Kur'an-ı Kerim meal tercümesi - Savahili Dili Tercüme - Ali Muhsin Al-Barvani

external-link copy
71 : 11

وَٱمۡرَأَتُهُۥ قَآئِمَةٞ فَضَحِكَتۡ فَبَشَّرۡنَٰهَا بِإِسۡحَٰقَ وَمِن وَرَآءِ إِسۡحَٰقَ يَعۡقُوبَ

Na mkewe alikuwa kasimama wima, akacheka. Basi tukambashiria (kuzaliwa) Is-haq, na baada ya Is-haq Yaaqub. info

Na mkewe alikuwa kasimama karibu akisikia maneno yao. Akacheka kwa furaha ya kuwa mwenyewe Lut', ambaye ni mtoto wa ndugu wa mumewe, atasalimika. Basi Sisi tulimbashiria kwa ndimi za wale Malaika kuwa atamzalia mumewe Ibrahimu mtoto mwanamume ataye itwa Is-haq, na huyo mtoto ataishi, na baadae Is-haq atampata Yaaqub.

التفاسير: