قۇرئان كەرىم مەنىلىرىنىڭ تەرجىمىسى - ساۋاھىلچە تەرجىمىسى - روۋاد تەرجىمە مەركىزى

بەت نومۇرى:close

external-link copy
21 : 9

يُبَشِّرُهُمۡ رَبُّهُم بِرَحۡمَةٖ مِّنۡهُ وَرِضۡوَٰنٖ وَجَنَّٰتٖ لَّهُمۡ فِيهَا نَعِيمٞ مُّقِيمٌ

Mola wao Mlezi anawabashiria rehema zitokazo kwake, na radhi, na Bustani ambazo humo wana neema za kudumu. info
التفاسير:

external-link copy
22 : 9

خَٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدًاۚ إِنَّ ٱللَّهَ عِندَهُۥٓ أَجۡرٌ عَظِيمٞ

Watadumu humo milele. Hakika kwa Mwenyezi Mungu yapo malipo makubwa. info
التفاسير:

external-link copy
23 : 9

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَتَّخِذُوٓاْ ءَابَآءَكُمۡ وَإِخۡوَٰنَكُمۡ أَوۡلِيَآءَ إِنِ ٱسۡتَحَبُّواْ ٱلۡكُفۡرَ عَلَى ٱلۡإِيمَٰنِۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمۡ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلظَّٰلِمُونَ

Enyi mlioamini! Msiwafanye baba zenu na ndugu zenu kuwa marafiki walinzi wenu ikiwa wanaupendelea ukafiri kuliko Imani. Na mwenye kuwafanya marafiki walinzi miongoni mwenu, basi hao ndio madhalimu. info
التفاسير:

external-link copy
24 : 9

قُلۡ إِن كَانَ ءَابَآؤُكُمۡ وَأَبۡنَآؤُكُمۡ وَإِخۡوَٰنُكُمۡ وَأَزۡوَٰجُكُمۡ وَعَشِيرَتُكُمۡ وَأَمۡوَٰلٌ ٱقۡتَرَفۡتُمُوهَا وَتِجَٰرَةٞ تَخۡشَوۡنَ كَسَادَهَا وَمَسَٰكِنُ تَرۡضَوۡنَهَآ أَحَبَّ إِلَيۡكُم مِّنَ ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَجِهَادٖ فِي سَبِيلِهِۦ فَتَرَبَّصُواْ حَتَّىٰ يَأۡتِيَ ٱللَّهُ بِأَمۡرِهِۦۗ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡفَٰسِقِينَ

Sema: Ikiwa baba zenu, na wana wenu, na ndugu zenu, na wake zenu, na jamaa zenu, na mali mlizozichuma, na biashara mnazohofia kuharibika kwake, na makazi mnayoyaridhia, ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kufanya Jihadi katika Njia yake, basi ngojeni mpaka Mwenyezi Mungu aje na amri yake. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu wavukao mipaka. info
التفاسير:

external-link copy
25 : 9

لَقَدۡ نَصَرَكُمُ ٱللَّهُ فِي مَوَاطِنَ كَثِيرَةٖ وَيَوۡمَ حُنَيۡنٍ إِذۡ أَعۡجَبَتۡكُمۡ كَثۡرَتُكُمۡ فَلَمۡ تُغۡنِ عَنكُمۡ شَيۡـٔٗا وَضَاقَتۡ عَلَيۡكُمُ ٱلۡأَرۡضُ بِمَا رَحُبَتۡ ثُمَّ وَلَّيۡتُم مُّدۡبِرِينَ

Hakika Mwenyezi Mungu aliwanusuru katika maeneo mengi, na siku ya Hunayni wakati wingi wenu uliwapa majivuno, lakini haukuwafaa kitu, na ardhi ikawa finyu kwenu pamoja na upana wake. Kisha mkageuka mkapeana migongo. info
التفاسير:

external-link copy
26 : 9

ثُمَّ أَنزَلَ ٱللَّهُ سَكِينَتَهُۥ عَلَىٰ رَسُولِهِۦ وَعَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَأَنزَلَ جُنُودٗا لَّمۡ تَرَوۡهَا وَعَذَّبَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْۚ وَذَٰلِكَ جَزَآءُ ٱلۡكَٰفِرِينَ

Kisha Mwenyezi Mungu akateremsha utulivu wake juu ya Mtume wake na juu ya Waumini. Na akateremsha majeshi ambayo hamkuyaona, na akawaadhibu wale waliokufuru. Na hayo ndiyo malipo ya makafiri. info
التفاسير: