قۇرئان كەرىم مەنىلىرىنىڭ تەرجىمىسى - سەۋاھىلچە تەرجىمىسى. ئەلىي مۇھسىن بەرۋانىي قىلغان

external-link copy
62 : 8

وَإِن يُرِيدُوٓاْ أَن يَخۡدَعُوكَ فَإِنَّ حَسۡبَكَ ٱللَّهُۚ هُوَ ٱلَّذِيٓ أَيَّدَكَ بِنَصۡرِهِۦ وَبِٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Na wakitaka kukukhadaa basi Mwenyezi Mungu atakutosheleza. Kwani Yeye ndiye aliye kuunga mkono kwa nusura yake na kwa Waumini. info

Ikiwa hao maadui wanataka kukukhadaa na kukufanyia ujanja kwa hivyo kuonyesha kuwa wanataka amani, basi Mwenyezi Mungu anakutosheleza kukulinda na vitimbi vyao kwa kila upande. Kwani Yeye alikwisha tangulia kukuunga mkono kwa kukupa ushindi pale alipo kutengenezea sababu zilizo onekana na za siri za kutia imara nyoyo za Waumini katika Wahajiri, wahamiaji walio toka Makka, na Ansari, wasaidizi wa Madina.

التفاسير: