Қуръони Карим маъноларининг таржимаси - Савоҳилча таржима

Бет рақами:close

external-link copy
13 : 20

وَأَنَا ٱخۡتَرۡتُكَ فَٱسۡتَمِعۡ لِمَا يُوحَىٰٓ

Na mimi nimekuteua , ewe Mūsā, kwa ujumbe wangu, basi sikiliza yale unayoletewa ya wahyi kutoka kwangu. info
التفاسير:

external-link copy
14 : 20

إِنَّنِيٓ أَنَا ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّآ أَنَا۠ فَٱعۡبُدۡنِي وَأَقِمِ ٱلصَّلَوٰةَ لِذِكۡرِيٓ

Mimi Ndiye Mwenyezi Mungu, hakuna mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa mimi, sina mshirika, basi niabudu mimi na usimamishe Swala ili unikumbuke ndani yake. info
التفاسير:

external-link copy
15 : 20

إِنَّ ٱلسَّاعَةَ ءَاتِيَةٌ أَكَادُ أُخۡفِيهَا لِتُجۡزَىٰ كُلُّ نَفۡسِۭ بِمَا تَسۡعَىٰ

Hakika Kiyama ambacho watu hapo watafufuliwa hapana budi ni chenye kutukia. Nakaribia kukificha kwangu mimi mwenyewe, basi ni vipi atakijua mtu yoyote miongoni mwa viumbe. Hivyo ni apate kulipwa kila mtu kwa alilolitenda ulimwenguni, liwe zuri au baya. info
التفاسير:

external-link copy
16 : 20

فَلَا يَصُدَّنَّكَ عَنۡهَا مَن لَّا يُؤۡمِنُ بِهَا وَٱتَّبَعَ هَوَىٰهُ فَتَرۡدَىٰ

Basi asikuepushe, ewe Mūsā, na kukiamini na kujitayarisha nacho, asiyekikubali kuwa kitatukia na asiyetenda ya kumfaa huko na akayafuata matamanio ya nafsi yake na akakikanusha, kwani ukifanya hivyo utaangamia. info
التفاسير:

external-link copy
17 : 20

وَمَا تِلۡكَ بِيَمِينِكَ يَٰمُوسَىٰ

Na ni nini hii iliyo kwenye mkono wako wa kulia, ewe Mūsā? info
التفاسير:

external-link copy
18 : 20

قَالَ هِيَ عَصَايَ أَتَوَكَّؤُاْ عَلَيۡهَا وَأَهُشُّ بِهَا عَلَىٰ غَنَمِي وَلِيَ فِيهَا مَـَٔارِبُ أُخۡرَىٰ

Akasema Mūsā, «Hii ni ni fimbo yangu, naitegemea katika kwenda na ninapigia miti ili mbuzi wangu walishe majani yake yanayoanguka na pia nina maslahi nayo mengine.» info
التفاسير:

external-link copy
19 : 20

قَالَ أَلۡقِهَا يَٰمُوسَىٰ

Mwenyezi Mungu Akamwambia Mūsā, «Itupe fimbo yako!» info
التفاسير:

external-link copy
20 : 20

فَأَلۡقَىٰهَا فَإِذَا هِيَ حَيَّةٞ تَسۡعَىٰ

Mūsā akaitupa chini, ikageuka kwa amri ya Mwenyezi Mungu ikawa nyoka anayetembea, na Mūsā akaona jambo kubwa na akazunguka kukimbia. info
التفاسير:

external-link copy
21 : 20

قَالَ خُذۡهَا وَلَا تَخَفۡۖ سَنُعِيدُهَا سِيرَتَهَا ٱلۡأُولَىٰ

Mwenyezi Mungu Akasema kumwambia Mūsā, «Mshike huyo nyoka na usimuogope, tutamrudisha kuwa fimbo vile alivyokuwa mwanzo. info
التفاسير:

external-link copy
22 : 20

وَٱضۡمُمۡ يَدَكَ إِلَىٰ جَنَاحِكَ تَخۡرُجۡ بَيۡضَآءَ مِنۡ غَيۡرِ سُوٓءٍ ءَايَةً أُخۡرَىٰ

Na ukumbatie mkono wako kwenye ubavu wako chini ya shina la mkono utatoka hali ni mweupe kama barafu bila ya kuwa na mbalanga, ili iwe ni alama nyingine. info
التفاسير:

external-link copy
23 : 20

لِنُرِيَكَ مِنۡ ءَايَٰتِنَا ٱلۡكُبۡرَى

Tumefanya hivyo ili kukuonesha , ewe Mūsā, dalili zetu kubwa zenye kutolea ushahidi uweza wetu, ukubwa wa ufalme wetu na usahihi wa utume wako. info
التفاسير:

external-link copy
24 : 20

ٱذۡهَبۡ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ إِنَّهُۥ طَغَىٰ

Enda, ewe Mūsā, kwa Fir'awn, kwa kuwa yeye amepitisha kipimo chake na ametoka kwenye utiifu wa Mola wake, umuite kwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumuabudu. info
التفاسير:

external-link copy
25 : 20

قَالَ رَبِّ ٱشۡرَحۡ لِي صَدۡرِي

Mūsā akasema, «Ewe Mola wangu! Nikunjulie kifua changu, info
التفاسير:

external-link copy
26 : 20

وَيَسِّرۡ لِيٓ أَمۡرِي

nirahisishie mambo yangu info
التفاسير:

external-link copy
27 : 20

وَٱحۡلُلۡ عُقۡدَةٗ مِّن لِّسَانِي

na nifungulie ulimi wangu uwe na ufasaha wa matamshi, info
التفاسير:

external-link copy
28 : 20

يَفۡقَهُواْ قَوۡلِي

ili waelewe maneno yangu. info
التفاسير:

external-link copy
29 : 20

وَٱجۡعَل لِّي وَزِيرٗا مِّنۡ أَهۡلِي

Na unipatie msaidizi miongoni mwa watu wangu, info
التفاسير:

external-link copy
30 : 20

هَٰرُونَ أَخِي

naye ni Hārūn ndugu yangu. info
التفاسير:

external-link copy
31 : 20

ٱشۡدُدۡ بِهِۦٓ أَزۡرِي

Nitilie nguvu kwa yeye na uuthibitishe mgongo wangu kwa ajili yake. info
التفاسير:

external-link copy
32 : 20

وَأَشۡرِكۡهُ فِيٓ أَمۡرِي

Na umshirikishe na mimi katika unabii na ufikishaji ujumbe. info
التفاسير:

external-link copy
33 : 20

كَيۡ نُسَبِّحَكَ كَثِيرٗا

Tupate kukuepusha na kila sifa ya upungufu na tukutakase kwa wingi, info
التفاسير:

external-link copy
34 : 20

وَنَذۡكُرَكَ كَثِيرًا

na tukutaje kwa wingi na tukushukuru. info
التفاسير:

external-link copy
35 : 20

إِنَّكَ كُنتَ بِنَا بَصِيرٗا

Kwa hakika, wewe ni mwenye kutuona, hakuna chochote kinachofichika kwako miongoni mwa vitendo vyetu.» info
التفاسير:

external-link copy
36 : 20

قَالَ قَدۡ أُوتِيتَ سُؤۡلَكَ يَٰمُوسَىٰ

Mwenyezi Mungu Akasema, «Nishakupa kila ulichokiomba, ewe Mūsā. info
التفاسير:

external-link copy
37 : 20

وَلَقَدۡ مَنَنَّا عَلَيۡكَ مَرَّةً أُخۡرَىٰٓ

«Na tulikupa , ewe Mūsā, kabla ya neema hii, neema nyingine ulipokuwa ni mtoto wa kunyonya tukakuokoa na unyanyasaji wa Fir'awn. info
التفاسير: