Kur'an-ı Kerim meal tercümesi - Savahili Dilinde Tercüme - Abdullah Muhammed ve Nasır Hamiys

Sayfa numarası:close

external-link copy
27 : 53

إِنَّ ٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ لَيُسَمُّونَ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةَ تَسۡمِيَةَ ٱلۡأُنثَىٰ

Hakika wale ambao hawaamini kuwa kuna maisha ya Akhera miongoni mwa makafiri wa Kiarabu wala hawafanyi matendo ya kuwafaa huko, wanawaita Malaika vile wanavyowaita wanawake, kwa kuitakidi kwao kuwa Malaika ni wanawake na kuwa wao ni watoto wa kike wa Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
28 : 53

وَمَا لَهُم بِهِۦ مِنۡ عِلۡمٍۖ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّۖ وَإِنَّ ٱلظَّنَّ لَا يُغۡنِي مِنَ ٱلۡحَقِّ شَيۡـٔٗا

Na wao hawana ujuzi wowote ulio sahihi, kuhusu jambo hilo, wenye kusadikisha hayo waliyoyasema. Hawafuati isipokuwa dhana ambayo haifalii kitu na haisimami kabisa mahali pa haki. info
التفاسير:

external-link copy
29 : 53

فَأَعۡرِضۡ عَن مَّن تَوَلَّىٰ عَن ذِكۡرِنَا وَلَمۡ يُرِدۡ إِلَّا ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا

Basi mpuuze yule anaoupa mgongo utajo wetu, nao ni Qur’ani, na asitake chochote isipokuwa uhai wa kilimwengu. info
التفاسير:

external-link copy
30 : 53

ذَٰلِكَ مَبۡلَغُهُم مِّنَ ٱلۡعِلۡمِۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعۡلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِۦ وَهُوَ أَعۡلَمُ بِمَنِ ٱهۡتَدَىٰ

Hali hiyo waliyonayo ndio upeo wa ujuzi wao na lengo lao. Hakika Mola wako Ndiye Anayemjua zaidi aliyepotoka kutoka kwenye njia ya uongofu, na Yeye ndiye Anayemjua zaidi aliyeongoka na akafuata njia ya Uislamu.. Hapa pana onyo kali kwa wenye kuasi na kukataa kukitumia Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kufuata mwenendo wa Mtume Wake, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, wenye kufadhilisha matamanio ya nafsi na hadhi za ulimwenguni juu ya Akhera. info
التفاسير:

external-link copy
31 : 53

وَلِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ لِيَجۡزِيَ ٱلَّذِينَ أَسَٰٓـُٔواْ بِمَا عَمِلُواْ وَيَجۡزِيَ ٱلَّذِينَ أَحۡسَنُواْ بِٱلۡحُسۡنَى

Ni ya Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka, mamlaka ya vilivyoko mbinguni na vilivyoko ardhini, ili Awalipe wale waliokosa kwa kuwatesa kwa maovu waliyoyafanya na Awalipe Pepo wale waliofanya wema, info
التفاسير:

external-link copy
32 : 53

ٱلَّذِينَ يَجۡتَنِبُونَ كَبَٰٓئِرَ ٱلۡإِثۡمِ وَٱلۡفَوَٰحِشَ إِلَّا ٱللَّمَمَۚ إِنَّ رَبَّكَ وَٰسِعُ ٱلۡمَغۡفِرَةِۚ هُوَ أَعۡلَمُ بِكُمۡ إِذۡ أَنشَأَكُم مِّنَ ٱلۡأَرۡضِ وَإِذۡ أَنتُمۡ أَجِنَّةٞ فِي بُطُونِ أُمَّهَٰتِكُمۡۖ فَلَا تُزَكُّوٓاْ أَنفُسَكُمۡۖ هُوَ أَعۡلَمُ بِمَنِ ٱتَّقَىٰٓ

nao ni wale wanaojiepusha na madhambi makubwa na machafu isipokuwa dhambi ndogondogo nazo ni dhambi ndogo ambazo haendelei nazo mwenye kuzifanya, au zile ambazo mja amezifanya kwa nadra. Kwani hizo pamoja na kufanya mambo ya wajibu na kujiepusha na mambo ya haramu, Atayasamehe nayo Mwenyezi Mungu na Atawasitiria. Hakika Mola wako ni Mkunjufu wa msamaha. Yeye Anazijua zaidi hali zenu Alipomuumba baba yenu Ādam kwa mchanga, na mlipokuwa bado hamjazaliwa, mko ndani ya matumbo ya mama zenu. Basi msizitakase nafsi zenu, mkazipamba na mkazipa sifa za uchamungu. Yeye Anamjua zaidi anayeogopa mateso Yake miongoni mwa waja Wake na akajiepusha na kufanya mambo ya kumuasi. info
التفاسير:

external-link copy
33 : 53

أَفَرَءَيۡتَ ٱلَّذِي تَوَلَّىٰ

Unamuonaje, ewe Mtume, yule anayekataa kumtii Mwenyezi Mungu info
التفاسير:

external-link copy
34 : 53

وَأَعۡطَىٰ قَلِيلٗا وَأَكۡدَىٰٓ

na akatoa kidogo katika mali yake kisha akaacha kutoa na akakata hisani yake? info
التفاسير:

external-link copy
35 : 53

أَعِندَهُۥ عِلۡمُ ٱلۡغَيۡبِ فَهُوَ يَرَىٰٓ

Je huyu anayekata kheri yake ya kutoa ana ujuzi wa ghaibu kuwa yeye atamalizikiwa na mali yaliyoko mkononi mwake ndipo akaizuia kheri yake asiitoe, na akawa aliona hilo waziwazi? Mambo si hivyo! Hakika ni kwamba yeye aliacha kutoa sadaka na kufanya kheri, kutenda wema na kuunga kizazi kwa ubahili na uchoyo. info
التفاسير:

external-link copy
36 : 53

أَمۡ لَمۡ يُنَبَّأۡ بِمَا فِي صُحُفِ مُوسَىٰ

Kwani hakupewa habari ya yaliyomo ndani ya kurasa za Taurati info
التفاسير:

external-link copy
37 : 53

وَإِبۡرَٰهِيمَ ٱلَّذِي وَفَّىٰٓ

na nyaraka za Ibrāhīm aliyetekeleza kile alichoamrishwa na akakifikisha? info
التفاسير:

external-link copy
38 : 53

أَلَّا تَزِرُ وَازِرَةٞ وِزۡرَ أُخۡرَىٰ

Kwamba haipatilizwi nafsi yoyote kwa kosa la nafsi nyingine, na mzigo wake hakuna yoyote atakayembebea. info
التفاسير:

external-link copy
39 : 53

وَأَن لَّيۡسَ لِلۡإِنسَٰنِ إِلَّا مَا سَعَىٰ

Na kwamba binadamu hapewi malipo isipokuwa kwa kile alichokichuma yeye mwenyewe kwa juhudi zake. info
التفاسير:

external-link copy
40 : 53

وَأَنَّ سَعۡيَهُۥ سَوۡفَ يُرَىٰ

Na kwamba juhudi zake zitaonekana Akhera, yapambanuliwe mazuri yake na mabaya yake, ili kumkirimu mtenda wema na kumlaumu mfanya mabaya. info
التفاسير:

external-link copy
41 : 53

ثُمَّ يُجۡزَىٰهُ ٱلۡجَزَآءَ ٱلۡأَوۡفَىٰ

kisha binadamu atalipwa kwa juhudi zake malipo yenye kuenea kikamilifu matendo yake yote. info
التفاسير:

external-link copy
42 : 53

وَأَنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ ٱلۡمُنتَهَىٰ

Na kwamba kwa Mola wako, ewe Mtume, ndipo watakapokomea viumbe Vyake vyote Siku ya Kiyama. info
التفاسير:

external-link copy
43 : 53

وَأَنَّهُۥ هُوَ أَضۡحَكَ وَأَبۡكَىٰ

Na kwamba Yeye, Aliyetukuka na kutakasika, Ndiye Anayemfanya Anayemtaka acheke duniani kwa kumfurahisha, na ndiye Anayemfanya Anayemtaka alie kwa kumpa makero. info
التفاسير:

external-link copy
44 : 53

وَأَنَّهُۥ هُوَ أَمَاتَ وَأَحۡيَا

Na kwamba Yeye Ndiye Anayemfisha Anayetaka afe miongoni mwa vuimbe Vyake na Ndiye Anayemuhuisha Anayetaka ahuike miongoni mwao. Basi Yeye Ndiye Aliyepwekeka, kutakasika ni Kwake, kwa kuhuisha na kufisha. info
التفاسير: