قۇرئان كەرىم مەنىلىرىنىڭ تەرجىمىسى - قۇرئان كەرىمنىڭ ساۋاھىلچە تەرجىمىسىنى ئابدۇللا مۇھەممەد ۋە ناسىر خەمىيس تەرجىمە قىلغان.

external-link copy
30 : 10

هُنَالِكَ تَبۡلُواْ كُلُّ نَفۡسٖ مَّآ أَسۡلَفَتۡۚ وَرُدُّوٓاْ إِلَى ٱللَّهِ مَوۡلَىٰهُمُ ٱلۡحَقِّۖ وَضَلَّ عَنۡهُم مَّا كَانُواْ يَفۡتَرُونَ

Katika kisimamo hiko cha kuhesabiwa, kila nafsi itazipekua na kuziona hali zake na matendo yake, na italipwa kulingana na hayo : yakiwa ni mema atalipwa mema na yakiwa ni maovu atalipwa maovu. Na wote watarejeshwa kwa Mwenyezi Mungu Aliye Muamuzi Muadilifu. Hapo watu wa Peponi watatiwa Peponi, na watu wa Motoni watatiwa Motoni, na vitawaondokea washirikina vile ambavyo walikua wakiviabudu badala ya Mwenyezi Mungu kwa kumzulia Yeye urongo. info
التفاسير: