قۇرئان كەرىم مەنىلىرىنىڭ تەرجىمىسى - قۇرئان كەرىمنىڭ ساۋاھىلچە تەرجىمىسىنى ئابدۇللا مۇھەممەد ۋە ناسىر خەمىيس تەرجىمە قىلغان.

Al-Waqi'ah

external-link copy
1 : 56

إِذَا وَقَعَتِ ٱلۡوَاقِعَةُ

Kitakaposimama Kiyama. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 56

لَيۡسَ لِوَقۡعَتِهَا كَاذِبَةٌ

Hakutakuwa na yoyote mwenye kukanusha kusimama kwake. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 56

خَافِضَةٞ رَّافِعَةٌ

Ni chenye kuwainamisha chini maadui wa Mwenyezi Mungu ndani ya Moto na ni chenye kuwainua juu Peponi wale wenye kumtegemea. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 56

إِذَا رُجَّتِ ٱلۡأَرۡضُ رَجّٗا

Itakapotikiswa ardhi mtikiso wa nguvu. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 56

وَبُسَّتِ ٱلۡجِبَالُ بَسّٗا

Na yakamumunyuliwa majabali mmumunyuo wa kina. info
التفاسير:

external-link copy
6 : 56

فَكَانَتۡ هَبَآءٗ مُّنۢبَثّٗا

Yakawa vumbi lenye kuruka angani lililosukumwa na upepo. info
التفاسير:

external-link copy
7 : 56

وَكُنتُمۡ أَزۡوَٰجٗا ثَلَٰثَةٗ

Na mkawa, enyi viumbe, makundi matatu: info
التفاسير:

external-link copy
8 : 56

فَأَصۡحَٰبُ ٱلۡمَيۡمَنَةِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَيۡمَنَةِ

Kundi la watu wa upande wa kulia, wenye daraja kubwa. Ni kikubwa kilioje cheo chao! info
التفاسير:

external-link copy
9 : 56

وَأَصۡحَٰبُ ٱلۡمَشۡـَٔمَةِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَشۡـَٔمَةِ

Kuna na kundi la watu wa upande wa kushoto, wenye daraja duni. Ni mbaya iliyoje hali yao! info
التفاسير:

external-link copy
10 : 56

وَٱلسَّٰبِقُونَ ٱلسَّٰبِقُونَ

Na wale waliotangulia mbele kwenye kheri duniani ndio wenye kutangulia mbele kwenye daraja za juu huko Akhera. info
التفاسير:

external-link copy
11 : 56

أُوْلَٰٓئِكَ ٱلۡمُقَرَّبُونَ

Wao ndio walioletwa karibu kwa Mwenyezi Mungu, info
التفاسير:

external-link copy
12 : 56

فِي جَنَّٰتِ ٱلنَّعِيمِ

Mola wao Atawatia kwenye mabustani ya Pepo ya starehe. info
التفاسير:

external-link copy
13 : 56

ثُلَّةٞ مِّنَ ٱلۡأَوَّلِينَ

Watayaingia watu wengi watu wa mwanzo wa ummah huu, na ummah wengineo wasiokuwa wao, info
التفاسير:

external-link copy
14 : 56

وَقَلِيلٞ مِّنَ ٱلۡأٓخِرِينَ

na wachache miongoni mwa watu mwisho wa ummah huu, info
التفاسير:

external-link copy
15 : 56

عَلَىٰ سُرُرٖ مَّوۡضُونَةٖ

wakiwa juu ya vitanda vilivyofumwa kwa dhahabu, info
التفاسير:

external-link copy
16 : 56

مُّتَّكِـِٔينَ عَلَيۡهَا مُتَقَٰبِلِينَ

na wakiwa katika hali ya kuvitegemea na huku wanaelekeana na kukutana. info
التفاسير:

external-link copy
17 : 56

يَطُوفُ عَلَيۡهِمۡ وِلۡدَٰنٞ مُّخَلَّدُونَ

Wanawazunguka wao kuwatumikia watumishi vijana wasiozeeka wala kufa, info
التفاسير:

external-link copy
18 : 56

بِأَكۡوَابٖ وَأَبَارِيقَ وَكَأۡسٖ مِّن مَّعِينٖ

wakiwa na vikombe, mabirika na gilasi kutoka kwenye chemchemi ya pombe yenye kupita ndani ya Pepo, info
التفاسير:

external-link copy
19 : 56

لَّا يُصَدَّعُونَ عَنۡهَا وَلَا يُنزِفُونَ

na hawaumwi na vichwa kutokana nayo wala hawarukwi na akili. info
التفاسير:

external-link copy
20 : 56

وَفَٰكِهَةٖ مِّمَّا يَتَخَيَّرُونَ

Na watawazunguka wao watumishi vijana na kila kitu wanachokichagua miongoni mwa matunda, info
التفاسير:

external-link copy
21 : 56

وَلَحۡمِ طَيۡرٖ مِّمَّا يَشۡتَهُونَ

nyama ya ndege ambayo nafsi zao inavutika nayo. info
التفاسير:

external-link copy
22 : 56

وَحُورٌ عِينٞ

Na watakuwa na wanawake wenye macho makubwa kama kwamba wao, info
التفاسير:

external-link copy
23 : 56

كَأَمۡثَٰلِ ٱللُّؤۡلُوِٕ ٱلۡمَكۡنُونِ

kwa usafi wao na uzuri wao, ni lulu iliyohifadhiwa ndani ya mashaza yake, info
التفاسير:

external-link copy
24 : 56

جَزَآءَۢ بِمَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

hali hayo yakiwa ni malipo yao kwa yale waliokuwa wakiyafanya duniani. info
التفاسير:

external-link copy
25 : 56

لَا يَسۡمَعُونَ فِيهَا لَغۡوٗا وَلَا تَأۡثِيمًا

Hawatasikia humo Peponi ubatilifu wala yale ya kuwatia madhambini kuyasikia, info
التفاسير:

external-link copy
26 : 56

إِلَّا قِيلٗا سَلَٰمٗا سَلَٰمٗا

isipokuwa maneno yasiyokuwa na kasoro hizi na kusalimiana wao kwa wao. info
التفاسير:

external-link copy
27 : 56

وَأَصۡحَٰبُ ٱلۡيَمِينِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلۡيَمِينِ

Na watu wa upande wa kulia, info
التفاسير:

external-link copy
28 : 56

فِي سِدۡرٖ مَّخۡضُودٖ

ni kikubwa kilioje cheo chao na malipo yao! info
التفاسير:

external-link copy
29 : 56

وَطَلۡحٖ مَّنضُودٖ

Watakuwa kwenye mikunazi isiyo na miba, na ndizi zilizopandana na kupangika, info
التفاسير:

external-link copy
30 : 56

وَظِلّٖ مَّمۡدُودٖ

kila ndizi juu ya nyingine, na vivuli vya daima visivyoondoka, info
التفاسير:

external-link copy
31 : 56

وَمَآءٖ مَّسۡكُوبٖ

na maji yanayotembea yasiyokatika, info
التفاسير:

external-link copy
32 : 56

وَفَٰكِهَةٖ كَثِيرَةٖ

na matunda mengi info
التفاسير:

external-link copy
33 : 56

لَّا مَقۡطُوعَةٖ وَلَا مَمۡنُوعَةٖ

yasiyomalizika wala kuwaishia wala hakuna kizuizi chochote kinachowazuia wao kuyafikia, info
التفاسير:

external-link copy
34 : 56

وَفُرُشٖ مَّرۡفُوعَةٍ

na matandiko yaliyoinuliwa juu ya vitanda. info
التفاسير:

external-link copy
35 : 56

إِنَّآ أَنشَأۡنَٰهُنَّ إِنشَآءٗ

Sisi tumewaumba wanawake wa watu wa Peponi umbile ambalo silo lile umbile lililokuwa duniani, umbile lililokamilika lisilokubali kutoweka, info
التفاسير:

external-link copy
36 : 56

فَجَعَلۡنَٰهُنَّ أَبۡكَارًا

na tumewafanya ni wanawali wenye kujipendekeza kwa waume zao, info
التفاسير:

external-link copy
37 : 56

عُرُبًا أَتۡرَابٗا

hali ya kuwa ni marika na wao kimiaka. info
التفاسير:

external-link copy
38 : 56

لِّأَصۡحَٰبِ ٱلۡيَمِينِ

Tumewaumbia wanawake hao watu wa upande wa kulia. info
التفاسير:

external-link copy
39 : 56

ثُلَّةٞ مِّنَ ٱلۡأَوَّلِينَ

Nao ni kundi la watu wengi wa mwanzo info
التفاسير:

external-link copy
40 : 56

وَثُلَّةٞ مِّنَ ٱلۡأٓخِرِينَ

na kundi la watu wengi wa mwisho. info
التفاسير:

external-link copy
41 : 56

وَأَصۡحَٰبُ ٱلشِّمَالِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلشِّمَالِ

Na watu wa upande wa kushoto, ni mbaya iliyoje hali yao na malipo yao! info
التفاسير:

external-link copy
42 : 56

فِي سَمُومٖ وَحَمِيمٖ

Watakuwa kwenye upepo ulio moto utokanao na joto la Moto wa Jahanamu utakaozuia pumzi zao, na maji moto yanayochemka, info
التفاسير:

external-link copy
43 : 56

وَظِلّٖ مِّن يَحۡمُومٖ

na kivuli cha moshi mweusi sana, info
التفاسير:

external-link copy
44 : 56

لَّا بَارِدٖ وَلَا كَرِيمٍ

usio na mashukio baridi wala mandhari mazuri. info
التفاسير:

external-link copy
45 : 56

إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَبۡلَ ذَٰلِكَ مُتۡرَفِينَ

Kwani wao walikuwa duniani wakijistarehesha kwa vitu vya haramu wakijiepusha na yale ambayo Mitume walikuja nayo. info
التفاسير:

external-link copy
46 : 56

وَكَانُواْ يُصِرُّونَ عَلَى ٱلۡحِنثِ ٱلۡعَظِيمِ

Na walikuwa wamesimama wima katika kumkanusha Mwenyezi Mungu na kumshirikisha na kumuasi, na hawakuwa na nia ya kutubia kwa hayo. info
التفاسير:

external-link copy
47 : 56

وَكَانُواْ يَقُولُونَ أَئِذَا مِتۡنَا وَكُنَّا تُرَابٗا وَعِظَٰمًا أَءِنَّا لَمَبۡعُوثُونَ

Na walikuwa wakisema hali ya kukanusha Ufufuzi, «Je hivi sisi tutafufuliwa tutakapokufa na tukawa mchanga na mifupa iliyochakaa?» Maneno yao hayo yanaonesha kuwa wao walikuwa wakiliona jambo hili la kufufuliwa kuwa liko mbali na ukweli na wakilikanusha. info
التفاسير:

external-link copy
48 : 56

أَوَءَابَآؤُنَا ٱلۡأَوَّلُونَ

«Je tutafufuliwa sisi na hali baba zetu waliotangulia wamekuwa mchanga uliotapakaa kwenye ardhi?» info
التفاسير:

external-link copy
49 : 56

قُلۡ إِنَّ ٱلۡأَوَّلِينَ وَٱلۡأٓخِرِينَ

Sema uwaambie, «Hakika wa mwanzo na wa mwisho miongoni mwa binadamu info
التفاسير:

external-link copy
50 : 56

لَمَجۡمُوعُونَ إِلَىٰ مِيقَٰتِ يَوۡمٖ مَّعۡلُومٖ

watakusanywa katika Siku iliyowekewa wakati maalumu, nayo ni Siku ya Kiyama. info
التفاسير:

external-link copy
51 : 56

ثُمَّ إِنَّكُمۡ أَيُّهَا ٱلضَّآلُّونَ ٱلۡمُكَذِّبُونَ

«Kisha nyinyi, enyi mliopotea njia ya uongofu mnaokanusha onyo la Mwenyezi Mungu na agizo Lake, info
التفاسير:

external-link copy
52 : 56

لَأٓكِلُونَ مِن شَجَرٖ مِّن زَقُّومٖ

ni wenye kula kutokana na mti wa zaqqūm, info
التفاسير:

external-link copy
53 : 56

فَمَالِـُٔونَ مِنۡهَا ٱلۡبُطُونَ

nao ni katika miti mibaya zaidi, na ni wenye kujaza matumbo yenu kutokana nao kwa sababu ya ukali wa njaa, info
التفاسير:

external-link copy
54 : 56

فَشَٰرِبُونَ عَلَيۡهِ مِنَ ٱلۡحَمِيمِ

na ni wenye kunywa juu yake maji yaliyo moto hadi ya mwisho, yasiyomaliza kiu. info
التفاسير:

external-link copy
55 : 56

فَشَٰرِبُونَ شُرۡبَ ٱلۡهِيمِ

Mtayanywa maji hayo kwa wingi kama vile ngamia wenye kiu wasioshiba maji kwa ugonjwa uliowapata.» info
التفاسير:

external-link copy
56 : 56

هَٰذَا نُزُلُهُمۡ يَوۡمَ ٱلدِّينِ

Adhabu hii watakayoipata ndiyo zawadi Aliyowaandalia Siku ya Kiyama. Katika haya kuna kuwalaumu na kuwacheza shere. info
التفاسير:

external-link copy
57 : 56

نَحۡنُ خَلَقۡنَٰكُمۡ فَلَوۡلَا تُصَدِّقُونَ

Sisi tumewaumba, enyi watu, na hamkuwa kitu chochote. Basi si msadiki kuwa kuna kufufuliwa? info
التفاسير:

external-link copy
58 : 56

أَفَرَءَيۡتُم مَّا تُمۡنُونَ

Mnayaonaje maji ya manii mnayoyatupa ndani ya vizazi vya wake zenu, info
التفاسير:

external-link copy
59 : 56

ءَأَنتُمۡ تَخۡلُقُونَهُۥٓ أَمۡ نَحۡنُ ٱلۡخَٰلِقُونَ

je nyinyi ndio mnaomuumba mwanadamu kutokana na hayo au ni sisi ndio wenye kuumba? info
التفاسير:

external-link copy
60 : 56

نَحۡنُ قَدَّرۡنَا بَيۡنَكُمُ ٱلۡمَوۡتَ وَمَا نَحۡنُ بِمَسۡبُوقِينَ

Sisi tumekadiria kifo kwenu, info
التفاسير:

external-link copy
61 : 56

عَلَىٰٓ أَن نُّبَدِّلَ أَمۡثَٰلَكُمۡ وَنُنشِئَكُمۡ فِي مَا لَا تَعۡلَمُونَ

na sisi si wenye kushindwa kubadilisha umbo lenu Siku ya Kiyama na kuwaumba kwa sifa na namna msizozijua. info
التفاسير:

external-link copy
62 : 56

وَلَقَدۡ عَلِمۡتُمُ ٱلنَّشۡأَةَ ٱلۡأُولَىٰ فَلَوۡلَا تَذَكَّرُونَ

Na hakika mlijua kuwa Mwenyezi Mungu Aliwaumba uumbaji wa kwanza na hamkuwa kitu chochote. Basi si mkumbuke uweza wa Mwenyezi Mungu wa kuwaumba mara nyingine? info
التفاسير:

external-link copy
63 : 56

أَفَرَءَيۡتُم مَّا تَحۡرُثُونَ

Mnazionaje mbegu mnazozipanda? info
التفاسير:

external-link copy
64 : 56

ءَأَنتُمۡ تَزۡرَعُونَهُۥٓ أَمۡ نَحۡنُ ٱلزَّٰرِعُونَ

Je ni nyinyi mnaoziotesha kutoka ardhini? Sisi ndio tuaozituliza na kuziotesha ardhini. info
التفاسير:

external-link copy
65 : 56

لَوۡ نَشَآءُ لَجَعَلۡنَٰهُ حُطَٰمٗا فَظَلۡتُمۡ تَفَكَّهُونَ

Lau tungalitaka tungaliifanya mimea inayotokana na mbegu hizo kuwa mapepe, haimkiniki kunufaika nayo kwa kula, info
التفاسير:

external-link copy
66 : 56

إِنَّا لَمُغۡرَمُونَ

mkawa mnaona ajabu kwa kilichoshukia mimea yenu na mnasema, «Sisi tumepata hasara na ni wenye kuungulika. info
التفاسير:

external-link copy
67 : 56

بَلۡ نَحۡنُ مَحۡرُومُونَ

Bali sisi tumekoseshwa riziki.» info
التفاسير:

external-link copy
68 : 56

أَفَرَءَيۡتُمُ ٱلۡمَآءَ ٱلَّذِي تَشۡرَبُونَ

Mnayaonaje maji mnayokunywa ili mhuike kwayo? info
التفاسير:

external-link copy
69 : 56

ءَأَنتُمۡ أَنزَلۡتُمُوهُ مِنَ ٱلۡمُزۡنِ أَمۡ نَحۡنُ ٱلۡمُنزِلُونَ

Je ni nyinyi mliyoyateremsha kutoka kwenye mawingu hadi kwenye kituo cha ardhi au ni sisi tuliyoyateremsha ili kuwarehemu nyinyi? info
التفاسير:

external-link copy
70 : 56

لَوۡ نَشَآءُ جَعَلۡنَٰهُ أُجَاجٗا فَلَوۡلَا تَشۡكُرُونَ

Lau tungalitaka tungaliyafanya maji haya yawe na chumvi sana, ikiwa haiwezekani kunufaika nayo kwa kunywa wala kwa mimea. Basi si mumshukuru Mola wenu kwa kuteremsha maji tamu kwa kuwanufaisha nyinyi. info
التفاسير:

external-link copy
71 : 56

أَفَرَءَيۡتُمُ ٱلنَّارَ ٱلَّتِي تُورُونَ

Mnaouonaje moto mnaouwasha? info
التفاسير:

external-link copy
72 : 56

ءَأَنتُمۡ أَنشَأۡتُمۡ شَجَرَتَهَآ أَمۡ نَحۡنُ ٱلۡمُنشِـُٔونَ

Je ni nyinyi mlioufanya mti wake, unaozalisha moto kwa kukwaruzwa, upatikane au ni sisi tulioufanya upatikane? info
التفاسير:

external-link copy
73 : 56

نَحۡنُ جَعَلۡنَٰهَا تَذۡكِرَةٗ وَمَتَٰعٗا لِّلۡمُقۡوِينَ

Sisi tumeufanya moto wenu mnaouwasha ni ukumbusho kwenu wa Moto wa Jahanamu na pia ni manufaa kwa wasafiri. info
التفاسير:

external-link copy
74 : 56

فَسَبِّحۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلۡعَظِيمِ

Basi mtakase Mola wako, ewe Nabii, Aliye mtukufu Mwenye ukamilifu wa majina na sifa, Mwingi wa wema na kheri. info
التفاسير:

external-link copy
75 : 56

۞ فَلَآ أُقۡسِمُ بِمَوَٰقِعِ ٱلنُّجُومِ

Mwenyezi Mungu Anaapa kwa mapomoko ya nyota nyakati za kuzama kwake mbinguni. info
التفاسير:

external-link copy
76 : 56

وَإِنَّهُۥ لَقَسَمٞ لَّوۡ تَعۡلَمُونَ عَظِيمٌ

Nacho ni kiapo kikubwa lau mnajua kadiri yake. info
التفاسير:

external-link copy
77 : 56

إِنَّهُۥ لَقُرۡءَانٞ كَرِيمٞ

Hakika hii Qur’ani iliyoteremshiwa Muhammad ni Qur’ani yenye manufaa makubwa, yenye kheri nyingi na yenye elimu tele, info
التفاسير:

external-link copy
78 : 56

فِي كِتَٰبٖ مَّكۡنُونٖ

iliyo ndani ya Kitabu kilichohifadhiwa, kilichofichwa na macho ya viumbe, nacho ni Kitabu ambacho kiko mikononi mwa Malaika. info
التفاسير:

external-link copy
79 : 56

لَّا يَمَسُّهُۥٓ إِلَّا ٱلۡمُطَهَّرُونَ

Hawaigusi Qur’ani isipokuwa malaika watukufu ambao Mwenyezi Mungu Amewasafisha na aibu na madhambi. Na pia hawaigusi isipokuwa watu waliojitohirisha na ushirikina na janaba na ukosefu wa udhu. info
التفاسير:

external-link copy
80 : 56

تَنزِيلٞ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Na hii Qur’ani tukufu imeteremshwa kutoka kwa Mola wa viumbe vyote, kwani hiyo ndiyo haki isiyo na shaka ndani yake. info
التفاسير:

external-link copy
81 : 56

أَفَبِهَٰذَا ٱلۡحَدِيثِ أَنتُم مُّدۡهِنُونَ

je hii Qur’ani, enyi washirikina, mnaikanusha? info
التفاسير:

external-link copy
82 : 56

وَتَجۡعَلُونَ رِزۡقَكُمۡ أَنَّكُمۡ تُكَذِّبُونَ

Na je mnaifanya shukrani yenu kwa neema za Mola wenu ni kuwa nyinyi mnazikanusha na kukufuru? Hapa pana makaripio kwa anayedharau amri za Qur’ani na kutojali mwito wake. info
التفاسير:

external-link copy
83 : 56

فَلَوۡلَآ إِذَا بَلَغَتِ ٱلۡحُلۡقُومَ

Basi je mnaweza pindi roho ya mmoja wenu inapofika kwenye koo katika uchungu wa kifo, info
التفاسير:

external-link copy
84 : 56

وَأَنتُمۡ حِينَئِذٖ تَنظُرُونَ

na hali nyinyi mmehudhuria mnamtazama, kuizuia roho yake ndani ya mwili wake? Hamtaweza hilo! info
التفاسير:

external-link copy
85 : 56

وَنَحۡنُ أَقۡرَبُ إِلَيۡهِ مِنكُمۡ وَلَٰكِن لَّا تُبۡصِرُونَ

Na sisi tuko karibu na yeye zaidi, kupitia Malaika wetu, kuliko nyinyi, lakini nyinyi hamuwaoni. info
التفاسير:

external-link copy
86 : 56

فَلَوۡلَآ إِن كُنتُمۡ غَيۡرَ مَدِينِينَ

Na je mnaweza, iwapo nyinyi si wenye kuhesabiwa wala kulipwa kwa matendo yenu, info
التفاسير:

external-link copy
87 : 56

تَرۡجِعُونَهَآ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

kuirudisha roho kwenye mwili, iwapo nyinyi ni wakweli? Hamtaweza kuirudisha. info
التفاسير:

external-link copy
88 : 56

فَأَمَّآ إِن كَانَ مِنَ ٱلۡمُقَرَّبِينَ

Basi iwapo yule anayekufa ni kati ya watu wa upande wa kulia, atapata rehema kunjufu na furaha, info
التفاسير:

external-link copy
89 : 56

فَرَوۡحٞ وَرَيۡحَانٞ وَجَنَّتُ نَعِيمٖ

wakati wa kufa kwake, na kila kinachoifurahisha nafsi yake, Na atapata Pepo ya starehe huko Akhera. info
التفاسير:

external-link copy
90 : 56

وَأَمَّآ إِن كَانَ مِنۡ أَصۡحَٰبِ ٱلۡيَمِينِ

Na iwapo yule anayekufa ni kati ya watu wa upande wa kulia, info
التفاسير:

external-link copy
91 : 56

فَسَلَٰمٞ لَّكَ مِنۡ أَصۡحَٰبِ ٱلۡيَمِينِ

ataambiwa, «Umesalimika na kuwa kwenye amani, kwa kuwa wewe ni miongoni mwa watu wa upande wa kulia.» info
التفاسير:

external-link copy
92 : 56

وَأَمَّآ إِن كَانَ مِنَ ٱلۡمُكَذِّبِينَ ٱلضَّآلِّينَ

Na iwapo yule anayekufa ni miongoni mwa wenye kukanusha kufufuliwa, waliopotoka na njia ya uongofu, info
التفاسير:

external-link copy
93 : 56

فَنُزُلٞ مِّنۡ حَمِيمٖ

basi atapata makaribisho ya kinywaji cha moto wa Jahanamu kilichochemshwa, kilicho na joto hadi ya mwisho, info
التفاسير:

external-link copy
94 : 56

وَتَصۡلِيَةُ جَحِيمٍ

na atachomwa na Moto na aungulike na adhabu yake kali. info
التفاسير:

external-link copy
95 : 56

إِنَّ هَٰذَا لَهُوَ حَقُّ ٱلۡيَقِينِ

Hakika habari hii tumezokuelezea, ewe Mtume, ni ukweli wa yakini usio na shaka. info
التفاسير:

external-link copy
96 : 56

فَسَبِّحۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلۡعَظِيمِ

Basi litakase jina la Mola wako Aliyetukuka na umtakase na yale ambayo madhalimu na wenye kukanusha wanayasema. Mwenyezi Mungu Yuko juu ya yale wanayoyasema ujuu mkubwa sana. info
التفاسير: