaapa Mwenyezi Mungu kwa upepo unapovuma kwa mfululizo, huu baada ya huu. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 77

فَٱلۡعَٰصِفَٰتِ عَصۡفٗا

Na kwa upepo wenye kuvuma kwa ukali wenye kuangamiza. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 77

وَٱلنَّٰشِرَٰتِ نَشۡرٗا

Na kwa Malaika waliopewa jukumu la mawingu, wakawa wayapeleka pale anapotaka Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 77

فَٱلۡفَٰرِقَٰتِ فَرۡقٗا

Na kwa Malaika wanaoshuka, kutoka kwa Mwenyezi Mungu, info
التفاسير:

external-link copy
5 : 77

فَٱلۡمُلۡقِيَٰتِ ذِكۡرًا

na amri zinazopambanua baina ya haki na batili na halali na haramu. info
التفاسير:

external-link copy
6 : 77

عُذۡرًا أَوۡ نُذۡرًا

Na kwa Malaika wanaoupokea wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kuuteremsha kwa Manabii Wake, unaowapa viumbe wake udhuru kutoka kwa Mwenyezi Mungu na pia onyo kutoka Kwake, ili watu wasiwe na hoja. info
التفاسير:

external-link copy
7 : 77

إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَوَٰقِعٞ

Hakika jambo la Kiyama mnaloahidiwa pamoja na lile la kuhesabiwa na kulipwa ni lenye kuwa hapana shaka. info
التفاسير:

external-link copy
8 : 77

فَإِذَا ٱلنُّجُومُ طُمِسَتۡ

Basi nyota zitakapofutwa na mwangaza wake ukaondoka, info
التفاسير:

external-link copy
9 : 77

وَإِذَا ٱلسَّمَآءُ فُرِجَتۡ

na mbingu zitakapopasuka, info
التفاسير:

external-link copy
10 : 77

وَإِذَا ٱلۡجِبَالُ نُسِفَتۡ

na majabali yatakapopeperuka na kukueanea huku na kule na yakawa ni mapepe yanayorushwa na upepo, info
التفاسير:

external-link copy
11 : 77

وَإِذَا ٱلرُّسُلُ أُقِّتَتۡ

Na Mitume watapowekewa wakati na muda wa baina yao na ummah wao na kusemwe, info
التفاسير:

external-link copy
12 : 77

لِأَيِّ يَوۡمٍ أُجِّلَتۡ

«Ni Siku kubwa gani Mitume wameahirishiwa?» info
التفاسير:

external-link copy
13 : 77

لِيَوۡمِ ٱلۡفَصۡلِ

Wameahirishiwa Siku ya hukumu na uamuzi baina ya viumbe. info
التفاسير:

external-link copy
14 : 77

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا يَوۡمُ ٱلۡفَصۡلِ

Na nilipi lililokujulisha wewe, ewe binadamu, ni siku gani hiyo ya kutolewa uamuzi na ni zipi shida zake na vituko vyake? info
التفاسير:

external-link copy
15 : 77

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ

Maangamivu makubwa Siku hiyo ni ya wale waliyoikanusha Siku hii iliyoahidiwa. info
التفاسير:

external-link copy
16 : 77

أَلَمۡ نُهۡلِكِ ٱلۡأَوَّلِينَ

Kwani hatukuawaangamiza walitangulia kati ya umma waliopita kwa kuwakanusha kwao Mitume, kama vile watu wa Nūḥ, ‘Ād na Thamūd? info
التفاسير:

external-link copy
17 : 77

ثُمَّ نُتۡبِعُهُمُ ٱلۡأٓخِرِينَ

Kisha tutawakutanisha na wao wale waliokuja nyuma kati ya wale waliokuwa ni kama wao katika ukanushaji na uasi. info
التفاسير:

external-link copy
18 : 77

كَذَٰلِكَ نَفۡعَلُ بِٱلۡمُجۡرِمِينَ

Mfano wa uangamizaji huo mkali ndivyo tutakavyowafanya wahalifu kati ya makafiri wa Makkah, kwa kumkanusha kwao Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. info
التفاسير:

external-link copy
19 : 77

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ

Maangamivu na adhabu kali Siku ya Kiyama kwa kila mwenye kuukanusha upweke wa Mwenyezi Mungu, unabii, kufufuliwa na kuhesabiwa. info
التفاسير: