قرآن کریم کے معانی کا ترجمہ - سواحلی ترجمہ - عبد اللہ محمد اور ناصر خمیس

صفحہ نمبر:close

external-link copy
36 : 27

فَلَمَّا جَآءَ سُلَيۡمَٰنَ قَالَ أَتُمِدُّونَنِ بِمَالٖ فَمَآ ءَاتَىٰنِۦَ ٱللَّهُ خَيۡرٞ مِّمَّآ ءَاتَىٰكُمۚ بَلۡ أَنتُم بِهَدِيَّتِكُمۡ تَفۡرَحُونَ

Mjumbe wa malkia alipokuja na tunu kwa Sulaymān, alisema Sulaymān, akilikataa hilo na akizungumzia neema za Mwenyezi Mungu juu yake, «Mnanipatia mali ili kuniridhisha? Yale aliyonipa Mwenyezi Mungu ya unabii, ufalme na mali mengi ni mazuri zaidi na ni bora zaidi kuliko hayo Aliyowapa nyinyi, bali nyinyi ndio mnaofurahia tunu mnayotunukiwa, kwa kuwa nyinyi ni watu wa kuonyeshana kwa kujifahiri na dunia na kuipapia kwa wingi.» info
التفاسير:

external-link copy
37 : 27

ٱرۡجِعۡ إِلَيۡهِمۡ فَلَنَأۡتِيَنَّهُم بِجُنُودٖ لَّا قِبَلَ لَهُم بِهَا وَلَنُخۡرِجَنَّهُم مِّنۡهَآ أَذِلَّةٗ وَهُمۡ صَٰغِرُونَ

Na Sulaymān, amani imshukiye, akasema kumwambia mjumbe wa watu wa Saba’, «Rejea kwao, kwani naapa kwa Mwenyezi Mungu, tutawajia wao na askari wasioweza kupambana nao na kukabiliana nao, na tutawatoa kutoka nchini mwao wakiwa wadhalilifu, hali ya kuwa wanyonge wenye kudharauliwa, iwapo hawatafuata Dini ya Mwenyezi Mungu Peke Yake na hawataacha kumuabudu asiyekuwa Yeye.» info
التفاسير:

external-link copy
38 : 27

قَالَ يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡمَلَؤُاْ أَيُّكُمۡ يَأۡتِينِي بِعَرۡشِهَا قَبۡلَ أَن يَأۡتُونِي مُسۡلِمِينَ

Sulaymān akasema akiwahutubia wale ambao Mwenyezi Mungu Amemdhalilishia miongoni mwa majini na binadamu, «Ni nani kati yenu ataniletea kitanda cha ufalme wake kabla hawajanijia wakiwa katika hali ya kufuata na kutii?» info
التفاسير:

external-link copy
39 : 27

قَالَ عِفۡرِيتٞ مِّنَ ٱلۡجِنِّ أَنَا۠ ءَاتِيكَ بِهِۦ قَبۡلَ أَن تَقُومَ مِن مَّقَامِكَۖ وَإِنِّي عَلَيۡهِ لَقَوِيٌّ أَمِينٞ

Akasema afriti wa kijini mwenye nguvu na ukali, «Mimi nitakuletea kabla hujainuka kutoka kwenye kikao chako hiki unachokaa kuhukumu baina ya watu. Na mimi ni mwenye nguvu na uwezo wa kukibeba, ni muaminifu wa kuvitunza vilivyomo ndani yake, nitakuja nacho kama kilivyo, sikipunguzi kitu chake chochote wala sikigeuzi.» info
التفاسير:

external-link copy
40 : 27

قَالَ ٱلَّذِي عِندَهُۥ عِلۡمٞ مِّنَ ٱلۡكِتَٰبِ أَنَا۠ ءَاتِيكَ بِهِۦ قَبۡلَ أَن يَرۡتَدَّ إِلَيۡكَ طَرۡفُكَۚ فَلَمَّا رَءَاهُ مُسۡتَقِرًّا عِندَهُۥ قَالَ هَٰذَا مِن فَضۡلِ رَبِّي لِيَبۡلُوَنِيٓ ءَأَشۡكُرُ أَمۡ أَكۡفُرُۖ وَمَن شَكَرَ فَإِنَّمَا يَشۡكُرُ لِنَفۡسِهِۦۖ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ رَبِّي غَنِيّٞ كَرِيمٞ

Akasema yule ambaye alikuwa na ujuzi kutoka kwenye Kitabu, «Mimi nitakuletea hiko kitanda kabla ya kupepesa macho yako yanapogeuka kuangalia kitu.» Sulaymān akamruhusu, naye akamuomba Mwenyezi Mungu na akakileta kitanda cha kifalme. Alipokiona Sulaymān kimehudhurishwa mbele yake na kimethibiti alisema, «Huu ni miongoni mwa wema wa Mola wangu Aliyeniumba na akaumba ulimwengu wote ili kunitahini mimi nitalishukuru hilo kwa kutambua neema Yake Aliyetukuka au nitakufuru kwa kuacha kushukuru? Na mwenye kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema Zake, nafuu ya hilo itamrudia yeye mwenyewe, na mwenye kukanusha neema na akaacha kushukuru, basi hakika Mola wangu Ametosheka Hahitajii shukrani yake, ni Karimu ambaye kheri Yake inamuenea hapa duniani mwenye kushukuru na mwenye kukufuru, kisha Atawahesabu huko Akhera na awalipe. info
التفاسير:

external-link copy
41 : 27

قَالَ نَكِّرُواْ لَهَا عَرۡشَهَا نَنظُرۡ أَتَهۡتَدِيٓ أَمۡ تَكُونُ مِنَ ٱلَّذِينَ لَا يَهۡتَدُونَ

Sulaymān akasema kuwaambia walioko mbele yake, «Kibadilisheni kitanda cha ufalme wake ambacho anakaa juu yake kwa namna ya yeye kutokitambua akikiona, tuone: ataelekezeka kukijua au atakuwa ni kati ya wale wasioelekezeka?» info
التفاسير:

external-link copy
42 : 27

فَلَمَّا جَآءَتۡ قِيلَ أَهَٰكَذَا عَرۡشُكِۖ قَالَتۡ كَأَنَّهُۥ هُوَۚ وَأُوتِينَا ٱلۡعِلۡمَ مِن قَبۡلِهَا وَكُنَّا مُسۡلِمِينَ

Alipokuja malkia wa Saba ’.kwa Sulaymān kwenye kikao chake aliambiwa, «je, kitanda cha ufalme wako kiko hivi?» Akasema, «Hicho kinafanana nacho.» Ikambainikia Sulaymān kuwa amejibu jawabu la sawa na ameshajua uweza wa Mwenyezi Mungu na usahihi wa unabii wa Sulaymān , amani imshukiye. Na tulipewa elimu ya kumjua Mwenyezi Mungu na kujuwa uweza Wake kabla yake yeye, na tulikuwa ni wenye kuifuata amri ya Mwenyezi Mungu ni wenye kuifuata dini ya Uislamu.» info
التفاسير:

external-link copy
43 : 27

وَصَدَّهَا مَا كَانَت تَّعۡبُدُ مِن دُونِ ٱللَّهِۖ إِنَّهَا كَانَتۡ مِن قَوۡمٖ كَٰفِرِينَ

Na kilimzuia yeye kumuabudu Mwenyezi Mungu Peke Yake kile alichokuwa akikiabudu badala ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka,. Kwa hakika yeye alikuwa ni kafiri na alikulia kati ya watu makafiri na akaendelea kwenye dini yao, isipokuwa hivyo, yeye ana werevu na busara ya kuijua haki na kuipambanua na batili, lakini itikadi za ubatilifu zinaondoa nuru ya moyo. info
التفاسير:

external-link copy
44 : 27

قِيلَ لَهَا ٱدۡخُلِي ٱلصَّرۡحَۖ فَلَمَّا رَأَتۡهُ حَسِبَتۡهُ لُجَّةٗ وَكَشَفَتۡ عَن سَاقَيۡهَاۚ قَالَ إِنَّهُۥ صَرۡحٞ مُّمَرَّدٞ مِّن قَوَارِيرَۗ قَالَتۡ رَبِّ إِنِّي ظَلَمۡتُ نَفۡسِي وَأَسۡلَمۡتُ مَعَ سُلَيۡمَٰنَ لِلَّهِ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Akaambiwa, «Ingia kwenye jumba.» na ukumbi wake ulikuwa wa ukoa, chini yake palikuwa na maji. Alipouona ukumbi alidhania ni maji yanayopiga mawimbi, na akafunua miguu yake ili kuingia majini. Sulaymān akamwambia, «Huo ni ukumbi laini wa ukoa ulio safi na maji yako chini yake.» Akatambua ukubwa wa ufalme wa Sulaymān na akasema, «Mola wangu! Nimeidhulumu nafsi yangu kwa ushirikina niliokuwa nao, na nimesalimu amri kwa kumfuata Sulaymān kwa kuingia kwenye dini ya Mola wa viumbe wote.» info
التفاسير: