قۇرئان كەرىم مەنىلىرىنىڭ تەرجىمىسى - قۇرئان كەرىمنىڭ ساۋاھىلچە تەرجىمىسىنى ئابدۇللا مۇھەممەد ۋە ناسىر خەمىيس تەرجىمە قىلغان.

external-link copy
118 : 16

وَعَلَى ٱلَّذِينَ هَادُواْ حَرَّمۡنَا مَا قَصَصۡنَا عَلَيۡكَ مِن قَبۡلُۖ وَمَا ظَلَمۡنَٰهُمۡ وَلَٰكِن كَانُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ يَظۡلِمُونَ

Na Mayahudi tuliwaharamishia vile vitu tulivyokupa habari zake, ewe Mtume, kabla, navyo ni kila mnyama mwenye kucha na mafuta ya ng’ombe, mbuzi na kondoo, isipokuwa kile kilichobebwa na migongo yao au matumbo yao au kilichotangamana na mifupa. Na sisi hatukuwadhulumu wao , lakini wao walikuwa ni wenye kuzidhulumu nafsi zao kwa kukanusha na kufanya uadui, ndipo wakastahili kuharamishiwa kwa njia ya kutiwa adabu. info
التفاسير: