Қуръони Карим маъноларининг таржимаси - Савоҳилча таржима

Бет рақами:close

external-link copy
48 : 74

فَمَا تَنفَعُهُمۡ شَفَٰعَةُ ٱلشَّٰفِعِينَ

Basi hayatawafalia neno maombezi ya wenye kuombea wote, miongoni mwa Malaika, Manabii na wengineo, kwa kuwa aombewaye ni yule aliyechaguliwa na Mwenyezi Mungu na akamuidhinisha mwenye kumuombea. info
التفاسير:

external-link copy
49 : 74

فَمَا لَهُمۡ عَنِ ٱلتَّذۡكِرَةِ مُعۡرِضِينَ

Basi wana nini hawa washirikina wamejiepusha na Qur’ani na info
التفاسير:

external-link copy
50 : 74

كَأَنَّهُمۡ حُمُرٞ مُّسۡتَنفِرَةٞ

mawaidha yaliyomo ndani yake? Kama kwamba wao ni pundamilia wanaobabaika info
التفاسير:

external-link copy
51 : 74

فَرَّتۡ مِن قَسۡوَرَةِۭ

wanaomkimbia simba mshambulizi. info
التفاسير:

external-link copy
52 : 74

بَلۡ يُرِيدُ كُلُّ ٱمۡرِيٕٖ مِّنۡهُمۡ أَن يُؤۡتَىٰ صُحُفٗا مُّنَشَّرَةٗ

Lakini kila mmoja, miongoni mwa hawa washirikina, ana matumaini ateremshiwe kitabu kutoka mbinguni kilichokunjuliwa kama kile kilichoteremshiwa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. info
التفاسير:

external-link copy
53 : 74

كَلَّاۖ بَل لَّا يَخَافُونَ ٱلۡأٓخِرَةَ

Mambo si hivyo kama wanavyodai. Ukweli ni kwamba wao hawaiogopi Akhera wala hawaamini kuwa kuna kufufuliwa na kulipwa. info
التفاسير:

external-link copy
54 : 74

كَلَّآ إِنَّهُۥ تَذۡكِرَةٞ

Ni kweli kwamba Qur’ani ni mawaidha yenye ufasaha, yanayotosha kuwafanya wao wawaidhike. info
التفاسير:

external-link copy
55 : 74

فَمَن شَآءَ ذَكَرَهُۥ

Anayetaka kuwaidhika, basi na awaidhike kwa yaliyomo ndani yake na anufaike na uongofu wake. info
التفاسير:

external-link copy
56 : 74

وَمَا يَذۡكُرُونَ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُۚ هُوَ أَهۡلُ ٱلتَّقۡوَىٰ وَأَهۡلُ ٱلۡمَغۡفِرَةِ

Na hawawaidhiki kwayo isipokuwa iwapo Mwenyezi Mungu Amewatakia kuongoka. Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Ndiye Anayestahiki kuogopewa na kutiiwa, na Ndiye Anayestahiki kumsamehe anayemuamini Yeye na kumtii. info
التفاسير: