Kur'an-ı Kerim meal tercümesi - Savahili Dilinde Tercüme - Abdullah Muhammed ve Nasır Hamiys

Sayfa numarası:close

external-link copy
88 : 20

فَأَخۡرَجَ لَهُمۡ عِجۡلٗا جَسَدٗا لَّهُۥ خُوَارٞ فَقَالُواْ هَٰذَآ إِلَٰهُكُمۡ وَإِلَٰهُ مُوسَىٰ فَنَسِيَ

Hivyo basi Sāmirīy aliwatengenezea Wana wa Isrāīl kutokana na dhahabu kigombe ambacho ni mwili unaotoa sauti ya ng’ombe. Hapo wakasema waliofitinika nacho , «Huyu ndiye mola wenu na mola wa Mūsā aliyemsahau na kughafilika naye. info
التفاسير:

external-link copy
89 : 20

أَفَلَا يَرَوۡنَ أَلَّا يَرۡجِعُ إِلَيۡهِمۡ قَوۡلٗا وَلَا يَمۡلِكُ لَهُمۡ ضَرّٗا وَلَا نَفۡعٗا

Je, hawaoni hawa walioabudu kigombe kwamba hicho hakianzi kusema nao wala hakiwapi jawabu na hakiwezi kuwaondolea madhara wala kuwaletea manufaa? info
التفاسير:

external-link copy
90 : 20

وَلَقَدۡ قَالَ لَهُمۡ هَٰرُونُ مِن قَبۡلُ يَٰقَوۡمِ إِنَّمَا فُتِنتُم بِهِۦۖ وَإِنَّ رَبَّكُمُ ٱلرَّحۡمَٰنُ فَٱتَّبِعُونِي وَأَطِيعُوٓاْ أَمۡرِي

Kwa kweli, Hārūn aliwaambia Wana wa Isrāīl kabla Mūsā hajarudi kuwajia, «Enyi watu wangu, hakika nyinyi mumetahiniwa na huyu kigombe, ili aonekana wazi mwenye Imani miongoni mwenu apate kujitenga na mwenye kukanusha. Kwa hakika Mola wenu ni Al-Rahmān (Mwingi wa Rehema) si mwingine. Basi nifuateni katika lile ninalowaitia la kumuabudu Mwenyezi Mungu na muitii amri yangu katika kufuata sheria Yake.» info
التفاسير:

external-link copy
91 : 20

قَالُواْ لَن نَّبۡرَحَ عَلَيۡهِ عَٰكِفِينَ حَتَّىٰ يَرۡجِعَ إِلَيۡنَا مُوسَىٰ

Walisema wenye kuabudu kigombe miongoni mwao, «Hatutaacha kusimama kukiabudu kigombe mpaka Mūsā arudi kwetu.» info
التفاسير:

external-link copy
92 : 20

قَالَ يَٰهَٰرُونُ مَا مَنَعَكَ إِذۡ رَأَيۡتَهُمۡ ضَلُّوٓاْ

Mūsā akasema kumwambia ndugu yake Hārūn, «Ni jambo gani lililokuzuia ulipowaona wamepotea na kuwa kando na Dini yao info
التفاسير:

external-link copy
93 : 20

أَلَّا تَتَّبِعَنِۖ أَفَعَصَيۡتَ أَمۡرِي

usinifuate ukawa na mimi na ukawaacha? Je, umeasi amri yangu niliyokuamrisha kwayo ya kushika mahali pangu na kutengeneza baada ya mimi kuondoka? info
التفاسير:

external-link copy
94 : 20

قَالَ يَبۡنَؤُمَّ لَا تَأۡخُذۡ بِلِحۡيَتِي وَلَا بِرَأۡسِيٓۖ إِنِّي خَشِيتُ أَن تَقُولَ فَرَّقۡتَ بَيۡنَ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ وَلَمۡ تَرۡقُبۡ قَوۡلِي

Kisha Mūsā alishika ndevu za Hārūn na kichwa chake akawa amvuta upande wake. Hārūn akamwambia, «Ewe mwana wa mamangu, usinishike ndevu zangu wala nywele za kichwa changu! Mimi niliogopa, lau niliwaacha na nikakutana na wewe, usije ukasema, «Umewagawanya Wana wa Isrāīl na hukutunza wasia wangu wa kukaa nao vizuri.» info
التفاسير:

external-link copy
95 : 20

قَالَ فَمَا خَطۡبُكَ يَٰسَٰمِرِيُّ

Mūsā akasema kumwambia Sāmirīy, «Una jambo gani, ewe Sāmirīy? Na ni lipi lililokupelekea kufanya hilo ulilolifanya? info
التفاسير:

external-link copy
96 : 20

قَالَ بَصُرۡتُ بِمَا لَمۡ يَبۡصُرُواْ بِهِۦ فَقَبَضۡتُ قَبۡضَةٗ مِّنۡ أَثَرِ ٱلرَّسُولِ فَنَبَذۡتُهَا وَكَذَٰلِكَ سَوَّلَتۡ لِي نَفۡسِي

Sāmirīy akasema, «Nilimuona ambaye hawakumuona, naye ni Jibrili, amani imshukiye, juu ya farasi, wakati walipotoka baharini na Fir'awn akazamishwa na askari wake, hapo niliteka kwa kitanga changu cha mkono mchanga wa athari ya kwato za farasi wa Jibrili nikaurusha kwenye pambo ambalo kwalo nimetengeneza kigombe, kikawa ni kigombe chenye mwili, chenye kutoa sauti ya ng’ombe, na kikawa ni kisirani na mtihani. Kufanya hivyo ndivyo nafsi yangu inayoamrisha maovu ilivyonipambia.» info
التفاسير:

external-link copy
97 : 20

قَالَ فَٱذۡهَبۡ فَإِنَّ لَكَ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ أَن تَقُولَ لَا مِسَاسَۖ وَإِنَّ لَكَ مَوۡعِدٗا لَّن تُخۡلَفَهُۥۖ وَٱنظُرۡ إِلَىٰٓ إِلَٰهِكَ ٱلَّذِي ظَلۡتَ عَلَيۡهِ عَاكِفٗاۖ لَّنُحَرِّقَنَّهُۥ ثُمَّ لَنَنسِفَنَّهُۥ فِي ٱلۡيَمِّ نَسۡفًا

Mūsā akasema kumwambia Sāmirīy, «Basi enda! Mateso yako katika uhai wa duniani ni uishi ukiwa umetengwa na umwambie kila mtu, ‘ Sigusi wala siguswi’, na una agizo huko Akhera la wewe kuadhibiwa na kuteswa, Mwenyezi Mungu Hataenda kinyume na agizo hilo na utalikuta. Na muangalie muabudiwa wako ambaye umesimama kumuabudu, tutamchoma kwa moto kisha tutampeperusha baharini achukuliwe na upepo kusiwe na athari yake yoyote yenye kusalia. info
التفاسير:

external-link copy
98 : 20

إِنَّمَآ إِلَٰهُكُمُ ٱللَّهُ ٱلَّذِي لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۚ وَسِعَ كُلَّ شَيۡءٍ عِلۡمٗا

Kwa kweli, mola wenu, enyi watu, ni Mola Mmoja Ambaye hakuna muabudiwa isipokuwa Yeye, ujuzi Wake umeenea kila kitu. info
التفاسير: