قۇرئان كەرىم مەنىلىرىنىڭ تەرجىمىسى - قۇرئان كەرىمنىڭ ساۋاھىلچە تەرجىمىسىنى ئابدۇللا مۇھەممەد ۋە ناسىر خەمىيس تەرجىمە قىلغان.

بەت نومۇرى:close

external-link copy
12 : 58

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِذَا نَٰجَيۡتُمُ ٱلرَّسُولَ فَقَدِّمُواْ بَيۡنَ يَدَيۡ نَجۡوَىٰكُمۡ صَدَقَةٗۚ ذَٰلِكَ خَيۡرٞ لَّكُمۡ وَأَطۡهَرُۚ فَإِن لَّمۡ تَجِدُواْ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٌ

Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkafuata Sheria Zake kivitendo! Mkitaka kusema na Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kwa siri baina yenu na yeye, basi tangulizeni kabla ya hilo kutoa sadaka kwa wahitaji. Hilo ni bora kwenu, kwa kuwa lina thawabu, na lenye kusafisha zaidi nyoyo zenu na madhambi. Basi mkitopata cha kutoa sadaka hamna makosa juu yenu. Kwani Mwenyezi Mungu, kwa hakika, ni Mwingi wa msamaha kwa waja Wake Waumini, ni Mwenye huruma kwao. info
التفاسير:

external-link copy
13 : 58

ءَأَشۡفَقۡتُمۡ أَن تُقَدِّمُواْ بَيۡنَ يَدَيۡ نَجۡوَىٰكُمۡ صَدَقَٰتٖۚ فَإِذۡ لَمۡ تَفۡعَلُواْ وَتَابَ ٱللَّهُ عَلَيۡكُمۡ فَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَ وَأَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥۚ وَٱللَّهُ خَبِيرُۢ بِمَا تَعۡمَلُونَ

Je, mmeogopa kuwa mtafukarika mkitanguliza sadaka kabla ya kunong’ona na Mtume wa Mwenyezi Mungu? Basi msipofanya hilo mliloamrishwa, na Mwenyezi Mungu Amewasamehe na Amewaruhusu msilifanye hilo, basi simameni imara na muendelee kusimamisha Swala, kutoa Zaka na kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake katika kila lile mliloamrishwa. Na Mwenyezi Mungu ni Mtambuzi wa Matendo yenu na ni Mwenye kuwalipa kwayo. info
التفاسير:

external-link copy
14 : 58

۞ أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ تَوَلَّوۡاْ قَوۡمًا غَضِبَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِم مَّا هُم مِّنكُمۡ وَلَا مِنۡهُمۡ وَيَحۡلِفُونَ عَلَى ٱلۡكَذِبِ وَهُمۡ يَعۡلَمُونَ

Je, huwaoni wanafiki waliowafanya Mayahudi ni marafiki na wakawategemea? Na wanafiki kihakika si miongoni mwa Waislamu wala mayahudi, na wanaapa urongo kuwa wao ni Waislamu na kuwa wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na hali wanajua kuwa wao ni warongo kwa kile walichokiapia. info
التفاسير:

external-link copy
15 : 58

أَعَدَّ ٱللَّهُ لَهُمۡ عَذَابٗا شَدِيدًاۖ إِنَّهُمۡ سَآءَ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Mwenyezi Mungu Amewatayarishia hawa wanafiki adhabu iliyofikia upeo wa ukali na uchungu. Hakika wao ni mabaya sana yale waliokuwa wakiyafanya ya unafiki na uapaji mayamini ya urongo. info
التفاسير:

external-link copy
16 : 58

ٱتَّخَذُوٓاْ أَيۡمَٰنَهُمۡ جُنَّةٗ فَصَدُّواْ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ فَلَهُمۡ عَذَابٞ مُّهِينٞ

Wanafiki wameyafanya yale mayamini yao ya urongo ni kinga yao wasipate kuuawa kwa ukafiri wao na kuwazuia Waislamu wasiwapige vita na kuchukua mali yao. Na kwa ajili hiyo wanajizuia wao na kuwazuia wengine njia ya Mwenyezi Mungu, nayo ni Uislamu. Basi watapata adhabu yenye kudhalilisha Motoni kwa kufanya kiburi kwao kwa kujiepusha na kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na kwa kuzuia kwao njia Yake isifuatwe. info
التفاسير:

external-link copy
17 : 58

لَّن تُغۡنِيَ عَنۡهُمۡ أَمۡوَٰلُهُمۡ وَلَآ أَوۡلَٰدُهُم مِّنَ ٱللَّهِ شَيۡـًٔاۚ أُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ

Hayatawakinga wanafiki hawa mali yao wala watoto wao kitu chochote na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Hao ni watu wa Motoni, watauingia na wasalie humo milele, hawatatoka humo kabisa. Malipo haya yanamkusanya kila anayeiwekea kizuizi Dini ya Mwenyezi Mungu kwa maneno yake au vitendo vyake. info
التفاسير:

external-link copy
18 : 58

يَوۡمَ يَبۡعَثُهُمُ ٱللَّهُ جَمِيعٗا فَيَحۡلِفُونَ لَهُۥ كَمَا يَحۡلِفُونَ لَكُمۡ وَيَحۡسَبُونَ أَنَّهُمۡ عَلَىٰ شَيۡءٍۚ أَلَآ إِنَّهُمۡ هُمُ ٱلۡكَٰذِبُونَ

Siku ya Kiyama, Mwenyezi Mungu Atawafufua wanafiki wote kutoka makaburini mwao wakiwa hai, na hapo wamuapie Yeye kuwa wao walikuwa Waumini kama walivyokuwa wakiwaapia nyinyi, enyi Waumini, duniani. Na watadhani kuwa hilo litawanufaisha kwa Mwenyezi Mungu kama lilivyokuwa linawanufaisha ulimwenguni kwa Waislamu. Basi jua na utanabahi kuwa wao ndio waliofikia upeo katika urongo ambao hawakuufikia wasiokuwa wao. info
التفاسير:

external-link copy
19 : 58

ٱسۡتَحۡوَذَ عَلَيۡهِمُ ٱلشَّيۡطَٰنُ فَأَنسَىٰهُمۡ ذِكۡرَ ٱللَّهِۚ أُوْلَٰٓئِكَ حِزۡبُ ٱلشَّيۡطَٰنِۚ أَلَآ إِنَّ حِزۡبَ ٱلشَّيۡطَٰنِ هُمُ ٱلۡخَٰسِرُونَ

Hao Shetani aliwaghilibu na akawatawala mpaka wakaacha amri za Mwenyezi Mungu na kufanya matendo ya utiifu Kwake. Hao ni kundi la Shetani na wafuasi wake. Jua utanabahi kwamba watu wa kundi la Shetani ndio wenye kupata hasara duniani na Akhera. info
التفاسير:

external-link copy
20 : 58

إِنَّ ٱلَّذِينَ يُحَآدُّونَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥٓ أُوْلَٰٓئِكَ فِي ٱلۡأَذَلِّينَ

Hakika wale wanaoenda kinyume na amri ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, hao ni miongoni mwa wadhalilifu walioshindwa na kufanywa wanyonge duniani na Akhera. info
التفاسير:

external-link copy
21 : 58

كَتَبَ ٱللَّهُ لَأَغۡلِبَنَّ أَنَا۠ وَرُسُلِيٓۚ إِنَّ ٱللَّهَ قَوِيٌّ عَزِيزٞ

Ameandika Mwenyezi Mungu kwenye Ubao Uliohifadhiwa na Amepitisha kuwa ushindi ni Wake Yeye, Kitabu Chake, Mitume Wake na waja Wake Waumini. Hakika mwenyezi Mungu, kutakasika ni Kwake, ni Mwenye nguvu, hakuna kitu kinachomuelemea, ni Mwenye ushindi juu ya viumbe Vyake. info
التفاسير: