የቅዱስ ቁርዓን ይዘት ትርጉም - የስዋሂሊ ትርጉም - በዐብደላህ ሙሐመድ ናስር ኸሚስ

የገፅ ቁጥር:close

external-link copy
51 : 33

۞ تُرۡجِي مَن تَشَآءُ مِنۡهُنَّ وَتُـٔۡوِيٓ إِلَيۡكَ مَن تَشَآءُۖ وَمَنِ ٱبۡتَغَيۡتَ مِمَّنۡ عَزَلۡتَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡكَۚ ذَٰلِكَ أَدۡنَىٰٓ أَن تَقَرَّ أَعۡيُنُهُنَّ وَلَا يَحۡزَنَّ وَيَرۡضَيۡنَ بِمَآ ءَاتَيۡتَهُنَّ كُلُّهُنَّۚ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ مَا فِي قُلُوبِكُمۡۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَلِيمٗا

Unamkalisha nyuma unayemtaka miongoni mwa wake zako katika ugawaji wa kulala, na unamleta karibu nawe unayemtaka miongoni mwao. Na yoyote unayemtaka kati ya wale uliochelewesha ugawaji wao, huna dhambi katika hilo. Kwani hiyari hiyo iko karibu zaidi ya kuwafanya wao wafurahike wala wasihuzunike na waridhike wote kwa kile ulichowagawia. Na Mwenyezi Mungu Anavijua vilivyomo ndani ya nyoyo za wanaume, vya kuelemea upande wa baadhi ya wake na kutoelekea upande wa wengine. Na Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa yaliyomo ndani ya nyoyo, ni Mpole, Hafanyi haraka ya kuwatesa wanaomuasi. info
التفاسير:

external-link copy
52 : 33

لَّا يَحِلُّ لَكَ ٱلنِّسَآءُ مِنۢ بَعۡدُ وَلَآ أَن تَبَدَّلَ بِهِنَّ مِنۡ أَزۡوَٰجٖ وَلَوۡ أَعۡجَبَكَ حُسۡنُهُنَّ إِلَّا مَا مَلَكَتۡ يَمِينُكَۗ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ رَّقِيبٗا

Haifai kwako kuwaoa wanawake baada ya wake zako walio mama wa Waumini, na usiwaache wao ukawaoa wengine badala yao, kwa kuwakirimu na kushukuru mazuri waliyoyatenda ya kumchagua Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na Nyumba ya Akhera, hata kama utavutiwa na uzuri wa hao wanawake wengine, isipokuwa kile ambacho mkono wako wa kulia umemiliki, miongoni mwa wajakazi, kwani hao ni halali kwako. Na Mwenyezi Mungu anakiona kila kitu, hakuna chochote kilicho nje ya ujuzi Wake. info
التفاسير:

external-link copy
53 : 33

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَدۡخُلُواْ بُيُوتَ ٱلنَّبِيِّ إِلَّآ أَن يُؤۡذَنَ لَكُمۡ إِلَىٰ طَعَامٍ غَيۡرَ نَٰظِرِينَ إِنَىٰهُ وَلَٰكِنۡ إِذَا دُعِيتُمۡ فَٱدۡخُلُواْ فَإِذَا طَعِمۡتُمۡ فَٱنتَشِرُواْ وَلَا مُسۡتَـٔۡنِسِينَ لِحَدِيثٍۚ إِنَّ ذَٰلِكُمۡ كَانَ يُؤۡذِي ٱلنَّبِيَّ فَيَسۡتَحۡيِۦ مِنكُمۡۖ وَٱللَّهُ لَا يَسۡتَحۡيِۦ مِنَ ٱلۡحَقِّۚ وَإِذَا سَأَلۡتُمُوهُنَّ مَتَٰعٗا فَسۡـَٔلُوهُنَّ مِن وَرَآءِ حِجَابٖۚ ذَٰلِكُمۡ أَطۡهَرُ لِقُلُوبِكُمۡ وَقُلُوبِهِنَّۚ وَمَا كَانَ لَكُمۡ أَن تُؤۡذُواْ رَسُولَ ٱللَّهِ وَلَآ أَن تَنكِحُوٓاْ أَزۡوَٰجَهُۥ مِنۢ بَعۡدِهِۦٓ أَبَدًاۚ إِنَّ ذَٰلِكُمۡ كَانَ عِندَ ٱللَّهِ عَظِيمًا

Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkazifuata Sheria Zake kivitendo, msiingie nyumba za Mtume, isipokuwa kwa ruhusa yake, kwa kula chakula bila ya kungoja kuiva kwake. Lakini mkiitwa ingieni, na mkimaliza kula ondokeni, bila ya kujipumbaza kwa mazungumzo baina yenu. Kwani kule kungoja kwenu na kujipumbaza kwenu kunamkera Nabii, naye anawaonea haya kuwatoa kwenye hizo nyumba pamoja na kuwa hiyo ni haki yake, na Mwenyezi Mungu Haoni haya kuieleza haki na kuifunua. Na mkiwaomba wake za Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, wawapatie kitu chochote mnachokihitajia katika vyombo vya nyumbani na mfano wake, basi waombeni mkiwa nyuma ya pazia. Kufanya kwenu hivyo kunatakasa zaidi nyoyo zenu na nyoyo zao na kuziepusha na mawazo ambayo yanawapitia wanaume kuhusu mambo ya wanawake na wanawake kuhusu mambo ya wanaume, kwani kuona ndio sababu ya kufitinika. Na haifai kwenu kumkera Mtume wa Mwenyezi Mungu wala kuwaoa wake zake baada ya kufa kwake kabisa, kwa kuwa wao ni mama zenu, na haifai mtu kumuoa mamake. Hakika kumkera kwenu Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na kuwaoa wake zake baada yake ni dhambi kubwa kwa Mwenyezi Mungu. Ummah huu ulitekeleza amri hii na ulijiepusha na kile Mwenyezi Mungu Aliukataza nacho. info
التفاسير:

external-link copy
54 : 33

إِن تُبۡدُواْ شَيۡـًٔا أَوۡ تُخۡفُوهُ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٗا

Mkidhihirisha chochote kwa ndimi zenu, enyi watu, kati ya vitu vinavyomkera Mtume katika vile alivyowakataza navyo au mkakificha ndani ya nafsi zenu, basi Mwenyezi Mungu, aliyetukuka anavijua vilivyomo ndani ya nyoyo zenu na vile mlivyovidhihirisha, na Atawalipa kwa hayo. info
التفاسير: