Қуръони Карим маъноларининг таржимаси - Савоҳилийча таржима - Али Муҳсин ал-Бервааний

Al-Lail

external-link copy
1 : 92

وَٱلَّيۡلِ إِذَا يَغۡشَىٰ

Naapa kwa usiku unapo funika! info

Naapa kwa usiku kinapo enea kiza chake!

التفاسير:

external-link copy
2 : 92

وَٱلنَّهَارِ إِذَا تَجَلَّىٰ

Na mchana unapo dhihiri! info

Na naapa kwa mchana unapo zagaa mwangaza wake!

التفاسير:

external-link copy
3 : 92

وَمَا خَلَقَ ٱلذَّكَرَ وَٱلۡأُنثَىٰٓ

Na kwa Aliye umba dume na jike! info

Na naapa kwa Mjuzi aliye umba viwili viwili, dume na jike, katika kila vinavyo zaliwa!

التفاسير:

external-link copy
4 : 92

إِنَّ سَعۡيَكُمۡ لَشَتَّىٰ

Hakika juhudi zenu bila ya shaka ni mbali mbali. info

Hakika juhudi zenu bila ya shaka zimekhitalifiana; kwani wapo wenye kubahatika katika juhudi zao, na wako wasio bahatika.

التفاسير:

external-link copy
5 : 92

فَأَمَّا مَنۡ أَعۡطَىٰ وَٱتَّقَىٰ

Ama mwenye kutoa na akamchamngu! info

Ama mwenye kutoa katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na akamkhofu Mola wake Mlezi, na kwa hivyo akaepuka anayo yakataza,

التفاسير:

external-link copy
6 : 92

وَصَدَّقَ بِٱلۡحُسۡنَىٰ

Na akaliwafiki lilio jema! info

Na akayakinika kufuata fadhila njema, nayo ni Imani kumuamini Mwenyezi Mungu kwa kumjua,

التفاسير:

external-link copy
7 : 92

فَسَنُيَسِّرُهُۥ لِلۡيُسۡرَىٰ

Tutamsahilishia yawe mepesi. info

Basi Sisi tutamtengenezea awe katika khulka ya wepesi na raha kwa kumwongoza kwenye njia ya kheri.

التفاسير:

external-link copy
8 : 92

وَأَمَّا مَنۢ بَخِلَ وَٱسۡتَغۡنَىٰ

Na ama mwenye kufanya ubakhili, na asiwe na haja ya wenzake! info

Ama mwenye kufanya ubakhili kwa mali yake asitoe haki ya Mwenyezi Mungu iliomo humo, na akawa hana haja na yatokayo kwa Mwenyezi Mungu,

التفاسير:

external-link copy
9 : 92

وَكَذَّبَ بِٱلۡحُسۡنَىٰ

Na akakanusha lilio jema! info

Na akakadhibisha khulka nzuri,

التفاسير:

external-link copy
10 : 92

فَسَنُيَسِّرُهُۥ لِلۡعُسۡرَىٰ

Tutamsahilishia yawe mazito! info

Basi huyo tutamtengenezea khulka ambayo inapelekea uzito na mashaka ya milele.

التفاسير:

external-link copy
11 : 92

وَمَا يُغۡنِي عَنۡهُ مَالُهُۥٓ إِذَا تَرَدَّىٰٓ

Na mali yake yatamfaa nini atapo kuwa anadidimia? info

Na kitu gani katika adhabu ambacho hayo mali yake yataweza kumkinga nacho, atapo teketea yeye mwenyewe mzima?

التفاسير:

external-link copy
12 : 92

إِنَّ عَلَيۡنَا لَلۡهُدَىٰ

Hakika ni juu yetu kuonyesha uwongofu. info

Hakika ni juu yetu, Sisi, kwa kufuatana na hikima yetu, ndio tuwabainishie viumbe njia ya uwongofu.

التفاسير:

external-link copy
13 : 92

وَإِنَّ لَنَا لَلۡأٓخِرَةَ وَٱلۡأُولَىٰ

Na hakika ni yetu Sisi Akhera na dunia. info

Na juu yetu Sisi peke yetu, bila ya shaka, hili jambo la kuendesha yaliomo duniani na Akhera.

التفاسير:

external-link copy
14 : 92

فَأَنذَرۡتُكُمۡ نَارٗا تَلَظَّىٰ

Basi nakuonyeni na Moto unao waka! info

Ndio maana tukakutieni khofu ya Moto unao waka na kuripuka!

التفاسير:

external-link copy
15 : 92

لَا يَصۡلَىٰهَآ إِلَّا ٱلۡأَشۡقَى

Hatauingia ila mwovu kabisa! info

Hawauingii kwa kudumu ila kafiri

التفاسير:

external-link copy
16 : 92

ٱلَّذِي كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ

Anaye kadhibisha na kupa mgongo. info

Aliye ikadhibisha Haki na akazipuuza Ishara za Mola wake Mlezi.

التفاسير:

external-link copy
17 : 92

وَسَيُجَنَّبُهَا ٱلۡأَتۡقَى

Na mchamngu ataepushwa nao, info

Na atakuwa mbali na huo Moto aliye mwingi wa kujikinga na ukafiri na maasi,

التفاسير:

external-link copy
18 : 92

ٱلَّذِي يُؤۡتِي مَالَهُۥ يَتَزَكَّىٰ

Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa. info

Amabye hutoa mali yake wakati wa nafasi ili kujisafisha na uchafu wa ubakhili, na najsi ya uchoyo.

التفاسير:

external-link copy
19 : 92

وَمَا لِأَحَدٍ عِندَهُۥ مِن نِّعۡمَةٖ تُجۡزَىٰٓ

Na wala si kwa kuwa yupo yeyote aliye mfanyia hisani ndio anamlipa. info

Na mtoaji huyu si kama anaye mtu yeyote ambaye ndio anamlipa kwa neema aliyo mfanyia zamani,

التفاسير:

external-link copy
20 : 92

إِلَّا ٱبۡتِغَآءَ وَجۡهِ رَبِّهِ ٱلۡأَعۡلَىٰ

Ila ni kutaka radhi ya Mola wake Mlezi aliye juu kabisa. info

Bali anatoa hicho kwa kutafuta radhi ya Mola wake Mlezi Mtukufu tu.

التفاسير:

external-link copy
21 : 92

وَلَسَوۡفَ يَرۡضَىٰ

Naye atakuja ridhika! info

Na bila ya shaka atakuja pata kutoka kwa Mola wake Mlezi anacho kitaka kwa njia za ukamilifu kabisa, hata itimie radhi kwake.

التفاسير: