Қуръони Карим маъноларининг таржимаси - Савоҳилийча таржима - Али Муҳсин ал-Бервааний

external-link copy
70 : 11

فَلَمَّا رَءَآ أَيۡدِيَهُمۡ لَا تَصِلُ إِلَيۡهِ نَكِرَهُمۡ وَأَوۡجَسَ مِنۡهُمۡ خِيفَةٗۚ قَالُواْ لَا تَخَفۡ إِنَّآ أُرۡسِلۡنَآ إِلَىٰ قَوۡمِ لُوطٖ

Basi alipoona mikono yao haimfikilii aliwatilia shaka, na akawaogopa. Wakasema: Usiogope! Hakika sisi tumetumwa kwa kaumu ya Lut'. info

Alipoona kuwa hawanyooshi mikono yao kama ada ya wageni akawatilia shaka kuwa hawa si wageni wa kawaida, na akahisi kuwa hawa ni Malaika. Ikamjia khofu kuwa isije kuwa kuja kwao ni kwa jambo ambalo halikumpendeza Mwenyezi Mungu, au kuwaadhibu watu wake. Wakasema, nao walijua athari ya ile khofu katika nafsi yake: Usiogope! Hakika sisi tumetumwa kuwahiliki kaumu Lut'.

التفاسير: