የቅዱስ ቁርዓን ይዘት ትርጉም - የስዋሂሊ ትርጉም - በዐብደላህ ሙሐመድ ናስር ኸሚስ

የገፅ ቁጥር:close

external-link copy
34 : 40

وَلَقَدۡ جَآءَكُمۡ يُوسُفُ مِن قَبۡلُ بِٱلۡبَيِّنَٰتِ فَمَا زِلۡتُمۡ فِي شَكّٖ مِّمَّا جَآءَكُم بِهِۦۖ حَتَّىٰٓ إِذَا هَلَكَ قُلۡتُمۡ لَن يَبۡعَثَ ٱللَّهُ مِنۢ بَعۡدِهِۦ رَسُولٗاۚ كَذَٰلِكَ يُضِلُّ ٱللَّهُ مَنۡ هُوَ مُسۡرِفٞ مُّرۡتَابٌ

«Na Mwenyezi Mungu Aliwatumilizia kwenu Nabii mtukufu, Yūsuf mwana wa Ya’qūb, amani ziwashukie, kabla ya Mtume Mūsā, Akampatia dalili zilizo wazi juu ya ukweli wake, na Akawaamuru nyinyi kumuabudu Mwenyezi Mungu Peke Yake Asiye na mshirika, mkaendelea kuwa na shaka juu ya yale aliyokuja nayo katika kipindi cha uhai wake mpaka alipokufa. Na alipokufa shaka yenu iliongezeka na pia ushirikina wenu na mkasema, ‘Mwenyezi Mungu Hatatuma mjumbe baada yake.’ Mfano wa upotevu huu ndivyo Mwenyezi Mungu Anavyompoteza kila anayeikiuka haki, mwenye shaka juu ya upweke wa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, Asimuafikie kwenye uongofu na unyofu. info
التفاسير:

external-link copy
35 : 40

ٱلَّذِينَ يُجَٰدِلُونَ فِيٓ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ بِغَيۡرِ سُلۡطَٰنٍ أَتَىٰهُمۡۖ كَبُرَ مَقۡتًا عِندَ ٱللَّهِ وَعِندَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْۚ كَذَٰلِكَ يَطۡبَعُ ٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ قَلۡبِ مُتَكَبِّرٖ جَبَّارٖ

«Wale wanaobishana na aya za Mwenyezi Mungu na hoja Zake kwa kuzipinga bila kuwa na hoja zenye kukubalika, upinzani wao huo unawaletea machukivu makubwa kwa Mwenyezi Mungu na kwa wale walioamini, kama Alivyopiga muhuri kwenye nyoyo za hawa wapinzani na Akazifinika zisiongoke, ndivyo Anavyoupiga muhuri moyo wa kila mwenye kiburi cha kumfanya akatae kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumtii, aliye mjeuri sana kwa wingi wa udhalimu wake na uadui wake.» info
التفاسير:

external-link copy
36 : 40

وَقَالَ فِرۡعَوۡنُ يَٰهَٰمَٰنُ ٱبۡنِ لِي صَرۡحٗا لَّعَلِّيٓ أَبۡلُغُ ٱلۡأَسۡبَٰبَ

Na Fir’awn akasema akimkanusha Mūsā katika ule mwito wake wa kumkubali Mola wa viumbe wote na kujisalimisha Kwake, «Ewe Hāmān! Nijengee jengo kubwa. Huenda mimi nikafikia milango ya mbingu au nikakifikia kile chenye kunifikisha hapo, info
التفاسير:

external-link copy
37 : 40

أَسۡبَٰبَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ فَأَطَّلِعَ إِلَىٰٓ إِلَٰهِ مُوسَىٰ وَإِنِّي لَأَظُنُّهُۥ كَٰذِبٗاۚ وَكَذَٰلِكَ زُيِّنَ لِفِرۡعَوۡنَ سُوٓءُ عَمَلِهِۦ وَصُدَّ عَنِ ٱلسَّبِيلِۚ وَمَا كَيۡدُ فِرۡعَوۡنَ إِلَّا فِي تَبَابٖ

nipate kumtazama Mungu wa Mūsā mimi mwenyewe. Na mimi ninadhani kuwa Mūsā ni mrongo katika madai yake kwamba sisi tuna Mola na kwamba Yeye Yuko juu ya mbingu.» Hivyo ndivyo alivyopambiwa Fir'awn matendo yake mabaya akayadhania ni mazuri, na ndivyo alivyozuiliwa njia ya haki kwa sababu ya ubatilifu aliopambiwa nao. Na hazikuwa hila za Fir’awn na mipango yake ya kuwalaghai watu kuwa yeye yuko katika usawa na Mūsā yuko kwenye ubatilifu isipokuwa kwenye hasara na maangamivu, hakukuwa na kitu chenye kumfidisha isipokuwa ni kupata usumbufu wa duniani na Akhera. info
التفاسير:

external-link copy
38 : 40

وَقَالَ ٱلَّذِيٓ ءَامَنَ يَٰقَوۡمِ ٱتَّبِعُونِ أَهۡدِكُمۡ سَبِيلَ ٱلرَّشَادِ

Na akasema yule aliyeamini, akirudia ushauri wake, «Enyi watu wangu! Nifuateni niwaongoze njia ya uongofu na usawa. info
التفاسير:

external-link copy
39 : 40

يَٰقَوۡمِ إِنَّمَا هَٰذِهِ ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَا مَتَٰعٞ وَإِنَّ ٱلۡأٓخِرَةَ هِيَ دَارُ ٱلۡقَرَارِ

«Enyi watu wangu! Hakika ya uhai huu wa kilimwengu ni uhai wa watu kustarehe kidogo, kisha unakatika na kuondoka, basi inatakikana msiutegemee na kwamba Nyumba ya Akhera na starehe za daima zilizomo ndani ndiyo mahali pa makazi ya nyinyi kutulia humo, basi inatakikana muipe kipaumbele na mtende kwa ajili yake matendo mema ambayo yatawapatia furaha huko. info
التفاسير:

external-link copy
40 : 40

مَنۡ عَمِلَ سَيِّئَةٗ فَلَا يُجۡزَىٰٓ إِلَّا مِثۡلَهَاۖ وَمَنۡ عَمِلَ صَٰلِحٗا مِّن ذَكَرٍ أَوۡ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤۡمِنٞ فَأُوْلَٰٓئِكَ يَدۡخُلُونَ ٱلۡجَنَّةَ يُرۡزَقُونَ فِيهَا بِغَيۡرِ حِسَابٖ

«Mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu katika uhai wake na akapotoka kwenye njia ya uongofu, hatalipwa huko Akhera isipokuwa mateso yanayolingana na maasia yake. Na mwenye kumtii Mwenyezi Mungu na akafanya matendo mema, kwa kufuata maamrisho Yake na kujiepusha na makatazo Yake, awe mwanamume au mwanamke, na hali yeye ni mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na kumpwekesha, basi hao wataingia Peponi na humo Mwenyezi Mungu Atawaruzuku kutokana na matunda yake na starehe zake pasi na hesabu. info
التفاسير: