قرآن کریم کے معانی کا ترجمہ - سواحلی ترجمہ - علی محسن البروانی

Al-Alaq

external-link copy
1 : 96

ٱقۡرَأۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلَّذِي خَلَقَ

Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba! info

Ewe Muhammad! Soma unayo funuliwa kwa kufunguliwa kwa Jina la Mola wako Mlezi ambaye ni Yeye tu peke yake ndiye Mwenye uweza wa kuumba.

التفاسير:

external-link copy
2 : 96

خَلَقَ ٱلۡإِنسَٰنَ مِنۡ عَلَقٍ

Amemuumba binaadamu kwa tone la damu! info

Amemuumba mtu kwa ukamilifu wa mwili wake na ilimu kutokana na kipande cha damu ambacho hakina chochote cha kupelekea kujiona bora.

التفاسير:

external-link copy
3 : 96

ٱقۡرَأۡ وَرَبُّكَ ٱلۡأَكۡرَمُ

Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote! info

Endelea na kusoma, na Mola wako Mlezi aliye Karimu kushinda wote, atakutukuza wala hatakudharau.

التفاسير:

external-link copy
4 : 96

ٱلَّذِي عَلَّمَ بِٱلۡقَلَمِ

Ambaye amefundisha kwa kalamu. info

Yeye ndiye ambaye aliye mfunza mtu kuandika kwa kalamu, na wala kwanza hakuwa anajua hayo.

التفاسير:

external-link copy
5 : 96

عَلَّمَ ٱلۡإِنسَٰنَ مَا لَمۡ يَعۡلَمۡ

Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui. info

Amemfunza mtu yasiyo kuwa yanampitia katika mawazo yake.

التفاسير:

external-link copy
6 : 96

كَلَّآ إِنَّ ٱلۡإِنسَٰنَ لَيَطۡغَىٰٓ

Kwani! Hakika mtu bila ya shaka huwa jeuri. info

Ni hakika kweli mtu hupindukia mpaka na hupanda kiburi mbele ya Mola wake Mlezi

التفاسير:

external-link copy
7 : 96

أَن رَّءَاهُ ٱسۡتَغۡنَىٰٓ

Akijiona katajirika. info

Anapo jiona si mhitaji, katajirika.

التفاسير:

external-link copy
8 : 96

إِنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ ٱلرُّجۡعَىٰٓ

Hakika kwa Mola wako Mlezi ndio marejeo. info

Ewe Muhammad! Hakika ni kwa Mola wako Mlezi peke yake ndiyo yako marejeo ya wote kwa kufufuliwa na kulipwa.

التفاسير:

external-link copy
9 : 96

أَرَءَيۡتَ ٱلَّذِي يَنۡهَىٰ

Umemwona yule anaye mkataza. info

Je! Umemwona huyu jeuri

التفاسير:

external-link copy
10 : 96

عَبۡدًا إِذَا صَلَّىٰٓ

Mja anapo sali? info

Anaye mzuia mja asisali anapo taka kusali?

التفاسير:

external-link copy
11 : 96

أَرَءَيۡتَ إِن كَانَ عَلَى ٱلۡهُدَىٰٓ

Umeona kama yeye yuko juu ya uwongofu? info

Hebu niambie khabari za jeuri huyu kama yeye yumo katika uwongofu katika huku kuzuia kwake,

التفاسير:

external-link copy
12 : 96

أَوۡ أَمَرَ بِٱلتَّقۡوَىٰٓ

Au anaamrisha uchamngu? info

Au kwamba ndio anaamrisha uchamngu katika hayo anayo amrisha!

التفاسير:

external-link copy
13 : 96

أَرَءَيۡتَ إِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰٓ

Umeona kama yeye akikanusha na anarudi nyuma? info

Niambie khabari za huyu mwenye kukataza anapo yakadhibisha aliyo kuja nayo Mtume, na akapuuza Imani na vitendo vyema!

التفاسير:

external-link copy
14 : 96

أَلَمۡ يَعۡلَم بِأَنَّ ٱللَّهَ يَرَىٰ

Hajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anaona? info

Hivyo hajui kwamba Mwenyezi Mungu anazijua vyema hali zake, naye atamlipa kwazo?

التفاسير:

external-link copy
15 : 96

كَلَّا لَئِن لَّمۡ يَنتَهِ لَنَسۡفَعَۢا بِٱلنَّاصِيَةِ

Kwani! Kama haachi, tutamkokota kwa shungi la nywele! info

Kwa kumkemea huyu mwenye kuzuia, anaambiwa kama hakuacha hayo anayo yafanya, basi hapana shaka tutamkokota kwa nguvu tukimshika kwa shungi lake la nywele mpaka Motoni!

التفاسير:

external-link copy
16 : 96

نَاصِيَةٖ كَٰذِبَةٍ خَاطِئَةٖ

Shungi la uwongo, lenye makosa! info

Hilo shungi lilio juu ya uso wake mwenye kuropokwa uwongo na mwenye athari za ukosefu!

التفاسير:

external-link copy
17 : 96

فَلۡيَدۡعُ نَادِيَهُۥ

Basi na awaite wenzake! info

Basi yeye awaite wenziwe na watu wa baraza lake wawe ndio wasaidizi duniani au Akhera.

التفاسير:

external-link copy
18 : 96

سَنَدۡعُ ٱلزَّبَانِيَةَ

Nasi tutawaita Mazabania! info

Sisi tutawaita askari wetu wamsaidie Muhammad na walio pamoja naye, na wapambane na huyo mwenye kukanya na wasaidizi wawasukume kwenye Jahannamu!

التفاسير:

external-link copy
19 : 96

كَلَّا لَا تُطِعۡهُ وَٱسۡجُدۡۤ وَٱقۡتَرِب۩

Hasha! Usimt'ii! Nawe sujudu na ujongee! info

Kumnyamazisha huyu mwenye kuzuia, wewe usimkubalie kwa hayo anayo kukataza nayo, na dumu juu ya Swala zako, na endelea na sijida zako, na jijongeze kwa Mola wako Mlezi kwa hivyo.

التفاسير: