قۇرئان كەرىم مەنىلىرىنىڭ تەرجىمىسى - قۇرئان كەرىمنىڭ ساۋاھىلچە تەرجىمىسىنى ئابدۇللا مۇھەممەد ۋە ناسىر خەمىيس تەرجىمە قىلغان.

Al-Haqqah

external-link copy
1 : 69

ٱلۡحَآقَّةُ

Kiyama chenye kutukia kikweli ambacho ndani yake inahakikika ahadi ya Mwenyezi Mungu na onyo Lake. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 69

مَا ٱلۡحَآقَّةُ

Kiyama chenye kutukia kikweli ni zipi sifa zake na hali zake? info
التفاسير:

external-link copy
3 : 69

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡحَآقَّةُ

Na kitu gani kilichokujulisha wewe, ewe Mtume, na kukueleza uhakika wa Kiyama na kikakupa wewe picha ya janga lake na shida zake? info
التفاسير:

external-link copy
4 : 69

كَذَّبَتۡ ثَمُودُ وَعَادُۢ بِٱلۡقَارِعَةِ

Thamūd, nao ni watu wa Ṣāliḥ, na ‘Ād, nao ni watu wa Hūd, walikikanusha Kiyama ambacho kinagonga nyoyo kwa vituko janga lake. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 69

فَأَمَّا ثَمُودُ فَأُهۡلِكُواْ بِٱلطَّاغِيَةِ

Ama hao Thamūd waliangamizwa kwa ukelele mkubwa uliopita kiasi ukali wake, info
التفاسير:

external-link copy
6 : 69

وَأَمَّا عَادٞ فَأُهۡلِكُواْ بِرِيحٖ صَرۡصَرٍ عَاتِيَةٖ

na ama‘Ād waliangamizwa kwa upepo baridi unaovuma kwa nguvu. info
التفاسير:

external-link copy
7 : 69

سَخَّرَهَا عَلَيۡهِمۡ سَبۡعَ لَيَالٖ وَثَمَٰنِيَةَ أَيَّامٍ حُسُومٗاۖ فَتَرَى ٱلۡقَوۡمَ فِيهَا صَرۡعَىٰ كَأَنَّهُمۡ أَعۡجَازُ نَخۡلٍ خَاوِيَةٖ

Mwenyezi Mungu Aliwasaliti nao masiku saba na michana minane yenye kufuatana, isiyokatika wala kusimama. Utawaona watu katika masiku hayo na michana wamekufa, kama kwamba wao ni vigogo mitende iliyo mibovu iliyolika ndani. info
التفاسير:

external-link copy
8 : 69

فَهَلۡ تَرَىٰ لَهُم مِّنۢ بَاقِيَةٖ

Basi je utamuona mtu yoyote miongoni mwao mwenye kusalia bila kuangamia? info
التفاسير: