قۇرئان كەرىم مەنىلىرىنىڭ تەرجىمىسى - ساۋاھىلچە تەرجىمىسى - روۋاد تەرجىمە مەركىزى

external-link copy
20 : 2

يَكَادُ ٱلۡبَرۡقُ يَخۡطَفُ أَبۡصَٰرَهُمۡۖ كُلَّمَآ أَضَآءَ لَهُم مَّشَوۡاْ فِيهِ وَإِذَآ أَظۡلَمَ عَلَيۡهِمۡ قَامُواْۚ وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ لَذَهَبَ بِسَمۡعِهِمۡ وَأَبۡصَٰرِهِمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Unakaribia umeme kunyakua macho yao. Kila ukiwatolea mwangaza, wanatembea ndani yake. Na linapowawia giza, wanasimama. Na angelitaka Mwenyezi Mungu angeliondoa kusikia kwao na kuona kwao. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.[1] info

[1] Aya imemalizika kwa kusema: "Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu." Kwa sababu aliwaonya wanafiki juu ya adhabu yake na uwezo wake, na akawaambia kwamba amewazunguka, na kwamba ana uwezo wa kuondoa kusikia na kuona kwao. (Tafsir Ibn Kathir)

التفاسير: