قۇرئان كەرىم مەنىلىرىنىڭ تەرجىمىسى - قۇرئان كەرىمنىڭ ساۋاھىلچە تەرجىمىسىنى ئابدۇللا مۇھەممەد ۋە ناسىر خەمىيس تەرجىمە قىلغان.

بەت نومۇرى:close

external-link copy
34 : 10

قُلۡ هَلۡ مِن شُرَكَآئِكُم مَّن يَبۡدَؤُاْ ٱلۡخَلۡقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥۚ قُلِ ٱللَّهُ يَبۡدَؤُاْ ٱلۡخَلۡقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥۖ فَأَنَّىٰ تُؤۡفَكُونَ

Sema, ewe Mtume, kuwaambia wao, «Je, kuna yoyote, miongoni mwa waungu wenu na waabudiwa wenu, mwenye kuanzisha kuumba chochote kisicho na asili (ya mfano uliotangulia) kisha akifanye kitoweke baada ya kukianzisha, kisha akirudishe kama namna kilivyokuwa kabla hajakifanya kitoweke?» Kwa hakika, wao hawawezi kufanya madai hayo. Sema, ewe Mtume, «Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Ndiye Anayeanzisha kuumba kisha Akakifanya kitoweke kile Alichokiumba, kisha Akakirudisha. Basi ni vipi nyinyi mnajiepusha na njia ya haki na kufuata ubatilifu, nao ni kumuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu?» info
التفاسير:

external-link copy
35 : 10

قُلۡ هَلۡ مِن شُرَكَآئِكُم مَّن يَهۡدِيٓ إِلَى ٱلۡحَقِّۚ قُلِ ٱللَّهُ يَهۡدِي لِلۡحَقِّۗ أَفَمَن يَهۡدِيٓ إِلَى ٱلۡحَقِّ أَحَقُّ أَن يُتَّبَعَ أَمَّن لَّا يَهِدِّيٓ إِلَّآ أَن يُهۡدَىٰۖ فَمَا لَكُمۡ كَيۡفَ تَحۡكُمُونَ

Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina, «Je, kuna yoyote, miongoni mwa washirika wenu, mwenye kuongoza kwenye njia iliyolingana sawa?» Hakika wao hawawezi hilo. Waambie, «Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Anamuongoza aliyepotea njia ya uongofu na kumuelekeza kwenye haki. Basi ni yupi anayefaa zaidi kufuatwa: ni yule anayeongoza, peke yake, kwenye njia ya haki au ni yule ambaye haongoki, kwa kutojua kwake na kwa upotevu wake, nao ndio hao washirikina wenu ambao hawaongozi wala hawaongoki mpaka waongozwe? Basi muna nini nyinyi, vipi mnamsawazisha Mwenyezi Mungu na viumbe vyake?» Huu ni uamuzi uliotanguka. info
التفاسير:

external-link copy
36 : 10

وَمَا يَتَّبِعُ أَكۡثَرُهُمۡ إِلَّا ظَنًّاۚ إِنَّ ٱلظَّنَّ لَا يُغۡنِي مِنَ ٱلۡحَقِّ شَيۡـًٔاۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمُۢ بِمَا يَفۡعَلُونَ

Na wengi wa washirikina hawa hawafuati, katika kuwafanya masanamu ni waungu na kuitakidi kwao kwamba hao masanamu wanawaleta karibu na Mwenyezi Mungu, isipokuwa urongo na dhana, nazo hazifai kitu mbele ya ukweli. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa wanayoyafanya washirikina hawa ya ukafiri na kukanusha. info
التفاسير:

external-link copy
37 : 10

وَمَا كَانَ هَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانُ أَن يُفۡتَرَىٰ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلَٰكِن تَصۡدِيقَ ٱلَّذِي بَيۡنَ يَدَيۡهِ وَتَفۡصِيلَ ٱلۡكِتَٰبِ لَا رَيۡبَ فِيهِ مِن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Haikuwa ni yenye kumkinika kwa yoyote kuja nayo Qur’ani hii kutoka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, sababu ni kwamba hakuna yoyote awezae kufanya hilo miongoni mwa viumbe. Lakini Mwenyezi Mungu Aliiteremsha kusadikisha vitabu alivyowateremshia Manabii Wake, kwa kuwa dini ya Mwenyezi Mungu ni moja. Na katika hii Qur’ani kuna maelezo na ufafanuzi wa sheria ya Mwenyezi Mungu Aliyowaekea ummah wa Muhammad. Hapana shaka kwamba hii Qur’ani ni wahyi unaotoka kwa Mola wa viumbe wote. info
التفاسير:

external-link copy
38 : 10

أَمۡ يَقُولُونَ ٱفۡتَرَىٰهُۖ قُلۡ فَأۡتُواْ بِسُورَةٖ مِّثۡلِهِۦ وَٱدۡعُواْ مَنِ ٱسۡتَطَعۡتُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Au kwani wao wanasema kwamba Muhammad ameizua hii Qur’ani yeye mwenyewe? Wao wanajua kwamba yeye ni mwanadamu kama wao. Waambie, «Basi leteni sura moja inayofanana na hii Qur’ani katika mpango wake na uongozi wake, na takeni usaidizi wa kufanya hilo kwa mnayemuweza, badala ya Mwenyezi Mungu, miongoni mwa majini na binadamu, iwapo nyinyi ni wakweli katika madai yenu.» info
التفاسير:

external-link copy
39 : 10

بَلۡ كَذَّبُواْ بِمَا لَمۡ يُحِيطُواْ بِعِلۡمِهِۦ وَلَمَّا يَأۡتِهِمۡ تَأۡوِيلُهُۥۚ كَذَٰلِكَ كَذَّبَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۖ فَٱنظُرۡ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلظَّٰلِمِينَ

Bali wao walifanya haraka kuikanusha Qur’ani mwanzo walipoisikia, kabla hawajazizingatia aya zake, na wakakikanusha kitu ambacho wao hawana ujuzi nacho, miongoni mwa habari ya Ufufuzi, Malipo, Pepo, Moto na vinginevyo, na bado haujawajia wao uhakika wa yale waliyoahidiwa katika Kitabu. Na kama walivyokanusha washirikina mambo Aliyowaonya nayo Mwenyezi Mungu, ndivyo walivyokanusha watu waliopita kabla yao. Basi tazama, ewe Mtume, ulikuwaje mwisho wa madhalimu? Baadhi yao Mwenyezi Mungu Aliwaangamiza kwa kuwadidimiza ardhini, wengine kwa kuwazamisha majini na wengine kwa kuwapa mateso mengineyo. info
التفاسير:

external-link copy
40 : 10

وَمِنۡهُم مَّن يُؤۡمِنُ بِهِۦ وَمِنۡهُم مَّن لَّا يُؤۡمِنُ بِهِۦۚ وَرَبُّكَ أَعۡلَمُ بِٱلۡمُفۡسِدِينَ

Na miongoni mwa watu wako, ewe Mtume, kuna anayeiamini Qur’ani na miongoni mwao kuna asiyeiamini mpaka afe kwenye msimamo huo na afufuliwe juu yake. Na Mola wako ni Anawajua zaidi hao waharibifu ambao hawaiamini kwa njia ya udhalimu, ushindani na uharibifu, na Atawalipa juu ya uharibifu wao kwa adhabu iliyo kali zaidi. info
التفاسير:

external-link copy
41 : 10

وَإِن كَذَّبُوكَ فَقُل لِّي عَمَلِي وَلَكُمۡ عَمَلُكُمۡۖ أَنتُم بَرِيٓـُٔونَ مِمَّآ أَعۡمَلُ وَأَنَا۠ بَرِيٓءٞ مِّمَّا تَعۡمَلُونَ

Na wakikukanusha, ewe Mtume, washirikina hawa waambie, «Mimi nina Dini yangu na matendo yangu, na nyinyi muna dini yenu na matendo yenu; nyinyi hamtaadhibiwa kwa matendo yangu, na mimi sitaadhibiwa kwa matendo yenu.» info
التفاسير:

external-link copy
42 : 10

وَمِنۡهُم مَّن يَسۡتَمِعُونَ إِلَيۡكَۚ أَفَأَنتَ تُسۡمِعُ ٱلصُّمَّ وَلَوۡ كَانُواْ لَا يَعۡقِلُونَ

Na miongoni mwa makafiri kuna wanaosikia maneno yako ya kweli na usomaji wako Qur’ani, lakini wao hawaongoki. Je, kwani wewe unaweza kuwasikizisha viziwi? Vilevile, huwezi kuwaongoa hawa isipokuwa Mwenyezi Mungu Atake kuwaongoa, kwa kuwa wao ni viziwi, hawaisikii haki na hawaielewi. info
التفاسير: