قرآن کریم کے معانی کا ترجمہ - سواحلی ترجمہ - عبد اللہ محمد اور ناصر خمیس

external-link copy
59 : 19

۞ فَخَلَفَ مِنۢ بَعۡدِهِمۡ خَلۡفٌ أَضَاعُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَٱتَّبَعُواْ ٱلشَّهَوَٰتِۖ فَسَوۡفَ يَلۡقَوۡنَ غَيًّا

Wakaja, baada ya hawa walioneemeshwa, wafuasi wabaya, waliacha Swala kabisa au waliitoa nje ya wakati wake au waliacha nguzo zake na mambo yake ya lazima na wakafuata yanayolingana na kunasibiana na matamanio yao. Basi hao watapata shari na upotevu na kupita patupu ndani ya Jahanamu. info
التفاسير: