قرآن کریم کے معانی کا ترجمہ - سواحلی ترجمہ - علی محسن البروانی

external-link copy
14 : 9

قَٰتِلُوهُمۡ يُعَذِّبۡهُمُ ٱللَّهُ بِأَيۡدِيكُمۡ وَيُخۡزِهِمۡ وَيَنصُرۡكُمۡ عَلَيۡهِمۡ وَيَشۡفِ صُدُورَ قَوۡمٖ مُّؤۡمِنِينَ

Piganeni nao, Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa mikono yenu, na awahizi na akunusuruni muwashinde, na avipoze vifua vya kaumu ya Waumini, info

Enyi Waumini, piganeni nao! Mwenyezi Mungu atawaonjesha adhabu itokayo mikononi mwenu, na atawadhalilisha na atakupeni ushindi juu yao. Na kwa kuwashinda hao, na kuunyanyua utukufu wa Uislamu, Mwenyezi Mungu atayapoza machungu yaliyomo katika vifua vya Waumini, yaliyo fichikana na yaliyo dhihiri, wakati wote walipo kuwa wakipata maudhi ya makafiri.

التفاسير: