Sema: Nambieni, ikiwa Mwenyezi Mungu akinifisha mimi na Waumini walio pamoja nami, kama mnavyo tamani yawe, au akaturehemu akaakhirisha ajali yetu, na akatusamehe asituadhibu, maana itakuwa katuokoa katika hali zote mbili, basi nani atakaye wakinga makafiri na adhabu chungu wanayo istahiki kuipata kwa sababu ya ukafiri wao, na kudanganyika kwao na miungu yao?