Kur'an-ı Kerim meal tercümesi - Savahili Dilinde Tercüme - Abdullah Muhammed ve Nasır Hamiys

Sayfa numarası:close

external-link copy
89 : 11

وَيَٰقَوۡمِ لَا يَجۡرِمَنَّكُمۡ شِقَاقِيٓ أَن يُصِيبَكُم مِّثۡلُ مَآ أَصَابَ قَوۡمَ نُوحٍ أَوۡ قَوۡمَ هُودٍ أَوۡ قَوۡمَ صَٰلِحٖۚ وَمَا قَوۡمُ لُوطٖ مِّنكُم بِبَعِيدٖ

«Na enyi watu wangu, usiwapelekee uadui wenu kwangu na kunichukia na kuiacha Dini niliyonayo, kufanya ukakamavu na kuendelea na ukanushaji wa Mwenyezi Mungu mlionao. Kwani mkifanya hivyo, yatawapata nyinyi maangamivu kama yaliyowapata watu wa Nūḥ, au watu wa Hūd au watu wa Ṣāliḥ,. Na hawakuwa watu wa Lūṭ, na adhabu iliyowashukia ni mbali na nyinyi, si nchi waliyoishi wala zama walizokuwako. info
التفاسير:

external-link copy
90 : 11

وَٱسۡتَغۡفِرُواْ رَبَّكُمۡ ثُمَّ تُوبُوٓاْ إِلَيۡهِۚ إِنَّ رَبِّي رَحِيمٞ وَدُودٞ

Na ombeni kutoka kwa Mola wenu msamaha wa dhambi zenu, kisha rudini kumtii na endeleeni juu yake. Hakika Mola wangu ni Mwingi wa rehema, ni Mwingi wa mapenzi na mahaba kwa aliyetubia na akarejea Kwake.» Katika hii aya, pana kuthibitisha sifa ya raḥmah (kurehemu) na mawaddah (kupenda) kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kama inavyonasibiana na Yeye, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake. info
التفاسير:

external-link copy
91 : 11

قَالُواْ يَٰشُعَيۡبُ مَا نَفۡقَهُ كَثِيرٗا مِّمَّا تَقُولُ وَإِنَّا لَنَرَىٰكَ فِينَا ضَعِيفٗاۖ وَلَوۡلَا رَهۡطُكَ لَرَجَمۡنَٰكَۖ وَمَآ أَنتَ عَلَيۡنَا بِعَزِيزٖ

Walisema, «Ewe Shu'ayb! Hatuyafahamu mengi unayotwambia, na sisi tunakuona wewe kuwa ni mnyonge kwetu, wewe si miongoni mwa watu wakubwa wala viongozi, na lau sisi si kuwastahi jamaa zako tungalikuua kwa kukupiga mawe.»- Na kundi la jamaa zake lilikuwa ni katika watu wanaofuata mila yao.- «Na wewe huna cheo wala heshima katika nafsi zetu.» info
التفاسير:

external-link copy
92 : 11

قَالَ يَٰقَوۡمِ أَرَهۡطِيٓ أَعَزُّ عَلَيۡكُم مِّنَ ٱللَّهِ وَٱتَّخَذۡتُمُوهُ وَرَآءَكُمۡ ظِهۡرِيًّاۖ إِنَّ رَبِّي بِمَا تَعۡمَلُونَ مُحِيطٞ

Akasema, «Enyi watu wangu! Kwani jamaa zangu ni wenye nguvu zaidi na ni watukufu zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu? Na mumeitupa amri ya Mola wenu, mkaiweka nyuma ya migongo yenu, mkawa hamjilazimishi kufuata amri Zake na hamjiepushi na makatazo Yake. Hakika Mola wangu ni kwa mnayoyafanya Ameyazunguka, hakuna chochote katika matendo yenu kinafichika Kwake hata kama kina uzito wa chungu mdogo, na Atawalipa kwa hizo kwa haraka au baadaye. info
التفاسير:

external-link copy
93 : 11

وَيَٰقَوۡمِ ٱعۡمَلُواْ عَلَىٰ مَكَانَتِكُمۡ إِنِّي عَٰمِلٞۖ سَوۡفَ تَعۡلَمُونَ مَن يَأۡتِيهِ عَذَابٞ يُخۡزِيهِ وَمَنۡ هُوَ كَٰذِبٞۖ وَٱرۡتَقِبُوٓاْ إِنِّي مَعَكُمۡ رَقِيبٞ

«Na enyi watu wangu! Fanyeni mnaloliweza kwa njia yenu na namna yenu. Mimi ni mwenye kuendelea kufanya kwa njia yangu na nikitumia kile Mwenyezi Mungu Amenipa cha kuwalingania nyinyi kwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu. Mtajua ni nani miongoni mwetu, itamjia adhabu yenye kumfanya mnyonge, na ni nani, miongoni mwetu, ni mrongo katika maneno yake: ni mimi au ni nyinyi? Na mngojee kitakachowashukia; mimi ni miongoni mwa wenye kungojea pamoja na nyinyi.» Hili ni onyo kali kwao. info
التفاسير:

external-link copy
94 : 11

وَلَمَّا جَآءَ أَمۡرُنَا نَجَّيۡنَا شُعَيۡبٗا وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥ بِرَحۡمَةٖ مِّنَّا وَأَخَذَتِ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ ٱلصَّيۡحَةُ فَأَصۡبَحُواْ فِي دِيَٰرِهِمۡ جَٰثِمِينَ

Na amri yetu ilipokuja ya kuwaangamiza watu wa Shu'ayb, tulimuokoa mjumbe wetu Shu'ayb na wale walioamini pamoja na yeye kwa rehema yetu. Na wale waliodhulumu walipatwa na ukulele kutoka mbinguni ukawaangamiza na wakawa wako majumbani mwao wamepiga magoti wakiwa ni wafu hawatikisiki. info
التفاسير:

external-link copy
95 : 11

كَأَن لَّمۡ يَغۡنَوۡاْ فِيهَآۗ أَلَا بُعۡدٗا لِّمَدۡيَنَ كَمَا بَعِدَتۡ ثَمُودُ

Kama kwamba wao hawakukaa kwenye nyumba zao wakati wowote. Jueni kwamba watu wa Madyan waliepushwa na rehema ya Mwenyezi Mungu, kwa kuwa Mwenyezi Mungu aliwaangamiza watu wake na akawalaani, kama vile kina Thamūd walivyoepushwa na rehema Yake. Makabila mawili haya yalishirikiana katika kuwa mbali na rehema ya Mwenyezi Mungu na kuangamia. info
التفاسير:

external-link copy
96 : 11

وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا مُوسَىٰ بِـَٔايَٰتِنَا وَسُلۡطَٰنٖ مُّبِينٍ

Hakika tulimtuma Mūsā na dalili zetu za upweke wetu na hoja inayomfahamisha mwenye kuiona na kuitia akilini, kwa moyo wenye siha, kwamba zinatoa dalili ya upweke wa Mwenyezi Mungu na urongo wa kila anayedai uola asiyekuwa Yeye, Aliyetakata na sifa za upungufu na kutukuka. info
التفاسير:

external-link copy
97 : 11

إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ وَمَلَإِيْهِۦ فَٱتَّبَعُوٓاْ أَمۡرَ فِرۡعَوۡنَۖ وَمَآ أَمۡرُ فِرۡعَوۡنَ بِرَشِيدٖ

Tulimtuma Mūsā kwa Fir'awn na wakubwa wa wafuasi wake na watukufu wa watu wake, Fir'awn akakanusha na akawaamuru watu wake wamfuate yeye, wakamtii yeye na wakaenda kinyume cha amri ya Mūsā. Na hakuna uongofu wowote wala muongozo mwema katika amri ya Fir'awn, ni ujinga mtupu, upotevu, ukanushaji na ujeuri. info
التفاسير: