Kur'an-ı Kerim meal tercümesi - Savahili Dilinde Tercüme - Abdullah Muhammed ve Nasır Hamiys

Sayfa numarası:close

external-link copy
31 : 7

۞ يَٰبَنِيٓ ءَادَمَ خُذُواْ زِينَتَكُمۡ عِندَ كُلِّ مَسۡجِدٖ وَكُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ وَلَا تُسۡرِفُوٓاْۚ إِنَّهُۥ لَا يُحِبُّ ٱلۡمُسۡرِفِينَ

Enyi wanadamu! Kuweni, kila mnapotekeleza Swala, katika hali ya pambo linalokubalika kisheria la nguo zinazofinika tupu zenu na muwe katika hali ya usafi, utohara na mfano wake. Na kuleni na kunyweni katika vizuri Alivyowapa Mwenyezi Mungu, wala msikiuke mipaka ya wastani, kwani Mwenyezi Mungu Hawapendi wakiukaji wenye kupitsha kiasi katika vyakula na vinywaji na mengineyo. info
التفاسير:

external-link copy
32 : 7

قُلۡ مَنۡ حَرَّمَ زِينَةَ ٱللَّهِ ٱلَّتِيٓ أَخۡرَجَ لِعِبَادِهِۦ وَٱلطَّيِّبَٰتِ مِنَ ٱلرِّزۡقِۚ قُلۡ هِيَ لِلَّذِينَ ءَامَنُواْ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا خَالِصَةٗ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۗ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ ٱلۡأٓيَٰتِ لِقَوۡمٖ يَعۡلَمُونَ

Sema, ewe Mtume, uwaambie hao wajinga miongoni mwa washirikina, «Ni nani aliyewaharamishia vazi zuri ambalo Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Amelifanya kuwa ni pambo kwenu? Na ni nani Aiyewaharamishia kujistarehesha kwa chakula kizuri cha halali kilichoruzukiwa na Mwenyezi Mungu?» Sema, ewe Mtume, uwaambie hawa washirikina, «Kwa hakika vile alivyoviruhusu Mwenyezi mungu, miongoni mwa mavazi na vitu vizuri miongoni mwa vyakula na vinywaji, ni haki kwa walioamini pamoja na wengineo katika maisha ya ulimwenguni, na ni haki kwa walioamini peke yao Siku ya Kiyama. Maelezo kama hayo ni mafundisho ambayo Mwenyezi Mungu Anayaelezea kwa watu wenye kuyajua mambo wanayoelezwa na kuyaelewa wanayofafanuliwa. info
التفاسير:

external-link copy
33 : 7

قُلۡ إِنَّمَا حَرَّمَ رَبِّيَ ٱلۡفَوَٰحِشَ مَا ظَهَرَ مِنۡهَا وَمَا بَطَنَ وَٱلۡإِثۡمَ وَٱلۡبَغۡيَ بِغَيۡرِ ٱلۡحَقِّ وَأَن تُشۡرِكُواْ بِٱللَّهِ مَا لَمۡ يُنَزِّلۡ بِهِۦ سُلۡطَٰنٗا وَأَن تَقُولُواْ عَلَى ٱللَّهِ مَا لَا تَعۡلَمُونَ

Sema,ewe Mtume, kuwaambia washirikina hawa, «Hakika Mwenyezi Mungu Ndiye Aliyeyafanya matendo maovu kuwa ni haramu, yale yaliyo waziwazi na yale yaliyofichika, na Ameyakataza maasia yote, na miongoni mwa makubwa zaidi ya maasia ni kuwafanyia watu uadui, kwani hilo liko kando na haki. Na Amewaharamishia kuabudu, pamoja na Mwenyezi Mungu, Aliyetuka, vitu vyingine kati ya vile ambavyo Hakuviteremshia ushahidi wala hoja, kwani afanyaye hayo hana kithibitisho chochote. Na Amewaharamishia kumnasibishia Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, sheria ambayo Hakuipasisha kwa kumzulia urongo,» kama madai ya kwamba Mwenyezi Mungu Ana mwana na kuharamisha baadhi ya vilivyo halali katika mavazi na chakula. info
التفاسير:

external-link copy
34 : 7

وَلِكُلِّ أُمَّةٍ أَجَلٞۖ فَإِذَا جَآءَ أَجَلُهُمۡ لَا يَسۡتَأۡخِرُونَ سَاعَةٗ وَلَا يَسۡتَقۡدِمُونَ

Kila kikundi kilichojikusanya kumkanusha Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na kuwakanusha Mitume Wake, amani iwashukie, kina wakati wa kushukiwa na mateso. Huo wakati, Aliouweka Mwenyezi Mungu wa kuwaangamiza, hawatakawia nao, japokuwa kwa muda mfupi, wala hawataungulia. info
التفاسير:

external-link copy
35 : 7

يَٰبَنِيٓ ءَادَمَ إِمَّا يَأۡتِيَنَّكُمۡ رُسُلٞ مِّنكُمۡ يَقُصُّونَ عَلَيۡكُمۡ ءَايَٰتِي فَمَنِ ٱتَّقَىٰ وَأَصۡلَحَ فَلَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ

Enyi wanadamu! Pindi watakapokuja kwenu Mitume wangu, miongoni mwa watu wenu, wakiwasomea aya za Kitabu changu na kuwafahamisha hoja juu ya ukweli wa yale waliyokuja nayo, basi watiini, kwani mwenye kujikinga na hasira zangu na akayatengeneza matendo yake, hao hawatakuwa na hofu na mateso ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Siku ya Kiyama wala hawatahuzunika juu yale yaliyowapita miongoni mwa hadhi za duniani. info
التفاسير:

external-link copy
36 : 7

وَٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا وَٱسۡتَكۡبَرُواْ عَنۡهَآ أُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ

Na makafiri ambao wamezikanusha hoja za kumpwekesha Mwenyezi Mungu na wakaacha kuzifuata kwa kujiona bora, hao ni watu wa Motoni wenye kukaa milele humo, hawatatoka humo kabisa. info
التفاسير:

external-link copy
37 : 7

فَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّنِ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا أَوۡ كَذَّبَ بِـَٔايَٰتِهِۦٓۚ أُوْلَٰٓئِكَ يَنَالُهُمۡ نَصِيبُهُم مِّنَ ٱلۡكِتَٰبِۖ حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءَتۡهُمۡ رُسُلُنَا يَتَوَفَّوۡنَهُمۡ قَالُوٓاْ أَيۡنَ مَا كُنتُمۡ تَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِۖ قَالُواْ ضَلُّواْ عَنَّا وَشَهِدُواْ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِمۡ أَنَّهُمۡ كَانُواْ كَٰفِرِينَ

Hakuna yoyote aliye na udhalimu zaidi kuliko yule anayemzulia Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, urongo au akazikanusha aya Zake zilizoteremshwa, hao itawafikia sehemu yao ya adhabu waliyoandikiwa katika Al-Lawh( Al-Mhfūd) (Ubao uliohifadhiwa) mpaka atakapowajia Malaika wa mauti pamoja na wasaidizi wake kuzichukua roho zao, watawaambia, «Wako wapi wale mliokuwa mnawaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, kati ya washirika, wategemewa na masanamu, waje wawaokoe na janga lililowafika?» Watasema, «Wametutoroka.» Wakati huo watakiri makosa kwamba wao duniani walikuwa ni wenye kuupinga na kuukanusha upweke wa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka. info
التفاسير: