قۇرئان كەرىم مەنىلىرىنىڭ تەرجىمىسى - قۇرئان كەرىمنىڭ ساۋاھىلچە تەرجىمىسىنى ئابدۇللا مۇھەممەد ۋە ناسىر خەمىيس تەرجىمە قىلغان.

Al-Qalam

external-link copy
1 : 68

نٓۚ وَٱلۡقَلَمِ وَمَا يَسۡطُرُونَ

«Nūn» Yametangulia maelezo kuhusu herufi zilizokatwakatwa na kutengwa mwanzo wa sura ya Al-Baqarah. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 68

مَآ أَنتَ بِنِعۡمَةِ رَبِّكَ بِمَجۡنُونٖ

Anaapa Mwenyezi Mungu kwa Kalamu ambayo kwayo Malaika na watu wanaandikia, na kwa kile wanachokiandika cha kheri, manufaa na aina za elimu. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 68

وَإِنَّ لَكَ لَأَجۡرًا غَيۡرَ مَمۡنُونٖ

Hukuwa wewe, ewe Mtume, kwa sababu ya neema ya Mwenyezi Mungu kwako, ya unabii na utume, ni mchache wa akili wala mwenye uduni wa maoni. Na wewe una malipo makubwa yasiyopunguzwa wala kukatwa kwa yale matatizo unayopambana nayo ya ufikishaji ujumbe. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 68

وَإِنَّكَ لَعَلَىٰ خُلُقٍ عَظِيمٖ

Na hakika wewe, ewe Mtume, uko juu ya tabia kubwa, nazo ni zile tabia njema zilizomo kwenye Qur’ani. Kwani kule kuifuata Qur’ani kulikuwa ni sifa yake, akitekeleza amri zake na kukomeka na yale yanayokatazwa nayo. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 68

فَسَتُبۡصِرُ وَيُبۡصِرُونَ

Kwa kipindi cha karibu kijacho, utaona ewe Mtume, na wataona info
التفاسير:

external-link copy
6 : 68

بِأَييِّكُمُ ٱلۡمَفۡتُونُ

makafiri ugonjwa wa akili na wazimu viko kwa nani miongoni mwenu? info
التفاسير:

external-link copy
7 : 68

إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعۡلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِۦ وَهُوَ أَعۡلَمُ بِٱلۡمُهۡتَدِينَ

Hakika Mola wako , kutakasika ni Kwake, Ndiye Mjuzi zaidi wa kumjua mpotofu aliyeenda kombo na Dini ya Mwenyezi Mungu na njia ya uongofu, na Yeye Ndiye Mjuzi zaidi wa kumjua mchamungu aliyeongoka kwenye njia ya haki. info
التفاسير:

external-link copy
8 : 68

فَلَا تُطِعِ ٱلۡمُكَذِّبِينَ

Basi jikite kwenye msimamo ulionao, ewe Mtume, wa kuenda kinyume na wakanushaji, na wala usiwatii. info
التفاسير:

external-link copy
9 : 68

وَدُّواْ لَوۡ تُدۡهِنُ فَيُدۡهِنُونَ

Wanatamani na wanapenda lau wewe unakuwa laini kwao na kuwakubalia baadhi ya misimamo waliyonayo, na wao wakawa laini kwako. info
التفاسير:

external-link copy
10 : 68

وَلَا تُطِعۡ كُلَّ حَلَّافٖ مَّهِينٍ

Usimkubalie, ewe Mtume, kila mtu mweye kuapa mayamini sana, info
التفاسير:

external-link copy
11 : 68

هَمَّازٖ مَّشَّآءِۭ بِنَمِيمٖ

mrongo sana, mtwevu, msengenyaji watu, anayetembea baina yao kwa kuchochea ugomvi na kuchukua maneno ya baadhi yao kuwapelekea wengine kwa lengo la kuharibu baina yao, bahili wa mali mwenye uchoyo wa kuyatumia katika njia ya haki, info
التفاسير:

external-link copy
12 : 68

مَّنَّاعٖ لِّلۡخَيۡرِ مُعۡتَدٍ أَثِيمٍ

mwenye kuzuia sana ufanyaji wema, anayevuka mpaka wake katika kuwafanyia watu uadui na kutumia yaliyohartamishwa, mwingi wa madhambi, info
التفاسير:

external-link copy
13 : 68

عُتُلِّۭ بَعۡدَ ذَٰلِكَ زَنِيمٍ

mshupavu katika ukafiri wake, mchafu na muovu na anayenasibishwa na baba asiye wake. info
التفاسير:

external-link copy
14 : 68

أَن كَانَ ذَا مَالٖ وَبَنِينَ

Na kwa kuwa yeye ni mwenye mali na wana ndipo akakiuka mipaka na akaifanyia kiburi haki. info
التفاسير:

external-link copy
15 : 68

إِذَا تُتۡلَىٰ عَلَيۡهِ ءَايَٰتُنَا قَالَ أَسَٰطِيرُ ٱلۡأَوَّلِينَ

Ikawa akisomewa aya za Qur’ani na mtu yoyote huzikanusha na kusema kuwa hizo ni maneno ya urongo na itikadi za watu waliopita. Aya hizi, ingawa zimeteremka kwa baadhi ya washirikina, kama vile al-Walīd bin \al-Mughīrah, zina onyo ndani yake kwa Muislamu asikubaliane na anayesifika kwa sifa hizi zenye kutukanika. info
التفاسير:

external-link copy
16 : 68

سَنَسِمُهُۥ عَلَى ٱلۡخُرۡطُومِ

Tutaweka alama ya kudumu juu ya pua yake isiyomuepuka, ili afedheheke mbele za watu. info
التفاسير:

external-link copy
17 : 68

إِنَّا بَلَوۡنَٰهُمۡ كَمَا بَلَوۡنَآ أَصۡحَٰبَ ٱلۡجَنَّةِ إِذۡ أَقۡسَمُواْ لَيَصۡرِمُنَّهَا مُصۡبِحِينَ

Sisi tumewatahini watu wa Makkah kwa njaa na ukame kama tulivyowatahini wenye shamba walipoapa wakiwa pamoja kwamba watakwenda kuvuna matunda ya shamba lao asubuhi mapema, ili wasiokuwa wao, kati ya masikini na mfano wao, wasipate kula katika mavuno hayo. info
التفاسير:

external-link copy
18 : 68

وَلَا يَسۡتَثۡنُونَ

Na wasiseme walipopanga hayo, «Mwenyezi Mungu Akitaka». info
التفاسير:

external-link copy
19 : 68

فَطَافَ عَلَيۡهَا طَآئِفٞ مِّن رَّبِّكَ وَهُمۡ نَآئِمُونَ

Mwenyezi Mungu akaliteremshia shamba hilo moto ukaliteketeza kipindi cha usiku na hali wao wakiwa wamelala. info
التفاسير:

external-link copy
20 : 68

فَأَصۡبَحَتۡ كَٱلصَّرِيمِ

Na likapambaukiwa nalo lishachomeka limekuwa leusi kama usiku wa giza. info
التفاسير:

external-link copy
21 : 68

فَتَنَادَوۡاْ مُصۡبِحِينَ

Hapo wakaitana kipindi cha asubuhi. info
التفاسير:

external-link copy
22 : 68

أَنِ ٱغۡدُواْ عَلَىٰ حَرۡثِكُمۡ إِن كُنتُمۡ صَٰرِمِينَ

«Haya tokeni mapema mwende kwenye shamba lenu iwapo bado mnataka kuvuna matunda!» info
التفاسير:

external-link copy
23 : 68

فَٱنطَلَقُواْ وَهُمۡ يَتَخَٰفَتُونَ

Wakatoka kwa haraka, huku wakinong’ onezana, info
التفاسير:

external-link copy
24 : 68

أَن لَّا يَدۡخُلَنَّهَا ٱلۡيَوۡمَ عَلَيۡكُم مِّسۡكِينٞ

«Leo msimpe nafasi masikini yoyote kuingia shamba lenu.» info
التفاسير:

external-link copy
25 : 68

وَغَدَوۡاْ عَلَىٰ حَرۡدٖ قَٰدِرِينَ

Wakaenda kipindi cha mwanzo wa mchana kuelekea kwenye shamba lao wakiwa na lengo baya la kuwanyima masikini matunda ya shamba, wakiwa wana uwezo kamili wa kulitekeleza hilo kulingana na madai yao. info
التفاسير:

external-link copy
26 : 68

فَلَمَّا رَأَوۡهَا قَالُوٓاْ إِنَّا لَضَآلُّونَ

Walipolishuhudia shamba lao limechomeka walilikataa na wakasema, ‘Kwa hakika tumepotea njia ya kulifikia!» na walipojua kuwa hilo ndilo shamba lao walisema, info
التفاسير:

external-link copy
27 : 68

بَلۡ نَحۡنُ مَحۡرُومُونَ

«Bali sisi tumekoseshwa mazao yake kwa sababu ya nia yetu ya uchoyo na kuwanyima masikini.» info
التفاسير:

external-link copy
28 : 68

قَالَ أَوۡسَطُهُمۡ أَلَمۡ أَقُل لَّكُمۡ لَوۡلَا تُسَبِّحُونَ

Akasema muadilifu zaidi miongoni mwao, «Kwani sikuwaambia myafunge maneno yenu na matakwa ya mwenyezi Mungu kwa kusema ‘Mwenyezi Mungu Akitaka’?» info
التفاسير:

external-link copy
29 : 68

قَالُواْ سُبۡحَٰنَ رَبِّنَآ إِنَّا كُنَّا ظَٰلِمِينَ

Hapo wakasema, baada ya kurudi kwenye fahamu za uongofu, «Mwenyezi Mungu Mola wetu Ametakasika na udhalimu katika haya yaliyotupata, lakini ni sisi ndio tuliojidhulumu nafsi zetu kwa kuacha kuyafunga maneno yetu na matakwa ya Mwenyezi Mungu na kwa lengo letu baya.» info
التفاسير:

external-link copy
30 : 68

فَأَقۡبَلَ بَعۡضُهُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٖ يَتَلَٰوَمُونَ

Wakazungukiana wao kwa wao wakilaumiana kwa kuacha kuyafunga maneno yao na matakwa ya Mwenyezi Mungu na kwa lengo lao baya, info
التفاسير:

external-link copy
31 : 68

قَالُواْ يَٰوَيۡلَنَآ إِنَّا كُنَّا طَٰغِينَ

wakasema, «Ewe ole wetu! Sisi tulikuwa tumekiuka mpaka kwa kuwanyima masikini na kuenda kinyume na amri ya Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
32 : 68

عَسَىٰ رَبُّنَآ أَن يُبۡدِلَنَا خَيۡرٗا مِّنۡهَآ إِنَّآ إِلَىٰ رَبِّنَا رَٰغِبُونَ

Tunatarajia kwa Mola wetu kuwa Atatupa kilicho bora zaidi kuliko shamba letu, kwa kuwa tumetubia na tumekubali makosa yetu. Sisi tuna matumaini mema kwa Mola wetu, tunatarajia msamaha na tunaomba kheri. Mfano wa mateso hayo tuliyowatesa nayo wenye shamba ndivyo yanavyokuwa mateso yetu duniani kwa kila anayeenda kinyume na amri ya Mwenyezi Mungu na akazifanyia uchoyo neema za Mwenyezi Mungu Alizompa kwa kutotekeleza haki ya Mwenyezi Mungu katika neema hizo. info
التفاسير:

external-link copy
33 : 68

كَذَٰلِكَ ٱلۡعَذَابُۖ وَلَعَذَابُ ٱلۡأٓخِرَةِ أَكۡبَرُۚ لَوۡ كَانُواْ يَعۡلَمُونَ

Na kwa hakika adhabu ya Mwenyezi Mungu ni kubwa zaidi na ni kali zaidi kuliko adhabu ya duniani. Lau wao wangalijua wangalijiepusha na kila jambo lenye kusababisha kupata mateso hayo. info
التفاسير:

external-link copy
34 : 68

إِنَّ لِلۡمُتَّقِينَ عِندَ رَبِّهِمۡ جَنَّٰتِ ٱلنَّعِيمِ

Hakika wale waliojikinga na mateso ya Mwenyezi Mungu kwa kufanya yale Aliyowaamrisha na kuacha yale Aliyoyakataza, watapata kwa Mola wao huko Akhera, mabustani ya Peponi ambayo ndani yake kuna starehe za daima. info
التفاسير:

external-link copy
35 : 68

أَفَنَجۡعَلُ ٱلۡمُسۡلِمِينَ كَٱلۡمُجۡرِمِينَ

Je tuwafanye wale wanaomnyenyekea Mwenyezi Mungu kwa kumtii ni kama wale waliokufuru? info
التفاسير:

external-link copy
36 : 68

مَا لَكُمۡ كَيۡفَ تَحۡكُمُونَ

Mna nini nyinyi? Vipi mnatoa uamuzi huu wa kudhalimu, mkalinganisha baina yao katika malipo? info
التفاسير:

external-link copy
37 : 68

أَمۡ لَكُمۡ كِتَٰبٞ فِيهِ تَدۡرُسُونَ

Au nyinyi mna kitabu kilichoteremshwa kutoka mbinguni ambacho mnakuta ndani yake kuwa mtiifu ni kama muasi, mkawa mnayasoma hayo mnayoyasema? info
التفاسير:

external-link copy
38 : 68

إِنَّ لَكُمۡ فِيهِ لَمَا تَخَيَّرُونَ

Hivyo basi nyinyi ndani ya kitabu hiki mna kila mnachokitamani. Basi hilo nyinyi hamnalo. info
التفاسير:

external-link copy
39 : 68

أَمۡ لَكُمۡ أَيۡمَٰنٌ عَلَيۡنَا بَٰلِغَةٌ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ إِنَّ لَكُمۡ لَمَا تَحۡكُمُونَ

Au nyinyi mna ahadi na mapatano ya lazima juu yetu kuwa mtapata mnayoyataka na kuyatamani? info
التفاسير:

external-link copy
40 : 68

سَلۡهُمۡ أَيُّهُم بِذَٰلِكَ زَعِيمٌ

Waulize washirikina, ewe Mtume, «Ni yupi katika wao anayeichukulia hukumu hiyo dhamana na ahadi kwamba atayapata hayo?» info
التفاسير:

external-link copy
41 : 68

أَمۡ لَهُمۡ شُرَكَآءُ فَلۡيَأۡتُواْ بِشُرَكَآئِهِمۡ إِن كَانُواْ صَٰدِقِينَ

Au wau wana waungu wanaowachukulia dhamana kwa wanayoyasema na kuwasaidia kuyafikia hayo wanayoyataka? Basi na wawalete iwapo wao ni wakweli katika madai yao. info
التفاسير:

external-link copy
42 : 68

يَوۡمَ يُكۡشَفُ عَن سَاقٖ وَيُدۡعَوۡنَ إِلَى ٱلسُّجُودِ فَلَا يَسۡتَطِيعُونَ

Siku ya Kiyama, mambo yatakuwa magumu na kituko chake kitakuwa kikubwa, na hapo Mwenyezi Mungu Aje ili kutoa uamuzi baina ya viumbe, Afunue muundi Wake usiofanana na kitu chochote. Amesema, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, «Atafunua Mola wetu muundi Wake, hapo amsujudie kila mwanamume aliyeamini na mwanamke aliyeamini, na atasalia yule aliyekuwa akisujudu duniani kwa kujionesha na kusikika, aende kusujudu na mgongo wake ugeuke kuwa mfupa mmoja.» Imepokewa na Bukhari na Muslim. info
التفاسير:

external-link copy
43 : 68

خَٰشِعَةً أَبۡصَٰرُهُمۡ تَرۡهَقُهُمۡ ذِلَّةٞۖ وَقَدۡ كَانُواْ يُدۡعَوۡنَ إِلَى ٱلسُّجُودِ وَهُمۡ سَٰلِمُونَ

Yatakuwa yameinama macho yao, hawayainui, wamefinikwa na unyonge mkubwa kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu, na hali wao walikuwa ulimwenguni wakiitwa kuswali na kumumuabudu Mwenyezi Mungu wakiwa na nguvu zao na uwezo wa kufanya hivyo, wakawa hawasujudu kwa kiburi na kujiona wakubwa. info
التفاسير:

external-link copy
44 : 68

فَذَرۡنِي وَمَن يُكَذِّبُ بِهَٰذَا ٱلۡحَدِيثِۖ سَنَسۡتَدۡرِجُهُم مِّنۡ حَيۡثُ لَا يَعۡلَمُونَ

Basi, niache, ewe Mtume, na wale wanaoikanusha hii Qur’ani! Ni juu yangu kuwalipa na kuwatesa. Tutawanyoshea mambo yao kwa kuwapa mali, watoto na neema nyiginezo kwa njia ya kuwavutavuta kwa namna ya wao kutofahamu kuwa hiyo ndiyo njia ya kuwaangamiza. info
التفاسير:

external-link copy
45 : 68

وَأُمۡلِي لَهُمۡۚ إِنَّ كَيۡدِي مَتِينٌ

Na ninawapa muhula na kuurefusha umri wao, wapate kuendelea kufanya dhambi. Hakika vitimbi vyangu kwa watu makafiri ni vya nguvu na vikali. info
التفاسير:

external-link copy
46 : 68

أَمۡ تَسۡـَٔلُهُمۡ أَجۡرٗا فَهُم مِّن مَّغۡرَمٖ مُّثۡقَلُونَ

Au unaomba, ewe Mtume, hawa washirikina ujira wa kidunia kwa kuufikisha ujumbe, hivyo basi wao wakawa wamelazimishwa kubeba mzigo mzito wa gharama? info
التفاسير:

external-link copy
47 : 68

أَمۡ عِندَهُمُ ٱلۡغَيۡبُ فَهُمۡ يَكۡتُبُونَ

Au wao wana ujuzi wa ghaibu, wakawa wanaandika kutokana nao kile wanachokiamulia nafsi zao kwamba wao wana cheo bora zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko wale wenye kumuamini? info
التفاسير:

external-link copy
48 : 68

فَٱصۡبِرۡ لِحُكۡمِ رَبِّكَ وَلَا تَكُن كَصَاحِبِ ٱلۡحُوتِ إِذۡ نَادَىٰ وَهُوَ مَكۡظُومٞ

Basi vumilia, ewe Mtume, kwa kile Alichokiamua Mola wako na kukipitisha. Na miongoni mwa hivyo ni kuwapa muhula na kuchelewesha ushindi wako kwao. Na usiwe ni kama yule mtu wa chewa, naye ni Yūnus, amani imshukie, alipokasirika na kutokuwa na uvumilivu na watu wake, pindi alipomuita Mola Wake, na huku amejawa na makero, akimuomba Awaharakishie adhabu, info
التفاسير:

external-link copy
49 : 68

لَّوۡلَآ أَن تَدَٰرَكَهُۥ نِعۡمَةٞ مِّن رَّبِّهِۦ لَنُبِذَ بِٱلۡعَرَآءِ وَهُوَ مَذۡمُومٞ

lau si yeye kufikiwa na neema ya Mola Wake kwa kumwafikia kutubia, angalitupwa chini, kutoka tumboni mwa chewa, kwenye ardhi kavu yenye kuangamiza, na hali amefanya jambo la kulaumiwa. info
التفاسير:

external-link copy
50 : 68

فَٱجۡتَبَٰهُ رَبُّهُۥ فَجَعَلَهُۥ مِنَ ٱلصَّٰلِحِينَ

Mola Wake Akamchagua kwa ujumbe Wake, Akamjaalia ni miongoni mwa watu wema waliokuwa wazuri wa nia, matendo na maneno. info
التفاسير:

external-link copy
51 : 68

وَإِن يَكَادُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَيُزۡلِقُونَكَ بِأَبۡصَٰرِهِمۡ لَمَّا سَمِعُواْ ٱلذِّكۡرَ وَيَقُولُونَ إِنَّهُۥ لَمَجۡنُونٞ

Kwa hakika wanakaribia makafiri wanapoisikia Qur’ani kukudhuru kwa jicho la uhasidi kwa kukuchukia, lau si Mwenyezi Mungu kukuokoa na kukuhami, na wanasema kwa matamanio yao kwamba yeye ni Mwendawazimu. info
التفاسير:

external-link copy
52 : 68

وَمَا هُوَ إِلَّا ذِكۡرٞ لِّلۡعَٰلَمِينَ

Na haikuwa Qur’ani isipokuwa ni mawaidha na ukumbusho kwa viumbe wote miongoni mwa binadamu na majini. info
التفاسير: