قۇرئان كەرىم مەنىلىرىنىڭ تەرجىمىسى - قۇرئان كەرىمنىڭ ساۋاھىلچە تەرجىمىسىنى ئابدۇللا مۇھەممەد ۋە ناسىر خەمىيس تەرجىمە قىلغان.

Al-Balad

external-link copy
1 : 90

لَآ أُقۡسِمُ بِهَٰذَا ٱلۡبَلَدِ

Mwenyezi Mungu Anaapa kwa mji huu mtakatifu wa Makkah. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 90

وَأَنتَ حِلُّۢ بِهَٰذَا ٱلۡبَلَدِ

Na wewe, ewe Nabii, ni mkazi wa mji huu mtakatifu. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 90

وَوَالِدٖ وَمَا وَلَدَ

Na Anaapa kwa mzazi wa wanaadamu, ambaye ni Ādam, amani imshukie, na kilichozalikana na yeye. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 90

لَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ فِي كَبَدٍ

Hakika Tumemuumba binadamu katika usumbufu na shida za kilimwengu. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 90

أَيَحۡسَبُ أَن لَّن يَقۡدِرَ عَلَيۡهِ أَحَدٞ

Kwani anadhani kwa mali aliyoyakusanya kuwa Mwenyezi Mungu Hatakuwa na uwezo juu yake? info
التفاسير:

external-link copy
6 : 90

يَقُولُ أَهۡلَكۡتُ مَالٗا لُّبَدًا

Huwa akisema kwa kujigamba: «Nimetumia mali mengi.» info
التفاسير:

external-link copy
7 : 90

أَيَحۡسَبُ أَن لَّمۡ يَرَهُۥٓ أَحَدٌ

Kwani anadhani, kwa kitendo chake hiko, kuwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na kushinda, Hamuoni wala hatamhesabu juu ya kubwa na dogo? info
التفاسير:

external-link copy
8 : 90

أَلَمۡ نَجۡعَل لَّهُۥ عَيۡنَيۡنِ

Kwani hatukumpa macho mawili ya kuonea, info
التفاسير:

external-link copy
9 : 90

وَلِسَانٗا وَشَفَتَيۡنِ

ulimi na midomo miwili ya kusemea info
التفاسير:

external-link copy
10 : 90

وَهَدَيۡنَٰهُ ٱلنَّجۡدَيۡنِ

na kumfafanulia njia mbili: ya kheri na ya shari? info
التفاسير:

external-link copy
11 : 90

فَلَا ٱقۡتَحَمَ ٱلۡعَقَبَةَ

Basi ajiepushe na janga la Akhera kwa kutoa mali yake ili aokoke. info
التفاسير:

external-link copy
12 : 90

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡعَقَبَةُ

Ni kitu gani kilichojulisha ni lipi hilo janga la Akhera na ni mambo gani yenye kusaidia kujiepusha nalo? info
التفاسير:

external-link copy
13 : 90

فَكُّ رَقَبَةٍ

Ni kuacha huru shingo iliyoamini kuikomboa na utumwa. info
التفاسير:

external-link copy
14 : 90

أَوۡ إِطۡعَٰمٞ فِي يَوۡمٖ ذِي مَسۡغَبَةٖ

Au kulisha, wakati wa shida ya njaa, info
التفاسير:

external-link copy
15 : 90

يَتِيمٗا ذَا مَقۡرَبَةٍ

yatima mwenye ujamaa, ili ipatikane fadhila ya sadaka na ya kuunga kizazi, info
التفاسير:

external-link copy
16 : 90

أَوۡ مِسۡكِينٗا ذَا مَتۡرَبَةٖ

au masikini asiyekuwa na kitu. info
التفاسير:

external-link copy
17 : 90

ثُمَّ كَانَ مِنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَتَوَاصَوۡاْ بِٱلصَّبۡرِ وَتَوَاصَوۡاْ بِٱلۡمَرۡحَمَةِ

Kisha akawa, baada ya kufanya amali njema zilizotajwa, ni miongoni mwa waliotakasa Imani yao kwa Mwenyezi Mungu, wakausiana kusubiri juu ya kumtii Mwenyezi Mungu kwa kufuata maamrisho Yake na kujiepusha na vitendo vya kumuasi na wakausiana kuwahurumia viumbe. info
التفاسير:

external-link copy
18 : 90

أُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَيۡمَنَةِ

Wenye kufanya hayo ndiwo watu wa kulia ambao watapelekwa Siku ya Kiyama upande wa kulia kuelekea Peponi. info
التفاسير:

external-link copy
19 : 90

وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِـَٔايَٰتِنَا هُمۡ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَشۡـَٔمَةِ

Na wale waliokanusha Qur’ani ndio ambao watapelekwa, Siku ya Kiyama, upande wa kushoto kuelekea Motoni. info
التفاسير:

external-link copy
20 : 90

عَلَيۡهِمۡ نَارٞ مُّؤۡصَدَةُۢ

Malipo yao ni Moto wa Jahanamu wenye kuwafinika na kuwaziba. info
التفاسير: