Kur'an-ı Kerim meal tercümesi - Savahili Dili Tercüme - Ali Muhsin Al-Barvani

An-Najm

external-link copy
1 : 53

وَٱلنَّجۡمِ إِذَا هَوَىٰ

Naapa kwa nyota inapo tua! info

Ninaapa kwa nyota inapo tua kwa kuchwa, ya kwamba Muhammad hakuiacha Njia iliyo sawa ya kufuata Haki, na wala hakupata kuitakidi upotovu.

التفاسير:

external-link copy
2 : 53

مَا ضَلَّ صَاحِبُكُمۡ وَمَا غَوَىٰ

Mwenzenu huyu hakupotea, wala hakukosea. info

ya kwamba Muhammad hakuiacha Njia iliyo sawa ya kufuata Haki, na wala hakupata kuitakidi upotovu.

التفاسير:

external-link copy
3 : 53

وَمَا يَنطِقُ عَنِ ٱلۡهَوَىٰٓ

Wala hatamki kwa matamanio. info

Wala halitoki katika anayo yatamka ya Qur'ani kwa mapendo ya nafsi yake.

التفاسير:

external-link copy
4 : 53

إِنۡ هُوَ إِلَّا وَحۡيٞ يُوحَىٰ

Hayakuwa haya ila ni ufunuo ulio funuliwa; . info

Hii Qur'ani anayo itamka si chochote ila ni Wahyi (Ufunuo) ulio toka kwa Mwenyezi Mungu anamfunulia yeye.

التفاسير:

external-link copy
5 : 53

عَلَّمَهُۥ شَدِيدُ ٱلۡقُوَىٰ

Amemfundisha aliye mwingi wa nguvu! info

Aliye mfundisha ufunuo huu ni mwenye nguvu nyingi.

التفاسير:

external-link copy
6 : 53

ذُو مِرَّةٖ فَٱسۡتَوَىٰ

Mwenye kutua, akatulia! info

Ambaye ametua akili zake na maoni yake, akasimama sawa sawa katika sura yake;

التفاسير:

external-link copy
7 : 53

وَهُوَ بِٱلۡأُفُقِ ٱلۡأَعۡلَىٰ

Naye yuko juu kabisa upeo wa macho. info

Naye yuko upande wa juu katika mbingu upeo wa macho wa mwenye kuangalia.

التفاسير:

external-link copy
8 : 53

ثُمَّ دَنَا فَتَدَلَّىٰ

Kisha akakaribia na akateremka. info

Kisha Jibrili alimkaribia, na akazidi kukaribia,

التفاسير:

external-link copy
9 : 53

فَكَانَ قَابَ قَوۡسَيۡنِ أَوۡ أَدۡنَىٰ

Akawa ni kama baina ya mipinde miwili, au karibu zaidi. info

hata akawa ukaribu wake ni kiasi ya mipinde miwili, bali karibu kuliko hivyo.

التفاسير:

external-link copy
10 : 53

فَأَوۡحَىٰٓ إِلَىٰ عَبۡدِهِۦ مَآ أَوۡحَىٰ

Akamfunulia mja wake (Mwenyezi Mungu) alicho mfunulia. info

Jibrili akamfunulia mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, alicho mfunulia, nao ufunuo huo ni jambo lenye shani kubwa na athari ya mbali kabisa.

التفاسير:

external-link copy
11 : 53

مَا كَذَبَ ٱلۡفُؤَادُ مَا رَأَىٰٓ

Moyo haukusema uwongo uliyo yaona. info

Moyo wa Muhammad haukukanya yale macho yake yaliyo yaona.

التفاسير:

external-link copy
12 : 53

أَفَتُمَٰرُونَهُۥ عَلَىٰ مَا يَرَىٰ

Je! Mnabishana naye kwa aliyo yaona? info

Hivyo nyinyi mnamkadhibisha Mtume wa Mwenyezi Mungu na mnabishana naye kwa aliyo yaona kwa macho yake?

التفاسير:

external-link copy
13 : 53

وَلَقَدۡ رَءَاهُ نَزۡلَةً أُخۡرَىٰ

Na akamwona mara nyingine, info

Na bila ya shaka Muhammad alimwona Jibrili kwa sura yake mara nyengine,

التفاسير:

external-link copy
14 : 53

عِندَ سِدۡرَةِ ٱلۡمُنتَهَىٰ

Penye Mkunazi wa mwisho. info

Katika pahala pasipo juulikana ila na Mwenyezi Mungu tu, ambapo amepaita Sidratul muntahaa, "Mkunazi wa Mwisho".

التفاسير:

external-link copy
15 : 53

عِندَهَا جَنَّةُ ٱلۡمَأۡوَىٰٓ

Karibu yake ndiyo ipo Bustani inayo kaliwa. info

Na akasimulia kuwa hapo ndio ipo Jannatul Ma-awa, Bustani inayo kaliwa.

التفاسير:

external-link copy
16 : 53

إِذۡ يَغۡشَى ٱلسِّدۡرَةَ مَا يَغۡشَىٰ

Kilipo ufunika huo Mkunazi hicho kilicho ufunuika. info

Vikafunikwa na kuzibwa, kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu, visio weza kuelezwa.

التفاسير:

external-link copy
17 : 53

مَا زَاغَ ٱلۡبَصَرُ وَمَا طَغَىٰ

Jicho halikuhangaika wala halikuruka mpaka. info

Jicho la Muhammad halikubabaika kwa aliyo yaona, na wala hakukiuka mpaka ya aliyo amrishwa kwa kuona kwake huko.

التفاسير:

external-link copy
18 : 53

لَقَدۡ رَأَىٰ مِنۡ ءَايَٰتِ رَبِّهِ ٱلۡكُبۡرَىٰٓ

Kwa yakini aliona katika Ishara kubwa kabisa za Mola wake Mlezi. info

Hakika ameona mengi katika Ishara za Mwenyezi Mungu na maajabu yake makubwa makubwa.

التفاسير:

external-link copy
19 : 53

أَفَرَءَيۡتُمُ ٱللَّٰتَ وَٱلۡعُزَّىٰ

Je! Mmemuona Lata na Uzza? info

Je! Mmeyajua hayo, na mkayafikiri ya kina Lata na Uzza?

التفاسير:

external-link copy
20 : 53

وَمَنَوٰةَ ٱلثَّالِثَةَ ٱلۡأُخۡرَىٰٓ

Na Manaat, mwingine wa tatu? info

Na Manata, huyo mwengine wa tatu, mlio wafanya kuwa ni miungu wa kuwaabudu?

التفاسير:

external-link copy
21 : 53

أَلَكُمُ ٱلذَّكَرُ وَلَهُ ٱلۡأُنثَىٰ

Je! Nyinyi mnao wana wanaume na Yeye ndio awe na wanawake? info

Mkagawa, nyinyi muwe na watoto wa kiume, na mkamfanyia Mwenyezi Mungu awe na watoto wa kike!

التفاسير:

external-link copy
22 : 53

تِلۡكَ إِذٗا قِسۡمَةٞ ضِيزَىٰٓ

Huo ni mgawanyo wa dhulma! info

Huo basi ni ugawaji wa dhulma, mnamgawia Mwenyezi Mungu kile mnacho kichukia nyinyi wenyewe!

التفاسير:

external-link copy
23 : 53

إِنۡ هِيَ إِلَّآ أَسۡمَآءٞ سَمَّيۡتُمُوهَآ أَنتُمۡ وَءَابَآؤُكُم مَّآ أَنزَلَ ٱللَّهُ بِهَا مِن سُلۡطَٰنٍۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّ وَمَا تَهۡوَى ٱلۡأَنفُسُۖ وَلَقَدۡ جَآءَهُم مِّن رَّبِّهِمُ ٱلۡهُدَىٰٓ

Hayo hayakuwa ila ni majina mliyo wapa nyinyi na baba zenu. Mwenyezi Mungu hakuleta uthibitisho wowote juu ya hayo. Hawafuati ila dhana tu na kipendacho nafsi. Na kwa yakini uwongofu ulikwisha wafikia kutoka kwa Mola wao Mlezi. info

Hayo masanamu yenu si chochote ila ni majina tu yasiyo na maana yoyote ya kiungu. Mmeyatunga nyinyi na baba zenu kwa kufuata pumbao lenu la upotovu. Mwenyezi Mungu hakuteremsha nayo hoja yoyote ya kusadikisha huo uzushi wenu mnao wadaia. Na hawa hawafuati ila ni dhana tu, na kipendacho nyoyo zao zilio potoka na kuacha maumbile yaliyo sawa. Na hakika yalikwisha wajia kutoka kwa Mola wao Mlezi yenye uwongofu, laiti wangeli ufuata huo!

التفاسير:

external-link copy
24 : 53

أَمۡ لِلۡإِنسَٰنِ مَا تَمَنَّىٰ

Ati mtu anakipata kila anacho kitamani? info

Mwanaadamu hapati kila anacho kitamani, ya kupata uombezi wa haya masanamu au mengineyo anayo yatamani kwa nafsi yake.

التفاسير:

external-link copy
25 : 53

فَلِلَّهِ ٱلۡأٓخِرَةُ وَٱلۡأُولَىٰ

Mwenyezi Mungu tu ndiye Mwenye dunia na Akhera. info

Kwani mambo yote, ya duniani na Akhera, ni ya Mwenyezi Mungu peke yake.

التفاسير:

external-link copy
26 : 53

۞ وَكَم مِّن مَّلَكٖ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ لَا تُغۡنِي شَفَٰعَتُهُمۡ شَيۡـًٔا إِلَّا مِنۢ بَعۡدِ أَن يَأۡذَنَ ٱللَّهُ لِمَن يَشَآءُ وَيَرۡضَىٰٓ

Na wako Malaika wangapi mbinguni, ambao uombezi wao hautafaa chochote isipo kuwa baada ya Mwenyezi Mungu kutoa idhini kwa amtakaye na kumridhia. info

Na malaika wengi wa mbinguni, juu ya ubora wa vyeo vyao, haufai kitu uombezi wao isipo kuwa baada ya kupewa idhini huyo mwombezi na Mwenyewe Mtukufu, na kumridhia huyo mwenye kuombewa.

التفاسير:

external-link copy
27 : 53

إِنَّ ٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ لَيُسَمُّونَ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةَ تَسۡمِيَةَ ٱلۡأُنثَىٰ

Hakika wasio amini Akhera bila ya shaka wao ndio wanawaita Malaika kwa majina ya kike. info

Hakika hao wasio iamini Akhera ndio bila ya shaka wanao sema kuwa Malaika ni wanawake. Wanasema: Malaika ni mabinti wa Mwenyezi Mungu!

التفاسير:

external-link copy
28 : 53

وَمَا لَهُم بِهِۦ مِنۡ عِلۡمٍۖ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّۖ وَإِنَّ ٱلظَّنَّ لَا يُغۡنِي مِنَ ٱلۡحَقِّ شَيۡـٔٗا

Nao hawana ujuzi wowote kwa hayo isipo kuwa wanafuata dhana tu. Na dhana haisaidii chochote mbele ya haki. info

Na kwa kauli hii hawana ujuzi wowote. Hawafuati kitu ila dhana zao tu zilio potoka, na dhana haifai kitu mbele ya haki.

التفاسير:

external-link copy
29 : 53

فَأَعۡرِضۡ عَن مَّن تَوَلَّىٰ عَن ذِكۡرِنَا وَلَمۡ يُرِدۡ إِلَّا ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا

Basi mwachilie mbali anaye upa kisogo ukumbusho wetu, na wala hataki ila maisha ya dunia. info

Basi jitenge nao hao makafiri walio ipuuza Qur'ani na ikawa hamu yao si chochote ila uhai wa duniani tu, wakiyakataa yenye maslaha nao.

التفاسير:

external-link copy
30 : 53

ذَٰلِكَ مَبۡلَغُهُم مِّنَ ٱلۡعِلۡمِۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعۡلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِۦ وَهُوَ أَعۡلَمُ بِمَنِ ٱهۡتَدَىٰ

Huo ndio mwisho wao wa ujuzi. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anaye mjua zaidi mwenye kuipotea njia yake, na Yeye ndiye anaye mjua zaidi mwenye kuongoka. info

Hayo wanayo yafuata katika itikadi zao, na vitendo vyao ndio ukomo walio yafikilia katika ilimu. Hakika Mola wako Mlezi anamjua vyema anaye shikilia upotovu, na anamjua vyema aliye elekea kupokea uwongofu.

التفاسير:

external-link copy
31 : 53

وَلِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ لِيَجۡزِيَ ٱلَّذِينَ أَسَٰٓـُٔواْ بِمَا عَمِلُواْ وَيَجۡزِيَ ٱلَّذِينَ أَحۡسَنُواْ بِٱلۡحُسۡنَى

Ni vya Mwenyezi Mungu vyote viliomo mbinguni na viliomo katika ardhi, ili awalipe walio tenda ubaya kwa waliyo yatenda, na walio tenda mema awalipe mema. info

Na ni vya Mwenyezi Mungu pekee vyote viliomo katika mbingu na ardhi, kwa kuviumba na kuvidabiri, ili awalipe walio potea wenye kufanya viovu vitendo vyao, na awalipe walio hidika watu wema kwa malipo yaliyo mema.

التفاسير:

external-link copy
32 : 53

ٱلَّذِينَ يَجۡتَنِبُونَ كَبَٰٓئِرَ ٱلۡإِثۡمِ وَٱلۡفَوَٰحِشَ إِلَّا ٱللَّمَمَۚ إِنَّ رَبَّكَ وَٰسِعُ ٱلۡمَغۡفِرَةِۚ هُوَ أَعۡلَمُ بِكُمۡ إِذۡ أَنشَأَكُم مِّنَ ٱلۡأَرۡضِ وَإِذۡ أَنتُمۡ أَجِنَّةٞ فِي بُطُونِ أُمَّهَٰتِكُمۡۖ فَلَا تُزَكُّوٓاْ أَنفُسَكُمۡۖ هُوَ أَعۡلَمُ بِمَنِ ٱتَّقَىٰٓ

Ambao wanajiepusha na madhambi makuu na vitendo vichafu, isipo kuwa makosa khafifu. Hakika Mola wako Mlezi ni Mkunjufu wa maghfira, naye anakujueni sana tangu alipo kuumbeni kutoka kwenye ardhi, na mlipo kuwa mimba matumboni mwa mama zenu. Basi msijisifu usafi. Yeye anamjua sana mwenye kujikinga na maovu. info

Wema hao ndio wale wanao jitenga na madhambi yenye adhabu kubwa kubwa, na yanayo chukiza mno. Lakini Mwenyezi Mungu husamehe dhambi ndogo ndogo. Hakika Mola wako Mlezi ni Mkuu wa kughufiria, naye anajua vyema hali zenu. Kwani Yeye ndiye aliye kuumbeni kutokana na ardhi, na mlipo kuwa mimba matumboni mwa mama zenu katika hali zenu mbali mbali za kukua na kugeuka. Basi msikae mkijisifu nafsi zenu kuwa mmesafika kwa kujigamba na kujifakhari. Na Yeye ndiye Mjuzi mkubwa kabisa wa kila mwenye kumcha na akajisafisha nafsi yake kweli kweli kwa uchamngu wake.

التفاسير:

external-link copy
33 : 53

أَفَرَءَيۡتَ ٱلَّذِي تَوَلَّىٰ

Je! Umemwona yule aliye geuka? info

Je! Umezingatia ukamwona anaye puuza kuifuata Haki,

التفاسير:

external-link copy
34 : 53

وَأَعۡطَىٰ قَلِيلٗا وَأَكۡدَىٰٓ

Na akatoa kidogo, kisha akajizuia? info

Na akatoa kidogo katika mali, na khalafu akakata kabisa kutoa?

التفاسير:

external-link copy
35 : 53

أَعِندَهُۥ عِلۡمُ ٱلۡغَيۡبِ فَهُوَ يَرَىٰٓ

Je! Anayo huyo ilimu ya ghaibu, basi ndio anaona? info

Je! Huyo anayo ilimu ya kujua mambo ya ghaibu, basi kwa hivyo ndio anayajua yanayo mpelekea kuiacha kuifuata Haki, na akafanya ubakhili wa mali?

التفاسير:

external-link copy
36 : 53

أَمۡ لَمۡ يُنَبَّأۡ بِمَا فِي صُحُفِ مُوسَىٰ

Au hakuambiwa yaliyomo katika Vitabu vya Musa? info

Kwani huyo hakuambiwa yaliomo katika Vitabu vya Musa

التفاسير:

external-link copy
37 : 53

وَإِبۡرَٰهِيمَ ٱلَّذِي وَفَّىٰٓ

Na vya Ibrahimu aliye timiza ahadi? info

Na Ibrahim, aliye fika ukomo wa kutimiza aliyo agana na Mwenyezi Mungu,

التفاسير:

external-link copy
38 : 53

أَلَّا تَزِرُ وَازِرَةٞ وِزۡرَ أُخۡرَىٰ

Ya kwamba hakika nafsi iliyo beba madhambi haibebi madhambi ya mwengine? info

Ya kwamba hapana mtu ataye mbebea dhambi mwenginewe?

التفاسير:

external-link copy
39 : 53

وَأَن لَّيۡسَ لِلۡإِنسَٰنِ إِلَّا مَا سَعَىٰ

Na ya kwamba hatapata mtu ila aliyo yafanya mwenyewe? info

Na kwamba mtu hapati ila malipo ya vitendo vyake mwenyewe.

التفاسير:

external-link copy
40 : 53

وَأَنَّ سَعۡيَهُۥ سَوۡفَ يُرَىٰ

Na kwamba vitendo vyake vitaonekana? info

Na kwamba vitendo vyake vitakuja tangazwa, na ataviona Siku ya Kiyama, iwe ni kumtukuza mtenda mema, na kumkebehi mtenda maovu.

التفاسير:

external-link copy
41 : 53

ثُمَّ يُجۡزَىٰهُ ٱلۡجَزَآءَ ٱلۡأَوۡفَىٰ

Kisha ndio atalipwa malipo yake kwa ukamilifu. info

Kisha kila mtu atalipwa malipo anayo stahiki.

التفاسير:

external-link copy
42 : 53

وَأَنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ ٱلۡمُنتَهَىٰ

Na kwamba kwao Mola wako Mlezi ndio mwisho. info

Na kwamba kwa hakika ni kwa Mola wako Mlezi, wala si kwa mwenginewe, ndio miadi ya kurejea.

التفاسير:

external-link copy
43 : 53

وَأَنَّهُۥ هُوَ أَضۡحَكَ وَأَبۡكَىٰ

Na kwamba Yeye ndiye anaye leta kicheko na kilio. info

Na Yeye peke yake ni Mwenye uweza wa kuufanya uso uonyeshe furaha au maudhiko, na pia ni Mwenye kuziumba sababu za starehe na dhiki.

التفاسير:

external-link copy
44 : 53

وَأَنَّهُۥ هُوَ أَمَاتَ وَأَحۡيَا

Na kwamba Yeye ndiye anaye fisha na kuhuisha. info

Na hakika ni Yeye, ndiye Mwenye kuondoa uhai, na kuuleta.

التفاسير:

external-link copy
45 : 53

وَأَنَّهُۥ خَلَقَ ٱلزَّوۡجَيۡنِ ٱلذَّكَرَ وَٱلۡأُنثَىٰ

Na kwamba Yeye ndiye aliye umba jozi, dume na jike info

Na Yeye ndiye aliye umba vitu kwa jozi, yaani dume na jike, binaadamu na wanyama,

التفاسير:

external-link copy
46 : 53

مِن نُّطۡفَةٍ إِذَا تُمۡنَىٰ

Kutokana na mbegu ya uzazi inapo miminwa. info

Kutokana na manii yanayo miminwa. Makusudio ya Aya hii tukufu ni kuonyesha uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwamba Yeye ameumba waume na wake katika wanaadamu na wanyama wote kutokana na tone ya manii ambayo humo humo mna ume na uke. Na juu ya udogo wake na udhaifu wake ndio chemchem ya uhai. Umuujiza wa Qur'ani unadhihirika katika Aya hii tukufu ukikumbuka kuwa ulimwengu ulikuwa haujui mpaka hivi karibu kuwa katika maji ya mwanamume ndio zimo mbegu "sperms" na katika maji ya mwanamke mna vijiyai "ova", ndio vikikutana vijidudu vya manii ya mwanamume na vijiyai vya mwanamke vikawa kitu kimoja ndio hiyo huwa mimba. Ukweli huu ulitajwa na Qur'ani kabla ya kuvumbuliwa na ilimu za Sayansi.

التفاسير:

external-link copy
47 : 53

وَأَنَّ عَلَيۡهِ ٱلنَّشۡأَةَ ٱلۡأُخۡرَىٰ

Na kwamba ni juu yake ufufuo mwengine. info

Na juu yake Yeye ndio kufufua baada ya kifo.

التفاسير:

external-link copy
48 : 53

وَأَنَّهُۥ هُوَ أَغۡنَىٰ وَأَقۡنَىٰ

Na kwamba ni Yeye ndiye anaye tosheleza na kukinaisha. info

Na Yeye ndiye anaye toa kinacho tosheleza, na akaridhisha kwa kinacho kinaisha na cha kuweka akiba.

التفاسير:

external-link copy
49 : 53

وَأَنَّهُۥ هُوَ رَبُّ ٱلشِّعۡرَىٰ

Na kwamba hakika Yeye ndiye Mola Mlezi wa nyota ya Shii'ra. info

Na hakika Yeye ndiye Mola Mlezi wa hii nyota kubwa inayo itwa Shii'ra (Sirius, Dog Star). Makusudio hapa ni Nyota hiyo inayo itwa Ash-shi'ra Alyamaaniya, au wanavyo ita Wazungu Sirius au Dog Star. Nyota hii inang'ara kwa nguvu zaidi kuliko nyota zote ziliomo katika kikundi cha nyota kinacho itwa Alkalbu l-akbar, kwa Kizungu Canis Major au Greater Dog. Nyota hiyo ndiyo inayo zagaa sana mbinguni, na huonekana kusini ya mstari wa kati wa mbinguni kiasi ya daraja 18. Na kwa jina hilo la Nyota ya Mbwa ikijuulikana hata miaka elfu tatu ilio pita. Katika mabaki ya michoro ya Mafirauni wa Misri imeashiriwa pia. Mwenyezi Mungu ameitaja khasa kwa kuwa Waarabu walikuwa wakiiabudu hapo kale, na pia Wamisri wa zamani, kwani kutokea kwake upande wa mashariki katikati ya mwezi wa Julai kabla ya kuchomoza jua kulikuwa kunawafikiana na wakati wa mafuriko ya Misri ya kati, yaani katika tukio muhimu kabisa katika ulimwengu huo wa kale. Na tukio hili huenda ndilo lilio fanya kuanzisha kuwekea kiwango urefu wa mwaka katika dunia nzima. Kwani kudhihiri Nyota ya Shiira kabla ya kuchomoza jua hakutokei ila mara moja tu katika mwaka. Basi huu ndio mwanzo wa mwaka mpya.

التفاسير:

external-link copy
50 : 53

وَأَنَّهُۥٓ أَهۡلَكَ عَادًا ٱلۡأُولَىٰ

Na kwamba Yeye ndiye aliye waangamiza A'di wa kwanza, info

Na Yeye ndiye aliye wateketeza kina A'di wa mwanzo, kaumu ya Nabii Hudi. Na akawateketeza Thamudi, kaumu ya Nabii Saleh. Hakuwabakisha.

التفاسير:

external-link copy
51 : 53

وَثَمُودَاْ فَمَآ أَبۡقَىٰ

Na Thamudi hakuwabakisha, info

Na akawateketeza Thamudi, kaumu ya Nabii Saleh. Hakuwabakisha.

التفاسير:

external-link copy
52 : 53

وَقَوۡمَ نُوحٖ مِّن قَبۡلُۖ إِنَّهُمۡ كَانُواْ هُمۡ أَظۡلَمَ وَأَطۡغَىٰ

Na kabla yao kaumu ya Nuhu. Na hao hakika walikuwa ni madhaalimu zaidi, na waovu zaidi; info

Na aliwaangamiza kaumu ya Nuhu kabla ya kuwaangamiza A'di na Thamudi. Hakika hao walikuwa wamekithiri kudhulumu, na wamezidi kwa uasi kuliko A'di na Thamudi.

التفاسير:

external-link copy
53 : 53

وَٱلۡمُؤۡتَفِكَةَ أَهۡوَىٰ

Na miji iliyo pinduliwa, ni Yeye aliye ipindua. info

Na miji ya kaumu Lut'i iliyo pinduliwa juu chini, ni Yeye Mwenyezi Mungu ndiye aliye ipindua.

التفاسير:

external-link copy
54 : 53

فَغَشَّىٰهَا مَا غَشَّىٰ

Vikaifunika vilivyo funika. info

Akaizunguka kwa kuiadhibu kama alivyo izunguka.

التفاسير:

external-link copy
55 : 53

فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكَ تَتَمَارَىٰ

Basi neema gani ya Mola wako Mlezi unayo ifanyia shaka? info

Basi katika neema za Mola wako Mlezi una shaka nayo ipi?

التفاسير:

external-link copy
56 : 53

هَٰذَا نَذِيرٞ مِّنَ ٱلنُّذُرِ ٱلۡأُولَىٰٓ

Hili ni Onyo katika maonyo yale yale ya zamani. info

Hii Qur'ani ni onyo katika jinsi ya yale yale maonyo ya kale waliyo onywa kwayo watu walio tangulia.

التفاسير:

external-link copy
57 : 53

أَزِفَتِ ٱلۡأٓزِفَةُ

Kiyama kimekaribia! info

Kiyama kimekaribia;

التفاسير:

external-link copy
58 : 53

لَيۡسَ لَهَا مِن دُونِ ٱللَّهِ كَاشِفَةٌ

Hapana wa kukifichua isipo kuwa Mwenyezi Mungu. info

Na wala hapana wa kuujuulisha wakati kitapo tokea ila mwenyewe Mwenyezi Mungu.

التفاسير:

external-link copy
59 : 53

أَفَمِنۡ هَٰذَا ٱلۡحَدِيثِ تَعۡجَبُونَ

Je! Mnayastaajabia maneno haya? info

Hivyo nyinyi mnapinga kila la kweli? Na mnaistaajabia kwa kuikaataa hii Qur'ani?

التفاسير:

external-link copy
60 : 53

وَتَضۡحَكُونَ وَلَا تَبۡكُونَ

Na mnacheka, wala hamlii? info

Na mnacheka kwa kejeli na maskhaara, wala hamlii kama wafanyavyo wenye yakini,

التفاسير:

external-link copy
61 : 53

وَأَنتُمۡ سَٰمِدُونَ

Nanyi mmeghafilika? info

Nanyi mmo katika pumbao na kutakabari?

التفاسير:

external-link copy
62 : 53

فَٱسۡجُدُواْۤ لِلَّهِۤ وَٱعۡبُدُواْ۩

Basi msujudieni Mwenyezi Mungu, na mumuabudu. info

Basi msujudieni Mwenyezi Mungu aliye iteremsha Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu wote, na muabuduni Yeye tu peke yake Mwenye kutukuka kwa utukufu wake.

التفاسير: