Kur'an-ı Kerim meal tercümesi - Savahili Dili Tercüme - Ali Muhsin Al-Barvani

Ash-Sharh

external-link copy
1 : 94

أَلَمۡ نَشۡرَحۡ لَكَ صَدۡرَكَ

Hatukukunjulia kifua chako? info

Hakika tumekukunjulia kifua chako kwa kuwa tulitia ndani yake Uwongofu na Imani.

التفاسير:

external-link copy
2 : 94

وَوَضَعۡنَا عَنكَ وِزۡرَكَ

Na tukakuondolea mzigo wako! info

Na tumekupunguzia mizigo iliyo kuwa mizito juu ya mgongo wako, kwa kukuunga mkono na kukusahilishia mambo yako,

التفاسير:

external-link copy
3 : 94

ٱلَّذِيٓ أَنقَضَ ظَهۡرَكَ

Ulio vunja mgongo wako? info

Ambayo yalikuwa ni mazito juu ya mgongo wako.

التفاسير:

external-link copy
4 : 94

وَرَفَعۡنَا لَكَ ذِكۡرَكَ

Na tukakunyanyulia utajo wako? info

Na tumelitukuza jina lako, tukalifanya linatajwa na ulimi wa kila Muumini pamoja na jina letu.

التفاسير:

external-link copy
5 : 94

فَإِنَّ مَعَ ٱلۡعُسۡرِ يُسۡرًا

Basi kwa hakika pamoja na uzito upo wepesi! info

Hizo ni baadhi ya neema zetu juu yako. Basi kuwa na yakini na uweza wa Mwenyezi Mtukufu, kwani pamoja na uzito upo wepesi mwingi unao kuja nao.

التفاسير:

external-link copy
6 : 94

إِنَّ مَعَ ٱلۡعُسۡرِ يُسۡرٗا

Hakika pamoja na uzito upo wepesi. info

Hakika pamoja na uzito (wakati huo huo ijapo kuwa wewe hujui), upo wepesi mwingi vile vile.

التفاسير:

external-link copy
7 : 94

فَإِذَا فَرَغۡتَ فَٱنصَبۡ

Na ukipata faragha, fanya juhudi. info

Basi ukipata nafasi katika kazi ya kuwalingania watu, na mambo yaliyo khusiana na Jihadi, endelea na jitihada ya ibada na jishughulishe nafsi yako katika hayo.

التفاسير:

external-link copy
8 : 94

وَإِلَىٰ رَبِّكَ فَٱرۡغَب

Na Mola wako Mlezi ndio mshughulikie. info

Kwa Mola wako Mlezi tu ndio uelekee kwa kumwomba na kumhitajia.

التفاسير: