قۇرئان كەرىم مەنىلىرىنىڭ تەرجىمىسى - قۇرئان كەرىمنىڭ ساۋاھىلچە تەرجىمىسىنى ئابدۇللا مۇھەممەد ۋە ناسىر خەمىيس تەرجىمە قىلغان.

Ar-Rahman

external-link copy
1 : 55

ٱلرَّحۡمَٰنُ

mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema info
التفاسير:

external-link copy
2 : 55

عَلَّمَ ٱلۡقُرۡءَانَ

Amemfundisha binadamu Qur’ani kwa kurahisisha kuisoma, kuihifadhi na kuelewa maana yake. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 55

خَلَقَ ٱلۡإِنسَٰنَ

Amemuumba binadamu, info
التفاسير:

external-link copy
4 : 55

عَلَّمَهُ ٱلۡبَيَانَ

Amemfundisha ufasaha wa kujieleza ili kumtenganisha na wengine. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 55

ٱلشَّمۡسُ وَٱلۡقَمَرُ بِحُسۡبَانٖ

Jua na mwezi zinatembea kwa kufuatana, moja baada ya nyingine, kwa hesabu madhubuti isiyotafautiana wala kugongana. info
التفاسير:

external-link copy
6 : 55

وَٱلنَّجۡمُ وَٱلشَّجَرُ يَسۡجُدَانِ

Na nyota iliyo mbinguni na miti ya ardhini, vinamjua Mola wao, vinamsujudia na vinanyosha shingo zao kufuata vile ambavyo vimepangiwa vifuate vya maslahi ya waja Wake na manufaa yao. info
التفاسير:

external-link copy
7 : 55

وَٱلسَّمَآءَ رَفَعَهَا وَوَضَعَ ٱلۡمِيزَانَ

Na mbingu Ameiinua na kuifanya iwe juu ya ardhi, Na Ameweka kwenye ardhi uadilifu Aliouamrisha na kuulazimisha kwa waja Wake. info
التفاسير:

external-link copy
8 : 55

أَلَّا تَطۡغَوۡاْ فِي ٱلۡمِيزَانِ

Ili msipite mipaka na msimfanyie hiyana mnayempimia. info
التفاسير:

external-link copy
9 : 55

وَأَقِيمُواْ ٱلۡوَزۡنَ بِٱلۡقِسۡطِ وَلَا تُخۡسِرُواْ ٱلۡمِيزَانَ

Na simamisheni upimaji kwa usawa na msipunguze mizani mnapowapimia watu. info
التفاسير:

external-link copy
10 : 55

وَٱلۡأَرۡضَ وَضَعَهَا لِلۡأَنَامِ

Na ardhi Ameiweka na Ameitayarisha, ili viumbe vitulie juu yake. info
التفاسير:

external-link copy
11 : 55

فِيهَا فَٰكِهَةٞ وَٱلنَّخۡلُ ذَاتُ ٱلۡأَكۡمَامِ

Humo mna matunda na mitende yenye makarara ya matunda. Na humo kuna nafaka zenye maganda, vikiwa ni chakula chenu na wanyama wenu. info
التفاسير:

external-link copy
12 : 55

وَٱلۡحَبُّ ذُو ٱلۡعَصۡفِ وَٱلرَّيۡحَانُ

Na humo mna kila mmea wenye harufu nzuri. info
التفاسير:

external-link copy
13 : 55

فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ

Bas ni neema gani za Mola wenu, za kidini na za kidunia, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha? Na ni jawabu nzuri ilioje ya majini alipowasomea wao Nabii, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, sura hii, kila akipita kwenye aya hii walikuwa wakisema, «Hakuna chochote miongoni mwa neema zako, ewe Mola wetu, tunachokanusha. Sifa njema zote ni zako.» Na hivi ndivyo inavyotakiwa kwa mja anapoelezewa neema za Mwenyezi Mungu na mema Yake akubali na amshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema hizo. info
التفاسير:

external-link copy
14 : 55

خَلَقَ ٱلۡإِنسَٰنَ مِن صَلۡصَٰلٖ كَٱلۡفَخَّارِ

Amemuumba baba wa wanadamu, naye ni Ādam, kwa udongo mkavu kama vyungu. info
التفاسير:

external-link copy
15 : 55

وَخَلَقَ ٱلۡجَآنَّ مِن مَّارِجٖ مِّن نَّارٖ

Na Amemuumba Iblisi, naye ni katika majini, kwa mroromo wa moto uliochanganyika. info
التفاسير:

external-link copy
16 : 55

فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ

Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha? info
التفاسير:

external-link copy
17 : 55

رَبُّ ٱلۡمَشۡرِقَيۡنِ وَرَبُّ ٱلۡمَغۡرِبَيۡنِ

Mola wa pande mbili za Mashariki ya jua, katika kusi na kaskazi, na Mola wa pande mbili za Magharibi ya jua, katika kusi na kaskazi, kwani vyote viko chini ya uendeshaji Wake na ulezi Wake.. info
التفاسير:

external-link copy
18 : 55

فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ

Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha? info
التفاسير: