قۇرئان كەرىم مەنىلىرىنىڭ تەرجىمىسى - قۇرئان كەرىمنىڭ ساۋاھىلچە تەرجىمىسىنى ئابدۇللا مۇھەممەد ۋە ناسىر خەمىيس تەرجىمە قىلغان.

external-link copy
155 : 3

إِنَّ ٱلَّذِينَ تَوَلَّوۡاْ مِنكُمۡ يَوۡمَ ٱلۡتَقَى ٱلۡجَمۡعَانِ إِنَّمَا ٱسۡتَزَلَّهُمُ ٱلشَّيۡطَٰنُ بِبَعۡضِ مَا كَسَبُواْۖ وَلَقَدۡ عَفَا ٱللَّهُ عَنۡهُمۡۗ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ حَلِيمٞ

Hakika wale waliokimbia kati yenu, enyi Maswahaba wa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kwenye vita siku waliokutana Waumimini na washirikina katika vita vya Uhud, ni Shetani ndiye aliyewatosa kwenye dhambi hili kutokana na baadhi ya madhambi waliyoyafanya. Kwa kweli Mwenyezi Mungu Amewasamehe na hakuwaadhibu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa Msamaha kwa wenye madhambi wanaotubia, ni Mpole Asiyekuwa na haraka ya kuwatesa wenye kumuasi. info
التفاسير: